Rais Magufuli hajawahi kuwa na Mpinzani

Rais Magufuli hajawahi kuwa na Mpinzani

Wana redbridgade
Wapinzani wana vyombo vya dola? Iweje ulinganishe mtu mwenye vyombo vya dola mahakama na mtu asiye na kitu na mmemfunga mikono nyuma plasta mdomoni, acha kuja na mifano yako ya kishamba toka kolomije
 
Taifa lina zaidi ya miaka 50 hakuna maendeleo na huto tuviendeleo kiduchu badala washirikiane na upinzani kuleta maendeleo kama kenya wamekalia kuwadhoofisha Chadema kwa gharama kubwa huku madalali wa siasa wakijinufaisha humo humo kwa njia haramu.
 
Ukweli usemwe tu. Kiutendaji, uwezo binafsi, ubunifu, uchapakazi, uzalendo ni vitu vinavyomuuza Rais Magufuli tokea awe mwanasiasa -- mbunge, waziri na sasa ni Rais

Rais Magufuli hajawai kuwa na mshindani katika kariba yake katika mambo hayo. Akiwa waziri katika wizara mbalimbali uwezo wake ulimuuza, hakuhitaji kuita vyombo vya habari na kusema yeye ni nani na anafanya nini, bali kazi zake na uwajibikaji vilimuuza.

Ni mtu asieyumbishwa, mwenye msimamo. Na huyu Watanzania walimuhitaji ndio maana wenye macho ya kizalendo, wanyonge wanaoipenda nchi yao wanatamani Rais Magufuli aongezewe muda sababu anajibu kero zao na kuzitatua kwa wakati.

Ukweli usemwe. Leo hata Watanzania tukiamua kujifanya hatuoni yakifayofanywa na Rais Magufuli ndani ya miaka miaka mitano, malaika watatujia ndotoni na kutuonesha yaliyofanywa na Rais Magufuli.

Tukijifanya hatuoni, tukipita katika flyover zitatukumbusha hii ni kazi ya Magufuli.

Tukijifanya hatusikii, zahanati, vituo vya afya kila kona, hospital za wilaya , hospital za kanda zitatuambia bila Magu, leo usingepata matibabu karibu na nyumbani kwako.

Tukijifanya hatusikii Watanzania wanyonge watamsemea na kutukumbusha Elimu bure imefanya watoto wengi wa masikini wawe shuleni.

Tukijifanya hatuoni ,wamachinga watatukumbusha Rais magufuli amerudisha thamani Yao na kuwafanya wafurahie nchi yao bila bugudha.

Rais Magufuli ni Baba lao

Kazi zilizofanywa na Rais Magufuli katika Taifa hili hazina mfano.

Tumpe MITANO TENA KWA KISHINDO.

WATANZANIA TUNAMPENDA Rais wetu ,Jembe letu ,anatupeleka katika Nchi ya Uchumi wa Kati , watanzania tuchape kazi

#Maliki,Malick
Basi magu kamzidi mungu no wonder maaskofu wanamnyeyekea maana hata mungu muda huu sasahivi kunawatu wanampinga
 
Watu, mnamjulia sana JPM! Ukitaka ulaji unaingia JF na verified user name, kujikita kumsifu JPM. Nayeye kwa misifa anaamua kutengua na kumteua Maliki Malick.
Huo unaitwa uteuzi wa kukurupuka na usishangae, baada ya muda mfupi, akianza kujiuliza kwa nini alikuteua na asipate jibu la maana. Ghafla bin vuu kama vile kazinduka huyoo, umetumbuliwa.
 
Sijawahi kuona bondia anapanda ulingoni, halafu mpinzani wake anafungiwa nje, halafu aliyepo ulingoni anajitapa hana mpinzani!!!!
 
Back
Top Bottom