Rais Magufuli: DC na DED wa Dodoma Muoe

Rais Magufuli: DC na DED wa Dodoma Muoe

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Dodoma ndio kila kitu, kwahiyo wewe Mkurugenzi (Kunambi), ni Mkurugenzi wa Jiji la Makao Makuu hata kama ni mdogo, ila utafute Mwanamke uoe, kwani hawapo Wanawake wanaotaka kuolewa na Mkugenzi jamani!?, nimekutangazia uanze kutafuta ndoa, DED unajipikia wakati Wagogo wapo wengi”-JPM

“Mkuu wa Wilaya Dodoma pia (Katambi) nae hajaoa kama DED (Kunambi), lazima tusemane hapahapa, na wewe uoe, huwezi kukaa na Viongozi wakubwa wa Makao Makuu hawana Wake, wakati Wasichana wapo wanapita hapa wengine wapo UDOM, CBE, Mipango wewe huoni tu!?”-JPM

“DC Dodoma na DED Dodoma mnataka muambiweje (ndio muoe), maana nyinyi sio Mapadri, sasa macho yenu hayaoni!?, wewe Nchimbi una Mke eeh? haya waambie hawa waoe..nilikuwa nachomekea tu kwamba tupo kwenye Makao Makuu ila tunaongozwa na Vijana ambao hawajaoa”-JPM
 
"Na wewe Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, ni mkubwa sasa, lakini uoe. Na Mkuu wa wilaya hujaoa, bado unajipikia. Huwezi kukaa na viongozi wakubwa hujaoa, wakati wasichana wapo, wengine UDOM na CBE."- Rais wa Tanzania, Dkt @MagufuliJP

Chanzo: swahilitimes
 
Huyu Katambi so ndo juzi alijidai kutaka kutoa orodha ya wabunge wanaochukua wanaochukua machangu kumbe hajaoa nae huwa anaenda kuchukua machangudoa mpaka anawajua wenzake wanaokutana kwa machangudoa.
Huenda akiwa nao ndio wanampa mastori.
 
Huyu Katambi so ndo juzi alijidai kutaka kutoa orodha ya wabunge wanaochukua wanaochukua machangu kumbe hajaoa nae huwa anaenda kuchukua machangudoa mpaka anawajua wenzake wanaokutana kwa machangudoa.

Ndo mchezo unavyokwenda mkuu
Naona ndo kiranja wa maeneo anaopoa vibinti na orodha ya wenzake
 
odoma ndio kila kitu, kwahiyo wewe Mkurugenzi (Kunambi), ni Mkurugenzi wa Jiji la Makao Makuu hata kama ni mdogo, ila utafute Mwanamke uoe, kwani hawapo Wanawake wanaotaka kuolewa na Mkugenzi jamani!?, nimekutangazia uanze kutafuta ndoa, DED unajipikia wakati Wagogo wapo wengi”-JPM
Hivi dogo Kunambi kumbe bado hujaoa ? Nilisahau kukwambia siku ile tunakunywa chai. Nonetheless, kamata mtoto mzuri hapo tuje kufanya harusi. Kaka zako tutakupa mafunzo ya kukaa na mke. Na nitaianza semina tukikutana tu kwenye kikao chetu kijacho
 
Huyu Katambi so ndo juzi alijidai kutaka kutoa orodha ya wabunge wanaochukua wanaochukua machangu kumbe hajaoa nae huwa anaenda kuchukua machangudoa mpaka anawajua wenzake wanaokutana kwa machangudoa.
Nani kakudanganya kuwa wasio oa ndio wateja wa machangu?

Hahahaaa tafuta uongo mpya mkuu [emoji16]
 
Back
Top Bottom