brider mask
New Member
- Sep 23, 2016
- 2
- 1
Uamuzi mzuri sana!,haiwezekani watu Fulani waendelee kuturudisha nyuma tulikotoka sababu ya ushabiki WA kitoto
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haitasaidia kitu chochote kwa sasa ni kupewa adhabu tu ndiyo wataelimikia hukohuko haitijiki hata elimu ya chekechea kwa mtu kujua kufanya hivyo vitendo ni ushenzi.Kwani usicho elewa nini? Yes campain kwenye vyombo vya habari na siku kadhaa kabla ya mechi kuwe na vipeperushi nk. .... inawezekana mkuu
Na wewe weka rekodi sawa. Timu zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana. Wakati mashabiki wanasubiri timu zirejee uwanjani kuanza ngwe ya pili, Simba wakaweka mpira kwapani wakatimua mbio!Naomba rekodi ikae sawa timu iliyowahi kukimbia uwanjani wakati huo NI simba ambayo mpaka wakati wa mapumziko walikuwa wamefungwa mabao mawili kwa bila,walipokwenda kwenye vyumba vya ndani ya uwanja hakukurudi tena uwanjani .HIYO ndiyo stories.
Wanatumia nguvu ya umma.[emoji41] Kwani wao kina nani katika nchi hii kwamba hawaguswi..?
Unamchagulia mtu jinsi y kushangilia?uko kma mwanamke wa kiswahili mpiga danga ili ale.Yako yamekushinda unabaki kushadadia vy watu.Kwani hukumuona msanii wenu jana,kaachia mdomo kama chatu anatega wadudu baada ya simba kusawazisha
Hapa naona Serikali nayo ikipoteza mapato ....View attachment 410879 Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.
Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.
Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.
Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"
.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.
Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.
Nape kasema kuna milango ya kuingilia uwanjani ambayo ilivunjwa kwa upande wa yanga na simba. Sidhani kama Yanga watahusilka na yaliyotokea ndani ya uwanja.Sasa hapo Yanga inaadhibiwa kwasababu gani? Kitendo cha kuzuia mapato ya Yanga kitawapa kiburi Simba ambao bila shaka wangekuwa tayari kugharamia uharibifu uliofanywa na mashabiki wao. Anyway, Azam wametengenezewa fedha za uwanja.
Mmmmmmmm!!!Wakati Al marhum Mzee Karume alipokuwa Rais wa ZNZ aliamuru timu ya Mwadui waondoke haraka ZNZ kwa kucheza rafu uwnjani.Mpira ulikuwa bado kwisha wakapelekwa Airport moja kwa moja bila ya kupitia hotelini
Siku hiyo waliharibu mali za uwanja kwa kiwango gani?Wakati mwinyi yupo rais wa tanzania aliwahi kuhudhuria mechi ya simba na yanga
Ile mechi haikumalizika mwenyekiti wa yanga wakat huo bw tarimba aliamuru timu yake itoke nje kabla ya mpira kwisha
Mwinyi alichukulia ni hali ya mpira tu
Magu angefanyaje...