Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

yeye ndiye ana wanausamama, hawa wa wizara wanatisha watu takwimu hazizi kuwa sahihi
Mkuu wanausalama wanachukua data hewani au hospital ? Na wanajuaje Kama huyu mgonjwa kapona au hajapona? Kama Ummy ana mdanganya anashindwaje kumtumbua? Mbona mama Malechela ilikuwa faster?
 
Marekani na Ulaya wanaonyesha idadi ya waliopimwa, Waliokutwa na maambukizi na Vifo.

Sijaelewa unaposema " Wasiopona" unamaanisha nini mkuu?
 
JokaKuu, Corona iipoingia kuna mahali nilieleza kuwa kuna umuhimu wa Timu ya Wataalam kuundwa na kuogoza mapambano.

Pascal Mayalla anajua fika nilitoa point 11 za nini kifanyike kama maoni likiwemo la wataalam.
Pasco anasema tusinyoosheane vidole wakati anaujua ukweli.

Haya ni mapambano ya kitaalamu na wataalam wa afya ndio wadau wakubwa. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni sehemu tu ya timu lakini si 'core team', ndivyo wanavyofanya kwingine duniani.

Uhai wa Raia sioni kama ni kipaumbele kabisa. Hivi kweli tunaweza kuwa na simple solution ya kujifukiza!

Joto la mwili ni 37c sasa unaingizaje mvuke wa 100c mapafu yakabaki salama?
Ombwe la kukosekana kwa watalaam lnaonekana wazi kama lile la RC kusema watu watoke kuchapa kazi

Hofu kubwa ya viongozi wetu ni uchumi,wanasahau kwamba afya za watu ni sehemu ya uchumi

Kenya, Uganda na Rwanda wapo serious sana, sisi ni wa mwisho kupata wagonjwa lakini sasa tuna idadi kubwa kuliko wenzetu. Kuna tatizo kubwa katika kushughulikia hili suala

Pascal Mayalla niweke rekodi sawa. Niliwahi kukueleza kuna uzembe na kwamba serikali imeshindwa.
Nikakueleza incubation period ikiisha mambukizi ya jamii yatajitokeza , hilo limetokea.

Tukasema mwezi May ndipo tutafikia peak na hapo hakuna kuchapa kazi ni kuhudhuria misiba.

Kwa hili la uchumi kuliko afya kuna mengi ya kujiuliza
 
Marekani na Ulaya wanaonyesha idadi ya waliopimwa, Waliokutwa na maambukizi na Vifo.

Sijaelewa unaposema " Wasiopona" unamaanisha nini mkuu?
Sijasema "wasiopona: nimesema "waliopona" kwa sababu siyo kila aliembukizwa lazima aumwe hivyo taarfa zinatolewa wangapi wamepimwa, wangapi wameambukizwa, wangapi wamelazwa, wangapi wamefariki. Hawasemi wangapi wamepona.
 
kavulata,
Eti cha ajabu watu mia3 ndo watufungishe ndani watu zaidi ya million 49. Huo ni uchizi
Namsapot mzee kwa kutotuweka lockdown.
 
Mtoa maada unaweza ukaniambia kwanini unalazimisha. tanzania iwemo? Kwanini si Burundi,Kenya na Uganda? By the way kwa East Africa ni nchi ngapi zimepata,na kama hazimo kwanini ulalamikie Tanzania ,Tanzania inauspecial gani hadi ipewe huo mkopo/ msamaha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viliachiliwa masika ili vitulize vizuri. Vingeachiliwa kiangazi nahisi visingetoboa kwa kiasi kikubwa hivi Africa. Nahisi kiangazi kikifika kasi ya maambukizi itapungua au kuisha kabisa sababu ya joto. Piga picha lile joto la Dar, hatutahitaji kujifukiza, hilohilo ndo litaua virusi
 
Watanzania wenzangu nawasalimu katika jina la bwana.
Tumshukuru mungu kwa kutuamsha salama sisi tuliobahatika kuiona siku ya leo.

Tunakumbuka kuwa mh Rais alitukaka tufunge na kuomba kwa siku tatu juu ya gonjwa hatari la corona linalo sumbua dunia kwa sasa.
Baadhi ya watu tulibeza na kupuuza bila kujua Mungu anaweza kila kitu na humpa kila mtu anacho omba.Sisi watanzania tulimwomba Mungu atuondoshee janga hili la corona na hakika amejibu maombi yetu,je unajua amejibu nini.?

Ni hivi sababu za Rais wetu mpendwa kuomba tufanye maombi na tumkabidhi Mungu janga hili la corona zipo wazi kabisa na kila mtu anajua vizuri sana.sisi kama nchi ya Tanzania vituo vyetu vya afya vipo hoi taabani.

Havipo vifaa vya kutosha vinavyo hitajika Kama vile mashine za oxygen,madaktari,na manurse na vifaa vya kujikingia,ukweli upo wazi ndio maana wagonjwa waliopo Amana kwa clip inayozunguka mitandaoni na nasikia mkuu wa wilaya ya Ilala akilalamika kuwa wagonjwa wametoroka hospital.huu ugonjwa ni hatari hauchagui hayupo muuguzi aliye tayari kufaa ikiwa hata hawajatangaziwa promotion yeyote kama ilivyo fanyika huko Kenya na Ghana n.k nasikia wahudumu wetu hawasogelei wagonjwa wanaogopa.

Kwa kuwa mazingira na kipato chetu ni tofauti na nchi nyingine njia pekee ya kutuondoshea janga hili ni kwa kujikabidhi kwa Mungu,tusingeweza kutumia njia Kama ya China ya kutengeneza hospital mbili kubwa za kubeba maelfu ya wagonjwa kwa siku sita, hospital inakamilika ikiwa na vifaa vyote,njia hiyo sisi hatuiwezi hilo lipo wazi ndio maana hadi leo hii bado tuna maabara moja tu nchi nzima ya kupima huu ugonjwa.Pia hatuwezi fanana na England ambao wanakaribia kupata chanjo kupita vyuo vyao vikuu vya Oxford na imperial college of Landon,

Njia yetu ilikuwa ni moja tu kuomba, kufunga na kumtegemea Mungu basi,ndivyo kwa sababu hatuwezi chochote na ukisemwa tufanye lockdown ndio unatumaliza,ilikuwa tukae tujikunyate tusubirie kufa na kuzikwa na magrader Kama tunavyo ona huko ugaibuni,Hilo kwetu halitokei mungu amejibu maombi yetu.

Unajua amejibu nini?unatamani kujua?
Kwa wakristu wanajua mateso aliyo yapata Musa akiwa jangwani kwanye safari ya canani,Wana wa Israeli wakiwa jangwani waligongwa na nyoka,wengi wao walikufa Musa hakuwa na Cha kufanya na hapakwepo na dawa, Musa alimlilia Mungu awaokoe Wana wa israeli.Mungu alijibu maombi ya Musa.unajua alijibuje?

Watu hawajui Kama maombi yetu ya siku tatu yamesha jibiwa wanafikiri labda maombi yetu yatajibiwa kwa njia ya muuigiza ila wanayofanya manabii wa uongo mara papuu ugonjwa umetoweka.

Mungu alimjibu Musa tengeneza nyoka wa shaba utundike kwenye mti,kila atakaye gongwa na nyoka na kutazama atapona.Mungu alikuwa na uwezo wa kuua nyoka wote ila hakutumia njia hiyo. Na kwa wote walio jifanya wajuaji kwa kuwa kisayansi hilo haliwezekani kwa kuangalia tu nyoka upone walikufa.

Ndivyo hivyo tumejibiwa aliye tuomba tuombe ambaye ndiye rais wetu,ametuletea majibu kwa kujua au kwa kuto kujua,inawezeka alijikuta anasema tu hajui hata alisemaje,ni maneno yalimtoka na huo ndio ukuu wa Mungu.

Umesha ambiwa dawa ya corona ni kujifukizia,chukua majani ya mipera,mapapai,majani ya sungura,miarobaini,milonge,michaichai,n.k chemsha mpaka yatokote,epua sufuria chukua shuka jifunike,pia unatakiwa uwe na mti au mwiko,ukisha jifunika koroga hayo majani mvuke utatoka,fanya zoezi hilo kwa muda,ukiona mvuke hautoki na hujaridhika rudisha sufuria jikoni then rudia tena,baada ya hapo chukua hayo maji yapooze nenda ukayaonge,hili zoezi fanya Mara mbili kwa siku mpaka upono.
Hakuna garama yeyote utakayo tumia ni imani yako na kutafuta hayo majani.ni njia ambayo kila mtu anaimudu,huo ndio ukuu wa Mungu tumpe sifa na utukufu.

Utakaye ona njia hiyo siyo tumia ya kwako unayoijua,na hakika utakufa Kama hao wana wa Israeli,njia rahisi ni hiyo kumbuka hatuna oxygen machine za kutosha ugonjwa unashambulia mapafu,kwa hiyo wakati unafanya utaratibu mwingine wa matibabu endelea kujifukiza.

Mungu ni mwema tumshukuru kwa kutupatia dawa.
 
Umesha ambiwa dawa ya corona ni kujifukizia,chukua majani ya mipera,mapapai,majani ya sungura,miarobaini,milonge,michaichai,n.k chemsha mpaka yatokote,epua sufuria chukua shuka jifunike,

Mungu ni mwema tumshukuru kwa kutupatia dawa.[/QUOTE]

Kwa hiyo dawa ya huyo msukuma unawezea kujikuta umetengeneza bomu la nyuklia likakuua wewe na familia yako badala ya kuua korona



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesha ambiwa dawa ya corona ni kujifukizia,chukua majani ya mipera,mapapai,majani ya sungura,miarobaini,milonge,michaichai,n.k chemsha mpaka yatokote,epua sufuria chukua shuka jifunike,

Mungu ni mwema tumshukuru kwa kutupatia dawa.

Kwa hiyo dawa ya huyo msukuma unawezea kujikuta umetengeneza bomu la nyuklia likakuua wewe na familia yako badala ya kuua korona



Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]Sijui ni trolling au ni serious. But for serious kase. Hakuna ushahid wa kitabibu kuwa hiyo kitu inafanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…