Rais Magufuli hakuvunja Katiba kuwateua Prof. Kabudi na Mpango kuwa Mawaziri kabla ya kumuapisha Waziri Mkuu. Zitto ndiye alifaulu kupotosha umma

mambo yanayoleta faida kwako utayapata kwa kuacha uvivu wa kusoma.

Kama hukuwa umezaliwa wakati yanatokea unayouliza, soma uelewe.

Kwa faida yangu na jukwaa, tuambie nini kilitokea mpaka Mh Waziri Mkuu Edward Lowasa kujiuzulu.
 
mambo yanayoleta faida kwako utayapata kwa kuacha uvivu wa kusoma.

Kama hukuwa umezaliwa wakati yanatokea unayouliza, soma uelewe.
Aisee we kilaza kweli, usiwe unaanzisha mada ambazo huwezi kutetea!.
 
Mimi nadhani matakwa ya kikatiba yangefuatwa kwanza kwa Rais kumuapisha Waziri mkuu halafu baada ya kiapo akiamua kushauriana naye ama la hilo litakuwa halituhusu maana katiba imemtaja Waziri mkuu akiwa na mamlaka kamili.

Maadamu katiba imesema Rais atashauriana na Waziri Mkuu basi sharti katiba ifuatwe halafu kipengele cha aidha Rais aufuate ushauri aliopewa ama asiufuate hilo ni juu yake.
 
Hauna summary yake mkuu?
 
Hapa ndio penye tatizo kwa wasomi wetu, yaani vifungu vya katiba viko wazi lakini msomi anatoa uchambuzi mrefu wa kimazoea ya mabeberu, badala yakuchambua vifungu vya katiba ya nchi vinasemaje.
 
Kwenye Banana republic nyingi watawala wanakuwa na washauri wengi,lakini badala yakupokea kuutathimi na kuufanyia kazi ushauri wanaopewa,watawala ndio wanageuka kuwa washauri wa washauri wao.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Hahaha nchi zetu hizi ukishauriwa unaonekana mjinga, sasa ndio maana huwa unaona kwenye press za ikulu yeye ndiye anaongea, na kuwatukana humohumo ili ionekane yeye ndiye mwenye madaraka na mamlaka, na hao wengine ni wajinga tu.

Utaona akiisha waapisha anawaambia na nini cha kufanya.

Utasikia " nimekuapisha kazi ya kwanza kamsimamishe kazi yule mkurugenzi aliye nunua gari la kifahari na utume watu wakachunguze haraka" .

Hii ni kutuonyesha sisi kwamba hiyo mijinga anaipa kazi lakini kila kitu yafanyacho ni mawazo yake.
 
Sasa mbona umetuma tu historia. Hizo systems unazozisemea mwisho wake zinatafsiriwa na nchi husika ama kupitia katiba au kupitia sheria nyingine inayotokana na katiba.

Watu tufuate katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Imetoa masharti na namna ya kutekeleza majukumu ya kitaifa. Hayo mambo ya Westminster na Presidential ni Frameworks tu wewe mbulula.

Katiba inasemaje kuhusu jambo hilo??
 
Kwa sababu anayeambiwa naa kujibiwa ni Zitto, nasubiri maana kwa nondo hizi natumai bado naye anachimbua atoke na jibu sahihi.
 
Zitto anajua kila kitu, alipotosha kisiasa. Hivyo hatajibu chochote kuhusu uzi huu.

Kwa sababu anayeambiwa naa kujibiwa ni Zitto, nasubiri maana kwa nondo hizi natumai bado naye anachimbua atoke na jibu sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…