Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Uwanja sio wa Rais wala waziri hou uwanja ni wa watanzania wote, wakiwemo hao mashabiki wa Simba na Yanga, kutafutwe adhabu mbadala na sio maneno ya kukurupuka tu.
 
Intelijensia ya Polisi haikuweza kuona kuwa vurugu zitatokea na Mali kuharibiwa?
 
Simba na Yanga wawe na viwanja vyao, Marefa wenye mapenzi ya timu hizi wasipewe nafasi kupuliza kipyenga wataleta maafa. Mpira wa kuzuia na kifua ukigusa eneo la mkono ni makusudi ya mchezaji. Lkn pia alikataa goli safi huyu atizamwe.
 
Wakati mwinyi yupo rais wa tanzania aliwahi kuhudhuria mechi ya simba na yanga

Ile mechi haikumalizika mwenyekiti wa yanga wakat huo bw tarimba aliamuru timu yake itoke nje kabla ya mpira kwisha

Mwinyi alichukulia ni hali ya mpira tu

Magu angefanyaje...
Angeamuru Mwenyekit akamatwe hapa kazi tu
 
Weka sawa yanga hakuna mwaka ilifika Uwanjani kecheza na Simba alafu wakatoa timu, ila nakumbuka Simba hawakurudi Uwanjani baada ya mapumziko ii ilikua mwaka 1991 na mbaka wanagomea mchezo timu hizo zilikua hazija Fungana.
 
Ni wakati muafaka sasa Simba na Yanga ziwe na viwanja vyao ili mashabiki wao uchwara wakaharibu miundo mbinu ya timu husika.
Mmesaidiwa kuchezea uwanja wa taifa na bado mnahabu. Shame on you. Wacha mfungiwe sasa.
 
Uwanja wataufungua tu, inatakiwa mechi zichezwe ili ulipie gharama za Matunzo na Ujenzi iitakua ni kwa muda tu.
 
Yanga ndo walivunja viti!?
Kama maamuzi yataambatana Na msukumo wa kisiasa, naona hatari mbele.
Watu wawajibike kwa kadiri ya matendo yao....Yanga wanaadhibiwa kwa kushangilia goli la Tambwe alifunga kwa mguu!?
 
Hiyo tunaita tit for tat!! Natamani hapo aliposema "Rais alitaka adhabu iwe kali zaidi" nilitamani kuijua hiyo adhabu! Kutumia uwanja wa Taifa kwa Simba na Yanga ni ili kupata mapato mengi na kutangaza timu hizo nje ya nchi. Sidhani kama adhabu hiyo ya kuzifungia kuutumia huo uwanja ni sahihi.

Pili swala la kuzuia mapato ya timu hizo liangaliwe kwa umakini maana kuna wachezaji wengi hapo ndipo wanapoponea kwa swala la posho za hapa na pale kama kina Kichuya. Hivyo kuzuia mapato yote na hasa kwa style ya serikali ya Magufuli huenda tathimini hiyo ikachukua muda na baada ya hapo huenda wakaambulia hewa maana tutaambiwa mengi. Swala la kufanyika tathimini mpaka sasa lilitakiwa liwe limeisha. Pia mambo ya vurugu na vitu vya kwenye mipira ya miguu ni la FIFA na huwa wanakasirishwa sana pale serikali inapojiingiza moja kwa moja kama hivi.

Hapo kwenye adhabu Kali nawaza labda alipanga kuzifuta Simba na Yanga nini?

Any way adhabu kama hizi kwenye mataifa yenye misimamo mikali zilikuwa za kawaida na baada ya muda michezo kwenye mataifa hayo ikafutikia mbali!!
mimi nafikiri hili swala kwa serikari wana haki ya kuingilia kwa upande mmoja au mwingine ukiangalia maamuzi yaliyo chukuliwa kwa upande mwingine ni funzo kwa hizi timu zitu kubwa.

YANGA na SIMBA ndiyo timu zenye udhamini mkubwa kwa Tanzania. KWA miaka ya hivi karibuni hizi timu zilitakiwa ziwe kwenye michakato ya kujenga viwanja vyao wenyewe.
SWALA la Mashabiki jana Kuvunja Viti so halal ikizingatiwa uwanja ni Mali ya serikali na sio Mali ya vilabu vya mpira vya Tanzania, Serikali imeingilia kwenye upande Wao. Maswala yaliyo bakia ni maswala ya TFF,

Maamuzi yaliyo tolewa yanaweza yakawa sawa au sio sawa kwa upande mmoja
kuzifungia SIMBA NA YANGA kuto tumia uwanja wa Taifa ni adhabu kubwa kwa upande wa club hizi mbili ikizingatiwa vilabu vya Tanzania vinajiendesha kwa kutegemea map ago ya mlangoni.Pia clubs hizi mbili zina Mashabiki wengi ni ngumu kuwazuia mashabiki, KWA hali ya jana tungewalaumu kwa upande mwingine Polisi .Serikali ilitazame hili kwa jicho jingine Mashabiki tuadhibiwe kwa vitendo tulivyo fanya tubaki hivi adhabu za Mashabiki zibebwe na vilabu vya mpira hatuta viendeleza vilabu vyetu mpira.

MKUU NAUNGANA NA WEWE
NINGETAMANI KUSIKIA TAMKO LA MKUU WA NCHI[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

#Mashabiki_wa_Simba_na_Yanga_Tungejuta_kwa_mbele_ya_mkuu
 
Watatumia uwanja gani? Wekeni njia mbadala za
kutatua matatizo kama ya kadi, kuwaelimisha mashabiki na wakifanya uharibifu basi mzuie pesa zao lakini sio kusema wote waadhibiwe kuto tumia uwanja wa taifa sabb ya wavuta bangi wachache.....

Haya unayoyasema ni kama unawazungumzia watu wasiojitambûa. Lakini mashabiki wote wana akili timamu na wanajua kuwa kufanya vurugu ni kosa la jinai.,,!!! Hawa wote ni wahuni tu na wanatakiwa kuadhibiwa vikali. Taratibu zote wanazijua sema ni ujinga tu basi. Zuia pesa Serikali, Piga wao faini, fungia kutotumia uwanja, viti wavitengeneze, haya yote wafanyiwe ili wakome....!!!!!
 
Mkuu hapo hamna cha kujikwaa wabongo wengi ni wapuuzi sana haswa linapokuja suala utunzaji mali za uma. Refa kuharibu mchezo halina uhusiano na viti. Refa atahukumiwa na wahusika baada ya mchezo. Nakumbuka siku ya ufunguzi ya ule uwanja watu waliiba koki vyooni. Sasa kama hapo utasema bahati mbaya
Utake usiteke hata kama mimi ndiye ningekua Sanya, jana ningeuwa Simba maana hakuna namna, huku nikijua natembelea pikipiki, watu waniahidi gari, na mbumba za kutosha. Urefa nini wananifungia kipindi cha mwaka mmoja, kwa kuzuga ila nikiwa nimekusanya maslahi ya miaka mitano, kwa sanya ni askari hategemei kuishi kwa kazi ya urefa. Kama mnategemea kilichotokea ni bahati mbaya poleni mashabiki wa Simba, wala wanaosimamia mpira mjue kuwa mengine nyie ndiyo chanzo, na mjuwe watu wanapenda mpira kuliko mnavyodhani. Mtu ataachana na mke au mumewe ila sio mapenzi ya Timu yake, angalia mipango mipango yenu isije leta dhahama.
 
agizo halitadumu muda mrefu. siku zote maagizo sahihi hutanguliwa na vikao vya kujadili pro and cons.
 
Kwan Yanga nao walingoa viti? Kwa nini adhabu hii imeihusisha Yanga? Kutaka kufurahisha wote hata km haileti maana? Simba ndio walifanya vurugu, Yanga haihusiki! Hivyo adhabu iwahusu Simba wenyewe!
Yanga walivunja geti wakati wanaingia na walipuliza sawa kwenye vyumba
 
Donald Trump, ulisema Africa bado tunahaja ya kutawaliwa, nilikuelewa sana. Hebu njoo utawale bongo tu, sio Tanzania nzima. Kuna tatizo sana pale
Umeongea vizuri sana mkuu
 
Refa hausiani na ujinga wa watu wetu
Umesahau aluvoibeba yanga dhidi ya coast union akafungiwa??
Utake usiteke hata kama mimi ndiye ningekua Sanya, jana ningeuwa Simba maana hakuna namna, huku nikijua natembelea pikipiki, watu waniahidi gari, na mbumba za kutosha. Urefa nini wananifungia kipindi cha mwaka mmoja, kwa kuzuga ila nikiwa nimekusanya maslahi ya miaka mitano, kwa sanya ni askari hategemei kuishi kwa kazi ya urefa. Kama mnategemea kilichotokea ni bahati mbaya poleni mashabiki wa Simba, wala wanaosimamia mpira mjue kuwa mengine nyie ndiyo chanzo, na mjuwe watu wanapenda mpira kuliko mnavyodhani. Mtu ataachana na mke au mumewe ila sio mapenzi ya Timu yake, angalia mipango mipango yenu isije leta dhahama.
 
Back
Top Bottom