Rais Magufuli eleza sababu zako kwa nchi jirani sio kuwakwepa

Rais Magufuli eleza sababu zako kwa nchi jirani sio kuwakwepa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Kwenye suala la Corona hakuna aliyeleta huu ugojwa. Nashangaa Raisi wetu kuwakwepa marafiki zake kama Odinga na majirani zetu kama Kagame, Musevi , Kenyatta na hata raisi wa Zambia kiasi cha kuanza kufungiana mipaka.

Kwnye Corona hakuna jibu zuri lakini ni bora ueleze sababu zako ili kujadiliana tufanyaje kwa pamoja. Mfano kama kuna jirani kapata njia mpya huu ni wakati wa kusaidiana na kushauriana.

Vilevile ni muda wa kuanza kuwa na namba za maambukizi pamoja ili tujue sehemu gani za kuangalia kwa ukaribu.

Lakini vilevile uhaba wa vifaa majirani zetu je vipimo vyao vina matatizo au ni vyetu tu na tutasaidiana vipi?.

Huwezi kuwa Raisi ukaishia kususa badala ya kueleza sababu zako za msingi maana hakuna jibu kamili kwenye haya.

Vilevile hali inabadilika hivyo misimamo inaendana na hali ambayo ni ugojwa mpya na kila mmoja anajaribu kujifunza.

Lakini vilevile waziri wa mambo ya nje au mawaziri wa Afya wawasiliane na kutangaza kuwa wanawasiliana ili kusiwe na kutokufahamu kwingi.
 
Back
Top Bottom