Rais Magufuli atangaza maombolezo ya siku 3, bendera kupepea nusu Mlingoti kufuatia kifo cha Rais wa Burundi, Marehemu Pierre Nkurunziza

Ni vizuri kujaliana,,africa ni moja
Alivyokuwa akiuwa waafrika wenzake hakujua ni vizuri kujaliana.? Tuache unafiki wakati yuko hai kila Jambo baya utasikia "acha ukurunziza" Sasa kafa ndo awe mzuri?

Wakimbizi wamejaa kigoma kutokana na Nkurunziza kuwashambulia 2015 aking'ang'ania madaraka. Akaua zaidi ya 1200 na zaidi ya 40000 kukimbilia kigoma na kwingineko.

Nadhani ni wakati haya madikteta wakifa tuongeze urefu wa milingoti ili viongozi wenye tabia hizi wapate somo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes ni kawaida kutokea kwa nchi nyingine.

Alitufanyia nini sisi kama Tanzania nadhani tafuta Press release ya IKULU jana.

Ile barua wameandika alichotufanyia watanzania.
Hayo yote ni yale ambayo yeye alinufaika kwetu, je alitufanyia kipi cha maana hata kustahili nusu mlingoti.?

Je, ni kawaida hii pia hutokea nchi zingine.?
 
Yes ni kawaida kutokea kwa nchi nyingine.

Alitufanyia nini sisi kama Tanzania nadhani tafuta Press release ya IKULU jana.

Ile barua wameandika alichotufanyia watanzania.
Tuna maslahi makubwa sana ya kiuchumi na Burundi. Tuweke siasa na Corona pembeni
 
Hii ndio tafsiri ya umoja wa East Africa. Magufuli kuongozi bora kwenye hizi nchi.
 
Kuna vifo vinatokea unasikitika.

Sasa Nkurunzinza tunaomboleza nini kama alizarau corona mwenyewe. Hii ni kosa la marehemu wala hatuna sababu ya kuomboleza.

Corona itawatafuna sana viongozi wa Burundi.
Msiba wa kujitakia hauna Kilio, kama umekunywa sumu sasa ya nini uombewe? By Afande Sele (enzi zile kichwani zimo).
 
Kwa huzuni gani niliyonayo nimwombolezee dikteta!!? Hayo ni madikteta yanaombolezeana.
 
kweli mkuu !

kifo hakina baunsa uwe mwema au mbaya ...
 
Hii nchi ni active member wa EAC kwa rais mmojawapo wa nchi members kufariki si jambo dogo kama baadhi ya wachangiaji humu mbavyofikiri na ni utaratibu wa kawaida kabisa.

Ila kwa akili ya watanzania wa sasa wengi hamjui hizi protocol za kimataifa na sintashangaa ukiwaona kina zittu wakikimbilia mahakamani kupinga wakidai benderai rudi juu mlingoti [emoji16]
 
Kwa huzuni gani niliyonayo nimwombolezee dikteta!!? Hayo ni madikteta yanaombolezeana.
Madikteta yaliyokataa uwapo wa COVID19 na baadaye yote yakafa kwa kuugua COVID19 sasa yako Jehenam yote mawili; Nkurunzinza na Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…