figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Rais Mhe. Dkt. John Magufuli leo atazinduzi mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia (Kinyerezi II) Jijini Dar es Salaam.
Mradi huu utaingiza megawatts 240 katika gridi ya Taifa. Matangazo ya moja kwa moja yatarushwa na TBC 1 & Azam Two kuanzia saa 3:30 asubuhi hii.
=================================================
Shughuli imeanza
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM , Humphrey Polepole naye yupo kwenyye uzinduzi huo, ansema mradi huu wa umeme utasaidia Tananzania kufikia kwenye uchumi wa kati mwaka 2025 kwa kuzalisha umeme utakaoendesha viwanda vitakavyochakata mazao ghafi
Rais John Magufuli, amabye nimgeni rasmi wa uzinduzi huo anawasili kwenye uzinduzi huo akipokelewa na waziri wa Nishati na Madini pamoja na maafisa wa Tanesco na wajumbe mbalimbali
Mradi huo unatumia gesi asilia kutoa Mtwara, unatarajiwa kuzalisha Megawatt 240 za umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya taifa yenye Megawatt 2200 na kupunguza upungufu wa umeme mikoa ya Kusini kama Mtwara na Lindi
Waziri wa Nishati na Madini anakaribishwa na Mkurugenzi wa Tanesco, ndugu Mwinuka kumpa maelezo ya kiufundi kuhusu mradi huo
Baada ya kumaliza kukagua mradi huo, Rais Magufuli ameuzindua rasmi mradi huo wa Megwatt 240
Baadae Rais anatarajiwa kuzungumza na wananchi waliohudhuria kushuhudia uzinduzi wa mradi huu
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda anatoa salamu na kuwatambulisha viongozi waliopo
Makonda anasema baada ya serikali kuhamia Dododma, jiji la Dar limekuwa jiji kubwa la kibiashara na linahitaji umeme wa uhakika
Makonda Jiji la Dar inahitaji Megawatt 548 na sasa wanapokea Megawatt 754 ila kuna changamoto ya kuwapelekea wananchi wautumia, eneo la Mbagala lilikuwa na tatizo la umeme lakini sasa hivi limetetuliwa kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya tano
Changamoto nyingine kwenye Wilaya za Kigamboni na Ubungo zinaendelea kutatuliwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Titus Mwinuka anatoa taarifa fupi ya mradi
Serikali inapanua miradi ya kinyerezi kinatumia teknolojia mpya inayoitwa Combine Cycle ambayo ina ufanisi mkubwa wa kuzalisha umeme kutoka kwenye gesi
Mradi huo ulianza kutekelezwa tarehe 1 Machi mwaka 2016 na unagharimu Shilingi bilioni 700 uliofadhiliwa kwa mkopo kutoka Japan kwa asilimi 85% na fedha kutoka serikalini kwa asilimia 15% serikali imeshalipa fedha yote iliyotakiwa kutoa
Mitambo yote ishaanza kuzalisha umeme na sasa inazalisha megawatt 160 kwenye gridi ya taifa
TANESCO wanaomba kuondolewa gharama za VAT na kodi za usafirishaji wa vifaa na utoaji vifaa bandarini ili kuwapunguzia gharama ambazo kwa sasa wamesema hawawezi kuzimudu
Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani anazungumza
Amemkaribisha mwenyekiti wa kamati ya bodi ya wakurugenzi TANESCO, Dk Kyaruzi ambaye anamshukuru Rais kwa kuliwezesha tanesco kuwa na vyanzo mbalimbali ya kuzalisha umeme ikiwemo Stieglers Gorge
Kalemani anasema kukamilika kwa mapema kwa mradi huo ni kutokana na utayari wa rais kutoa fedha fedha kwa wakati na kwa mkupuo
Pia Rais amewawezesha kutekeleza mradi wa kinyerezi namba moja mwaka juzi ambapo unapanuliwa iliuweze kuzalisha nyingine Megawatt 185 na unatarajiwa kuzinduliwa mwakani na utagharimu kiasi cha dola milioni 180, fedha za ndani
Pia kunja Kinyerezi namba 3 ambao utazalisha megawtt 600 utakaotekelezwa kwa awamu mbili na Kinyerezi namba nne uatakaozlisha megawatt 450
Pia kwa sasa kuna njia kuu ya kusafirisha umeme wa backbone unaosafirisha megwatt 600 ambao ndio utakuwa unatumika kwenye viwanda
Pia ndani ya miaka miwili wameweza kuwaunganisha wananchi umeme kutoka milioni 1,054,000 hadi 2,014,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 30
Rais John Magufuli anahutubia,
Anawasalimu wageni waliohudhuria uzinduzi huo
Rais anashukuru wananchi kuhudhuriakwa wingi licha ya mvua kunyesha, pia anawapongeza Tanesco kwa kufanya kazi nzuri na kusema yupo pamoja nao na hatawaangusha.
Rais anasema hakutegemea kuona mradi umekamilika kwa kiasi kikubwa kama ilivyo na kusema kaulimbiu ya hapa kazi tu inatekelezwa ipasavyo
Pia anashukuru kuwa kwenye wafanyakazi zaidi ya 2000 asilimia 95 ni Watanzania na hivyo fedha zilizogharamia mradi huo zitabaki Tanzania na kuishukuru serikali ya Japan.
Rais anasema matatizo ya umeme nchini sio mabaya sana lakini jitihada kubwa na za makusudi zinahitajika ili kukidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa
Bidii inatakiwa kuongezwa katika uzalishaji wa umeme katika nchi yetu
Rais anasema zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania hawajaunganishwa na umeme kutokana na gharama za uunganishaji kuwa mkubwa
Mikataba ya uzalishaji ni ya hovyo ndio inayosababisha kuzalisha umeme kwa gaharama kubwa
Bei ya umeme tunaozlisha ipo juu ukilinganishwa na nchi zilizoendela na kusababisha uwekezaji kutoka nje kuwa mgumu
Gharama za mradi huo ni dola za Kimarekani milioni 344, na Japan imetoa mkopo wa dola milioni 294.4 na zilizobaki kutolewa na serikali ya Tanzania
Mbalina mradi wa Kinyrezi 2 kunaupanuzi wa mradi wa Kinyerezi 1 kufikia megawatt 185 ambao utagharamiwa na serikali na utakamilika mwakani
Pia tupo kwenye utekelezaji wa mradi wa Stieglers Gorge utakaozalisha Megawatt 2100 na fedha za utekelezaji wa mradi huo zipo
Tanzania itakuwa na karibia jumla ya Megawatt 5000 kutoka Megawatt 1500 na sasa Wizara ya Nishati itabidi kushusha umeme bei
Sasa bei ya kujiunganishia umeme imeshushwa hadi shilingi 7000 tu na Rais ameiponheza nishati kwa hilo
Rais anasema ameigawa wizara ya Nishati kuwa wizara mbili ili kila waziri awajibike kivyake na asiwe na visingizio
Rais anahimiza Tanesco kuongeza kasi ya kuunganisha wananchi umeme na kusema wananchi wanalalamika kucheleweshewa na saa nyingine kuombwa ruswa
Pia amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujiunganishia umeme kwani serikali imeshusha bei yakuunganisha
Pia amaezitaka taasisi za serikali kushirikiana kwa karibu hasa katika kutekeleza miradi mikubwa ili isichelewe
Mfano kwenye uzinduzi wa magari ya bohari ya dawa bohari ya dawa ilillalamikia TFDA kutoshirikiana na bohari hiyo na kusababisha magari kukwama bandarini kwa sababu ya kodi
Anawataka watendaji wa serikali kuwasiliana ili kuepusha ucheleweshaji wa miradi na kusema mambo hayo yanamboa kweli kweli
Kama ni kifaa kinatakiwa kutolewa bandarini mara moja au kulipiwa fedha, kamishna wa TRA yupo na wizara ya fedha ipo, hivyo hakuna haja ya kuchelewesha
Rais anasema serikali inahamia dodoma lakini haina maana inaisahau Dar
Sasa Serikali inajenga barabara za juu Ubungo na Tazara ili kupunguza foleni, mradi wa mabasi ya mwendokasi kwenda tazara, ujenzi wa reli ya kisasa na upanuzi wa bandari ya Dar na mwelekeo wake ni mzuri
Pia serikali imepata mkopo wa bilioni 600 kutoa benki ya dunia ambayo itatumika kujenga barabara, masoko na madaraja katika jiji la Dar na inatarajia kukamili mwaka wa 2020
Amewataka wananchi kuendelea kuitunza amani na kushirikiana na serikali, wasiingizwe katika mambo ya udini,ukanda wala ukabila
Rais anasema aliapa kuilinda amani na atailinda amani kwa ajili ya wananchi
Pia amewaambia uongozi wa Tanesco kama kuna mabaki mabaki ya kuwaongeza wafanyakazi wao mshahara waongezewe