Rais Magufuli azindua Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro, aitaka mifuko ya hifadhi kuwekeza kwenye viwanda badala ya majengo

Rais Magufuli azindua Kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro, aitaka mifuko ya hifadhi kuwekeza kwenye viwanda badala ya majengo

mutuku fu wenu anapenda kuabudiwa na hizi ndo IMPACTS ...28 sio mbali
Hiyo ni siku ya uchaguzi wa wabunge na madiwani uraisi watanzania washaamua mitano tena.

We uoni Lissu kaamua kukimbilia Zanzibar mziki wa bara keshauona hana chake.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli anazindua kiwanda cha bidhaa za ngozi kilichopo mkoani Kilimanjaro. Rais ameshafika na kwa sasa ni wimbo wa Taifa kabla ya kuanza shughuli Rasmi. Kuwa nami.

======

TAARIFA FUPI YA MRADI
Mkurugenzi PSSF:
Ujenzi wa mradi huu ni utekelezaji wa maelekezo yako uliyoyatoa tarehe 9 May 2016 uliyoyatoa wakati wa ufunguzi wa majenga ya vitega uchumi wa mifuko ya hifadhi ya jamii jijini Arusha, katika hotuba yako ulituelekeza kuwekeza zaidi katika viwanda badala ya kuwekeza tu katika majengo.

Katika kutekeleza, May 2017 mfuko kwa kushirikiana na Jeshi la magereza tulianzisha kampuni ya ubia inayojulikana Karanga leather Industries company Limited ambayo kwa kwa sasa inajulikana kama Kilimanjaro International Leather Industries yenye mtaji wa bilioni 70 inamilikiwa na mfuko wa PSSF kwa asilimia 86 na Jeshi la Magereza kwa asilimia 14. Jeshi la Magereza likiwa limechangia eneo la kiwanda lenye ekari 25 pamoja na kiwanda cha zamani.

Mfuko wa PSSF unachangia gharama za ujenzi wa majengo, ununuzi wa mashine na mitambo na gharama za uendeshaji. Ujenzi huu unasimamiwa na wataalam wa ndani kupitia taasisi za umma.

Mkandarasi wa ujenzi ni Jeshi la Magereza kwa kiasi cha bilioni 27, mashine na mitambo vimenunuliwa nchini Italy kwa gharama ya Euro milioni 23.6, takribani bilioni 60 zikijumuisha gharama za usafirishaji, ufungaji wa mashine, mafunzo na ushuru wa forodha. Mpaka kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu bilioni 136.


MAGUFULI: Kuanzishwa kwa kiwanda hiki, mimi nina uhakika sasa baada ya mwaka mmoja, miwili tukikutana hata katika kusheherekea, nina uhakika tutakuwa tumevaa viatu vitavyokuwa vimetengenezwa hapa Kilimanjaro.

Wafungwa lazima watumike katika kuzalisha mali, ukifungwa lazima ukatumike vizuri ili ujutie makosa yako ili siku nyingine usifungwe tena na ukishatoka hapa utatoka umeshajua kuzalisha viatu akafungue kiwanda chako. Kufungwa ni sehemu ya mafunzo.

Nizipongeze pension fund zetu, PSSF na bodi yake pamoja na mkurugenzi mmeanza vizuri sana kwa sababu siku za nyuma pension fund zilikuwa zinawekeza kwenye majengo tu na kule ndiko kulikuwa na percentage nikasema masuala ya kuwekeza kwenye majengo uachwe.

Utakuta jengo limejengwa kwa mabilioni, wapangaji wapo nusu tu, faida yake ni ndogo.

Ukiwekeza kwenye viwanda faida yake ni kubwa. Kiwanda hiki kitakuwa kinatoa ajira ya watu elfu 3. Ungejenga jengo lisingetoa ajira ya watu 3,000 na hawa ni wale watakuwa wanafanya permanently hapa. Wale wengine watakaokuwa wanaleta vyakula, ngozi kwa nchi nzima unaweza ukajikuta umetengeneza ajira ya zaidi ya watu milioni 1.

==========

Mwisho Rais Magufuli amezindua kiwanda na kununua viatu kadhaa ikiwemo vya mke wa askofu, mwandishi wa habari nk
Ni makosa makubwa kufanya haya wakati wa uchaguzi NEC mpo wapi?!
 
Nchi inatakiwa kiwanda vya aina mbali mbali tuwauzie watu products na sio raw materials ili tupate faida kubwa sawa jiwe! ila Lissu imekaa vizur inasound good.
Tobo viwanda vyote ni kwa mabeberu. Hafu wananchi wote ni ufukara kama jimboni kwake
 
Yaani bado anataka kwenda kuchimbia fedha za wastaafu kule?
Wamezoea 'kuzibeba' kila watakavyo ndio maana mafao ya wastaafu yanazidi kubinywa kila kukicha!
Bima ya afya nako wameanza kuzichota watakvyo ndio maana huduma ya madawa mengi yameondolewa na kuacha malaria tiu!

haya mambo yanatia hasira sana sana!
 
Shekhe Ponda ahoji Viwanda kufunguliwa wakati wa Kampeni amesema Ile Sera ya Viwanda vya Cherehani nne ni Ulaghai wa kiwango cha hali ya juu
 
PSSSF na NSSF wana pesa ya kufanya miradi, lakini pesa ya kumlipa mfanyakazi aliyetumikia Taifa na kchangia mifuko hiyo kwa miaka Mingi na badae kupoteza ajira na kuendelea kuteseka na familia yake, Hawana..!!

Hovyo sana....
We jamaa wewe nawe, nani kakuambia kua hawana hizo pesa, usi comment kwa kufuata Mkumbo tu halafu ukute wewe mwenyewe hata sio mwajiriwa halafu una bwabwaja, nikupe taarifa tu kwa ninavyofahamu huo ni uwekezaji kama maagizo ya Mhe. Rais ilivyotoa kuwa wawekeze zaidi katika viwanda na suala la mafao kwa wafanyakazi pindi atakapo staafu au kuachishwa kazi wote watapata mafao. Usiandike mambo kama huelewi
 
Tuliambiwa kumejengwa viwanda zaidi ya elfu 6000 na pia mwaka jana tuliambiwa kila mkoa unatakiwa ujenge viwanda 100 kabya ya desemba. kwa maana hiyo mikoa 26 x 100 tunayo viwanda 2600. kwa mwaka jana tu. Sasa wewe unaturudisha nyuma tena kwenye viwanda 202
Tatizo watu hawana data hawana uelewa wanafata mikumbo ndio maana unaona wanaandika bora wameandika nao waonekane wamo
 
Upumbavu mtupu! Mifuko ya jamii inatunza fedha za wafanyakazi ili wanufaike wakistaafu na si fedha za kujenga viwanda ambavyo vinaweza kufa na hivyo kuwakosesha wastaafu haki yao.

Mwambieni Magufuli atafute wawekezaji binafsi wajenge viwanda.
Hivi wewe wa wapi, hivi unaelewa maana ya uwelezaji ww, sasa unataka pesa zikae tu bila kuzunguka, hebu uliza wenzako nini maana ya mzunguko wa fedha, na hapo hapo jiulize je pesa ulizo nazo unakaaga nazo au unatumia upate nyengine, kuwa kama mtu unaejielewa basi usiandike andike tuu, acha Mhe. Rais aendelee na Mitano ili tuwe na viwanda zaidi na maendeleo kwenda mbele. Unajua yapo sema ubishi tu.
 
Hivi wewe wa wapi, hivi unaelewa maana ya uwelezaji ww, sasa unataka pesa zikae tu bila kuzunguka, hebu uliza wenzako nini maana ya mzunguko wa fedha, na hapo hapo jiulize je pesa ulizo nazo unakaaga nazo au unatumia upate nyengine, kuwa kama mtu unaejielewa basi usiandike andike tuu, acha Mhe. Rais aendelee na Mitano ili tuwe na viwanda zaidi na maendeleo kwenda mbele. Unajua yapo sema ubishi tu.
Bado unanuka maziwa ya mama yako, ukikua utaelewa!
 
Back
Top Bottom