Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Hakuna aliyesema hawaweki takwimu. Kuna tofauti ya kuweka takwimu na kutangaza takwimu. Mbona unataka takwimu za corona tu, je za kifua kikuu unazijua? za ukimwi unazijua? nk! Hata leo ametoa takwimu maana yake zipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Visa vinazidi kuongezeka Morogoro ,Arusha na DAR ni hatari........Hawa wapiga zumari wa meko tusiwasikilize wanatetea ugali wao.
eti wanasema ..kama ipo mbona watu hawakufi...mbona hatujasikia misiba kwa amajirani...etiiii......corona ni propaganda za mabeberu lakini siyo yambuzi ni yale ya kutoka ulaya na amerika
 
Takwimu za TB,HIV za nini wakati hayo magonjwa yashathibitiwa? Tunataka kujua issue za korona mkuu kwasasa tuna wagonjwa wangapi tuweke wazi kama USA!! mambo ya kusema mloganzira sijui kuna wagonjwa 6 wengine wamepona ni kutuchukulia poa waTZ na kutuona "MAZWAZWA".
 
[emoji205][emoji205][emoji205][emoji23][emoji23][emoji23]
Misiba kila leo si ajabu! Hata kabla ya corona misiba ilikuwa kila leo!! Hivi kwa akili yako unafikiri misiba imeletwa na corona tu?? Je hii misiba kila leo IPO Tanzania tu? Huko mnakowasifia kwa lockdown kila leo wanakufa kwa maelfu na mamia! Ingia worldometer uone!! Unatutisha na misiba? Kuna ambaye hajawahi kufiwa humu ndani??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
eti wanasema ..kama ipo mbona watu hawakufi...mbona hatujasikia misiba kwa amajirani...etiiii......corona ni propaganda za mabeberu lakini siyo yambuzi ni yale ya kutoka ulaya na amerika
Wapuuuzi watu wanakufa wanaenda kuzika kimya kimya na wanawapiga biti wafiwa wasitangaze chochote wakae kimya,makaburi wanayozikia wagonjwa wa korona yanalindwa na JKT halafu wanatuletea ngonjera kwamba ushaona msiba wa jirani kafa kwa korona,yule jamaa wa aljazira alisema jina la ndugu yake ni la 256 wakati wizara ya afya bado ipo kwenye 11.
 
Tutakesha hapa.Mada iloyopo mezani ni COVID.

Tunazungumzia Covid unaleta mambo ya kifua kikuu na Tauni.

Talwimu zinasaidia ni

1.Vipimo vingapi vimefanyika?
2.Wangapi wamekutwa na maambukizi?
3.Wangapi wamefariki?
4.Wangapi wamepona?

Ukipata takwimi hizo unaweza kufanya tathmini ya mkakati wako wa udhibiti.

Takwiimu ya wangapi wameeruhusiwa haina tija kwa maana 80% ya wagonjwa hupona bila ya tiba yoyote.

Kutotoa takwimu au kutoa takwimu batili kunafanya watu wapuuzie kuchukua tahadhari.

Ugonjwa ukiendelea kusambaa watakaoumia ni wazee wetu na wagonjwa wetu wa magonjwa sugu.
 
HAPA MH RAIS UMEIBUKA MSHINDI,KAMA NI UWANJANI BASI UBAO UNASOMA TATU BILA NA NI DAKIKA YA 90
-Jiulize tu,ulaya na marekani wanajitahid tuchukua tahadhari nzito kuliko sisi lakin rate ya death na live cases bado ipo juu
-bongo maisha yanasonga ,tuko less strict kuliko wao,tuna less facilities kuliko wao lakin death rate ipo chini ,
-tuliamua kutokufanya lockdown mwisho wa siku dunia nzima imeungana nasi
-mkuu yupo very right kusisitiza watu wasitishane kuliko uhalisia,corona ipo lakin haina case fatality rate ya kwetu si sawa na ulaya na marekani hii inatoa chachu kwa tafiti zifanyike kujua why.....
-
 
Acha uzwazwa watu wanaenda kwa takwimu mkuu ndio maana tunaweza kuproject 20250 TZ kutakuwa na watu wangapi kwa kufata mahesabu ya takwimu na kucheza na rate.

Linganisha mwaka jana kuanzia January mpaka may walikufa watu wangapi na kisha linganisha mwaka huu jan-may 2020 wamekufa wangapi kisha njoo na tantalila zako.

Ndani ya mwezi mmoja wamekatika mawakili/wanasheria kama 15 hivi halafu unasema ni kawaida,je mwaka jana wanasheria wangapi walifariki? Leta takwimu za mwaka jana mie najua za mwaka huu wanasheria/mawakili 15 wamekatika.
 
Leo nimefahamu bila shaka prof Jalala kwanini alipanda ndege kufuata ile juice ya Madagascar ili nani apewe...

Wanasiasa siyo wa kuwaamini! NEEEVEEEERRRR

Everyday is Saturday....................... 😎
 
Kawapongeza na kuwashangilia waumini ambao hawajavaa barakoa leo
Kawapongeza kwa kuwa wanajua matumizi sahihi ya Barakoa! Angeshangaa kama wangevaa barakoa katika mazingira ya kukaa zaidi ya Mita moja kati ya mtu na mtu!
Wote tumemsikia akisema tuchape kazi HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI. Na wote tunafahamu kuvaa Barakoa ni sehemu ya tahadhari kwenye maeneo ambayo haiwezekani kukaa mbalimbali.
Sitafsiri kipengele kimoja nje ya muktadha (out of context). Ukifanya hivyo utapotosha ukweli wote. Inavyoonyesha watu wameshikilia sentensi moja tu as if hiyo ndiyo hotuba yake.
Hivi nikikutaka utupe kichwa (heading) ya hotuba yake si ajabu ukasema: "Rais apinga uvaaji wa Barakoa". Kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo aseme hauna dawa sio kutudanganya kua ukijifukiza unapona. Hehe mna matatizo kichwani?
Ukiona hivyo wengine wanapona kuna habari zimetapakaaa katika mitandao kuwa mgonjwa wa corona anapotumia azithromycin plus ascorbic acid na zinc tab anapona je hili hujawahi kulisikia?
 
Tunataka
Kwa nini mnalilia data za corona? Mna ajenda gani na data hizo? Mbona siwasikii mkitaka data za magonjwa mengine kama TB, ukimwi, cancer nk??

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunataka data kwa sababu ndio kitu pekee tunachoweza kuamini
Just in
Saivi saa kumi jioni naona breaking news hapa citizen TV kwamba kuna cases mpya za 12 Truck drives from TZ Sasa jiulize hawa huo ugonjwa wameupatia wapi kama sio huku TZ
That's why tunataka takwimu we can't rely on what a politician says
 
Hawa waliokuwa wanalazwa ni kwa siku au jumla?


Anasema jali ikiwa nzuri atafungua, kwani hali ilikuwa mbaya wakati yy mwenyewe alisema hali ni nzuri!

Kumbe hali ilikuwa mbaya hadi mtoto wa mkulu aliugua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…