Hilo angalizo la Magufuli ni la kweli kabisa, maana anaona anayofanya yeye na kufanya siasa pekee yake lakini bado watu hawakujitokeza kujiandikisha kupiga kura. Sasa anajiuliza iwapo atatokea kiongozi mwingine wa ccm aruhusu demokrasia na kisha asifanye kama afanyavyo yeye, ccm itakuwa na hali gani? Katika kipindi Magufuli amejuwa fika kuwa ccm haikubaliki na wananchi ni hiki kitendo cha watu kususia kupiga kura, yeye alitarajia watu watakuwa wengi sana maana anasema wameona maendeleo kwa macho, lakini wapi.