Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Hii timu ikiwezekana ifutwe maana inaonekana kuwa sio raia wa Tanzana kwani sijawawi kuona upuuzi kama huu bongo. Mona wenzo hawavunja viti? ilitokea tena wakati TP MAZEMBE walipokuja wakanunua jezi zao wakaingia na kufanya fujo kama hizi !!!!!!!!!!!!!!!!!!!ifutwe tuu sasa maana hatuna jinsi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Utake usiteke hata kama mimi ndiye ningekua Sanya, jana ningeuwa Simba maana hakuna namna, huku nikijua natembelea pikipiki, watu waniahidi gari, na mbumba za kutosha. Urefa nini wananifungia kipindi cha mwaka mmoja, kwa kuzuga ila nikiwa nimekusanya maslahi ya miaka mitano, kwa sanya ni askari hategemei kuishi kwa kazi ya urefa. Kama mnategemea kilichotokea ni bahati mbaya poleni mashabiki wa Simba, wala wanaosimamia mpira mjue kuwa mengine nyie ndiyo chanzo, na mjuwe watu wanapenda mpira kuliko mnavyodhani. Mtu ataachana na mke au mumewe ila sio mapenzi ya Timu yake, angalia mipango mipango yenu isije leta dhahama.
Askari mbona aliangushwa kizembe vile
 
Wakati mwinyi yupo rais wa tanzania aliwahi kuhudhuria mechi ya simba na yanga

Ile mechi haikumalizika mwenyekiti wa yanga wakat huo bw tarimba aliamuru timu yake itoke nje kabla ya mpira kwisha

Mwinyi alichukulia ni hali ya mpira tu

Magu angefanyaje...

Tarimba Abbas Tarimba tungemvua Uraia tena na ule ushombe shombe hahahah
 
Kuna watu mtaiponda serikali kwa hili lakini mimi naiunga mkono 100%. Watanzania imejaa wajinga wengi sana, viwanja vikiwa hamna wa kwanza kulaumu serikali, sasa vimetengenezwa mnaanza tabia za nyani mnavunja viti makusudi, alafu waafrika wakiitwa nyani wanakua wa kwanza kulalamika, hehehe! hizi tabia ni za myama gani sasa?
Bora umewapasha wanatetea ujinga, uharibufu wote huu bado mtu ana thubutu kuutetea!? Tena kwa hoja na mifano isiyo na mashiko hovyo sana
 
Viti ni vizima tusikuze mambo sehemu za kufungia bolts ni laini sana ukivuta tu kiti kinaachana na bolt lakini vile viti ni vizima tu
Kwa nini ving'olewe? Kwa nini wavitoe sehemu yake na kuvitupa hii tabia lazima itafutiwe tiba adhabu hiyo halitoshi kabisa mkuu,
 
Refa aliingia uwanjani kuchezesha mpira akiwa tayari na maelekezo ya ile mechi ,na yeye ndiyo chanzo cha yote yale hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.
 
Ya refali saanya asipewe adhabu peke pamoja na wale wasaidizi wake wana takiwa wapate adhabu
 
Mi naiponda serkal kwa kutengeneza viti visivyo imara. Ova
Ningeungana na wewe kuiponda serikali kama viti vile vingekuwa kwa ajili ya nyani maana yule ni hayawani chochote angeweza kufanya sio kwa binadam mwenye akili timamu afanye upuuzi huo uiponde serikali hapana mkuu
 
View attachment 410879 Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.

Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.

Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.

Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"

.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.

Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.

Hata Mimi Inanitia Hasira sana Kwa Miafrika Kutaka Maendeleo Lakini Sio Wote Wengine Ni Kama Manyani, Kila Kitu Kizuri Wataharibu. Mfano Nilipokuwa Nikisoma Azania Miaka ya 1989-92 Tulikuwa na Shida Kubwa sana ya Vyoo na Maji. Basi watu wa Denmark kwa Kutumia Shirika Lao la Danida, Wakatujengea Vyoo vizuri na Mabomba ya Maji Masinki, Na Kuweka Shule Mapaa Mapya, Na Kupaka Rangi, Lakini Mwezi haukuisha Utakuta Mishetani isiyojali Imejaza Kokoto na Mawe kwenye Vyoo, Imevunja Koki za Mabomba ya Maji. Imechora Grafidi Kutani, Na Kupasua Vioo Kwa Mawe. Iibakia Nusu hivi Nije Shuleni Na "Kisu Nichome" Hii Mimbwa Nilivyokerwa!

Rais Hapa Hasira yake Naungana Naye na Namwelewa sana, sana, Ila asiwe na Reaction ya Kama Mimi Nilipotaka kuja na Kisu shuleni! Simba na Yanga sidhani wanaweza Kuwakontrol Mashabiki wao, au sidhani Kama wao ndio wanawatuma Kufanya Huu Ushenzi. Mimi Nilidhani, asiruhusu Hasira yake ailekeze Vibaya. Ila from Now On, Waweke adhabu Kali, Na Ikitokea Mtu akifanya Ushenzi wa aina Hii, Iwe ni Kunya katika Vituo vya Mabasi, Iwe Ni kuvunja Viti vya Stadium au Kuharibu shule. Kama Ni mtu Mzima, aende Jela Miaka 20 Bila Huruma, sio rahisi Kukamata wote lakini kama 10 wakikamatwa Ready hand na Kufungwa watatoa somo Nchi Nzima.
Na kama Ni mwanafunzi wa Form 1 na Kuendelea na anavandalize (haribu) Shule. Huyu Ni Kumfukuza na asikanyage shule yoyote Milele, Wengine watapata somo.

Ila Mimi Nampinga Rais Kwa Udictator wa Kisiasa Lakini Kwa Hili Namkubali kwa 1000,000%.
 
Imeelezwa Kuwa Jana Rais Magufuli ameghadhibika sana na Kufoka, Kutokana na Uharibifu Uliofanywa Uwanja wa Taifa na Mashabiki wa Simba na Yanga.

Inanitia Hasira sana Kwa Miafrika Kutaka Maendeleo Lakini Sio Wote Wengine Ni Kama Manyani, Kila Kitu Kizuri Wataharibu. Mfano Nilipokuwa Nikisoma Azania Miaka ya 1989-92 Tulikuwa na Shida Kubwa sana ya Vyoo na Maji. Basi watu wa Denmark kwa Kutumia Shirika Lao la Danida, Wakatujengea Vyoo vizuri na Mabomba ya Maji Masinki, Na Kuweka Shule Mapaa Mapya, Na Kupaka Rangi, Lakini Mwezi haukuisha Utakuta Mishetani isiyojali Imejaza Kokoto na Mawe kwenye Vyoo, Imevunja Koki za Mabomba ya Maji. Imechora Grafidi Kutani, Na Kupasua Vioo Kwa Mawe. Iibakia Nusu hivi Nije Shuleni Na "Kisu Nichome" Hii Mimbwa Nilivyokerwa!

Rais Hapa Hasira yake Naungana Naye na Namwelewa sana, sana, Ila asiwe na Reaction ya Kama Mimi Nilipotaka kuja na Kisu shuleni! Simba na Yanga sidhani wanaweza Kuwakontrol Mashabiki wao, au sidhani Kama wao ndio wanawatuma Kufanya Huu Ushenzi. Mimi Nilidhani, asiruhusu Hasira yake ailekeze Vibaya. Ila from Now On, Waweke adhabu Kali, Na Ikitokea Mtu akifanya Ushenzi wa aina Hii, Iwe ni Kunya katika Vituo vya Mabasi, Iwe Ni kuvunja Viti vya Stadium au Kuharibu shule. Kama Ni mtu Mzima, aende Jela Miaka 20 Bila Huruma, sio rahisi Kukamata wote lakini kama 10 wakikamatwa Ready hand na Kufungwa watatoa somo Nchi Nzima.
Na kama Ni mwanafunzi wa Form 1 na Kuendelea na anavandalize (haribu) Shule. Huyu Ni Kumfukuza na asikanyage shule yoyote Milele, Wengine watapata somo.

Mimi Nampinga Rais Kwa Udictator wa Kisiasa Lakini Kwa Hili Namkubali kwa 1000,000%. Magufuli Hajui Tu watu hatumchukii, Na akiamua Kuweka Nchi ya haki, Na Kuruhusu Uhuru wa Kidemokrasia, 1)Hata shidwa 2020, 2) Atakumbukwa Miaka 2000 Ijayo 3) Atafanikiwa sana na hata wapinzani watamheshimu na Kumsaidia.

Hana haja ya Kuvumilia Ujinga, Anatakiwa Ajenge Nchi Fair, Na Watanzani wajisikie Uhuru. Upepo Utabadilika! Nguvu sio Kuwavuta watu Mh. Rais! Nguvu Ni Kuwafanya watu Kuvutiwa na Wewe na Kukufuata Kila Uendako. Nguvu sio Kuogopesha Watu Mh Rais, Nguvu Ni Kuwafanya watu wakupende, Wakuheshimu Mpaka Waingiwe Hofu ya Kukukosea. Nguvu sio Kuwalazimisha watu Kufanya Uyafanyayo Mh. Rais Nguvu Ni Kuwafanya watu wayapende Uyafanyayo Na Kwa Msukumo Binafsi wakuunge Mkono! Mr. President Do What is Right, Utafanikiwa. It is very hard when you have such Great power to do right to those who sometimes wish you Ill and demagogue against you! But Great people don't opt the easy way out!
 
Kwa hili la kuchezea miundombinu.....

Hata Mimi siwezi kuwaunga mkono wauni .......

Lazima watu tupende kulinda vitu vyetu tulivyovijenga kwa galama......

Huu ni upuuzi hakuna mtu makini anaueweza kuuvumilia......
 
Nilisikia uingereza ufaransa na ubelgij wanapoishi waafrika wengi wanachemsha maji ya kunywa.

Cleanliness is next to Godliness. Siyo tu kuabudu hadharan usifiwe mcha mungu
 
washabiki wa simba ni sawa na ma ccm huwa hayatumii akiri hata kufikiria.

swissme
 
Back
Top Bottom