Rais Magufuli bila kuleta Mageuzi ya Uchumi wa watu, Nchi utaiacha ikiwo hoi sana kiuchumi

Rais Magufuli bila kuleta Mageuzi ya Uchumi wa watu, Nchi utaiacha ikiwo hoi sana kiuchumi

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,718
Reaction score
58,893
Wafanyakazi waongezwe mishahara ili kuongeza parchasing power, Wakulima wapewe ruzuku kwenye dhana za kilimo mbolea, matrekita, wajasiliamali wanahitaji sera bora za upatikanaji wa mitaji na bima za kiserikali za kulinda mitaji yao, Wafanyabiashara wanahitaji upatikanaji wa mitaji na sera bora kutoka TRA.

Tunahitaji uwekezaji kutoka nje kwenye Technology, Kilimo, Uvuvi ili kupanua upatikanaji wa ajira sector binafsi. Watanzania tunahitaji makampuni ya ndani ndio yajenge miundombinu yetu kama reli, barabara ili matrion yanayolipwa yabaki nyumbani kukuza uchumi wetu.

Rais wetu ashauriwe vizuri atoe ajira mpya kila mwaka hii ni moja ya njia ya kugundua kwamba uchumi unakua,

Taifa liwekeze kwenye mambo yanayoleta multiple impacts na social development.

Hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa walio wengi ni mbaya kuanzia ngazi ya chini mpaka wakubwa tunapopiga kelele sio kwamba hatuipendi Tanzania ila ukweli kama Rais Magufuli hatorudisha uchumi uwe wa watu ataacha nchi ikiwa na hali mbaya sana kiuchumi.

Ukiangalia Reli, Pesa yote 75% inaenda nje, Ukiangalia ndege tumetumia tr 2+ zote zimeenda canada na Marekani, Je kama trioni 2 tungeziwekeza kwenye kilimo kinachotoa ajira kwa 80% ya watanzania hali ingekuwaje kwenye uchumi wetu?
 
True hela mtaani haipo ndo hiyo anayopeleka nje kwann matajiri au makumpuni ya hapa ndani yasijenge miundombinu kwa mtindo huu Hali itakuwa ngumu kwa kuwa fedha nyingi inaondoka katika mzunguko
 
Economic growth ni lazima iwe translated kwenda kwenye economic development na hii lazima ionekane kwenye human development. Umenena vyema sana na kuna mahali treni imehama reli.
 
Watu dizaini yako ya kushinda mitandaoni badala ya kufanya kazi au unataka mheshimiwa rais akuwekee pesa mfukoni kwako?

Huu muda unaokaa kuandika back to back UZI utajutia siku labda upo kwenye payrolls ya dj zero
 
Mkuu

Naona mimi niko tofauti na wewe mahali fulani, samahani!

Rais Magufuli anafanya kazi kubwa sana kwa hilo mi namsifu. Sera yake ya Viwanda ameibeba vyema.

Tatizo langu liko sehemu moja, hivi viwanda vinavyofunguliwa Tanzania havina manpower ( Rasilimali watu) kitu kinachosabisha mwekezaji kuja na watu wake hapa.

Kitu gani kingefanyika ; Rais Magufuli angezitizama Technical schools, mfano, Ifunda Tech, Moshi Tech na n.k zifufuliwe na zichape kazi kuzalisha manpower kwa ajili ya Viwanda hivi.

Tizama sasa tuna changamoto ya kupata Vibali Vya wafanyakazi wa Wawekezaji kwenye viwanda hivyo ambao wengi wao wametoka Kenya na India, na kwingineko na elimu zao siyo kubwa kiasi hicho.

Changamoto nayoisemea hapa kwenye vibali, nchi hii mambo yanabadilika overnight, sasa hivi kupata working permit class C ni lazima mwombaji awasilishe nyaraka zake za vyeti kwenye taasisi za elimu kwa ajili ya kufanya utambuzi na ULINGANIFU.

Hizi taasisi bado hazijajipanga kwa zoezi hili, Nashawishika kusema hivyo kwa muktadha huu.

kwa mfano taasisi moja ambayo ningependa niigusie hapa ni Baraza la Mitihani la Taifa.

Baraza la mitihani la Taifa linahitaji kufanya utambuzi na ulinganifu wa vyeti kwa kuona cheti halisi( original copy) na siyo scanned copy ya cheti halisi,

Kwa mfano, Huyu mfanyakazi wa mwekezaji anaishi india, atume hard copy original ije iende baraza la mitihani.

Na siyo kwamba inaenda kwa mkono inatakiwa kutumwa kwa njia ya posta. Hii ni changamoto sana tena sana.

Kama tumeamua kuweka taratibu hizi ambazo ni ngumu kuzifwata katika mazingira haya ya kawaida, basi tuzalishe vijana wetu hapa wenye taaluma hizo ili hawa wawekezaji waache kuleta watu wao hapa nchini kwetu.

Shukrani!

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ukiangalia Reli, Pesa yote 75% inaenda nje, Ukiangalia ndege tumetumia tr 2+ zote zimeenda canada na Marekani, Je kama trioni 2 tungeziwekeza kwenye kilimo kinachotoa ajira kwa 80% ya watanzania hali ingekuwaje kwenye uchumi wetu?
Na Covid hii sijui kama itamwacha salama. Yetu macho tu.
 
Mkuu viwanda vya vyerehani vinne na kufunguo vilivyokwisha funguliwa?? Inaonekana huna taarifa sahihi
 
Sawa nimekusikia kijana "TEKENIKALI", ila mimi "SIPANGIWI", ndio maana hata maswala ya "KOLONA" mmepiga kelele weeeeh ila mmesahau "MIMI SIPANGIWI".
 
miaka mitano kwishney tunapigwa saundi tu. huko marekani trump harudi madarakani na huyu asirudi.
 
Magufuli angeanza na elimu kuifumua mengine yangefata automatikalee..mfano unvyosema makampuni ya ndani yangejenga reli zetu...wangapi ndani ya hayo makampuni ya ndani yana watu competent?..sio mjinga kuwapa watu wa nje tenda anajua kuna skills shortage..sasa badala ya ku address hili skilss shortage yeye anaendelea tu kupoteza hela kwenye makampuni ya kigeni....sijui kama nimekuelewa topic yako..LOL
 
Mkuu viwanda vya vyerehani vinne na kufunguo vilivyokwisha funguliwa?? Inaonekana huna taarifa sahihi

Mkuu salama

Viwanda vinafunguliwa niko kwenye hiyo barabara naona mishe zake.

Tuwe na imani na mzee wetu atatuacha mahala fulani.

Shukrani sana

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ukiangalia Reli, Pesa yote 75% inaenda nje, Ukiangalia ndege tumetumia tr 2+ zote zimeenda canada na Marekani, Je kama trioni 2 tungeziwekeza kwenye kilimo kinachotoa ajira kwa 80% ya watanzania hali ingekuwaje kwenye uchumi wetu?
Wakati ule hatuna ndege na reli hizo pesa zilikuwa zinaenda wapi mpaka Leo umpigie kelele magufuli?
 
Wakati ule hatuna ndege na reli hizo pesa zilikuwa zinaenda wapi mpaka Leo umpigie kelele magufuli?
Kosa moja halihalalishwi kwa kosa jingine, mwisho tutajikuta pale pale au labda tumerudi nyuma hatua kadhaa
 
Vipi ile bilioni 8 alizopiga dj isingeweza kujenga hata ofisi ya kata? CDM = Chama cha Dili ya Mbowe
 
Sijajua ni viwanda gani hivo vilivyofunguliwa ambavyo vinakosa wafanyakazi, swala la viwanda bado Sana ni sera ambayo ilo mdomoni kwene awamu hii lakini hakukuwa na maandalizi ya awali ya kufanya nchi iwe ya viwanda..bado sekta ya kilimo na nishati ipo chini Sana ambayo zina enhance ukuaji wa sekta ya viwanda....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia Reli, Pesa yote 75% inaenda nje, Ukiangalia ndege tumetumia tr 2+ zote zimeenda canada na Marekani, Je kama trioni 2 tungeziwekeza kwenye kilimo kinachotoa ajira kwa 80% ya watanzania hali ingekuwaje kwenye uchumi wetu?
Hizo ndege at long run zitaingiza zaidi ya tril 2+, sio kitu cha kufikiria kama hauoni mbali. Hiyo reli at long run itaingiza zaidi ya tril 6 na itasaidianusafiri na kupunguza gharama za maisha.
Na sio kweli kwamba pesa yote ya ujenzi wa Sgr inaenda nje. Maana cement,nondo na material mengi wananunua kwenye viwanda vya ndani hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom