Rais Magufuli hali ya maisha ni ngumu sana, tuonee huruma

Mkuu we pambana kivyako, mtegemee Mungu afungue milango, kamwe usitegemee kuwa Magu ataleta unafuu wa kiuchumi/maisha hii ni kwa sababu falsafa yake ni uchumi wa vitu na sio watu, then kingine serikali yake ipo hoi kwenye makusanyo ya kodi so ataendelea kukopa ili atekeleze miradi yake ya vitu, halafu hawezi jali uchumi wa watu maana miaka yake 5 ijayo ikiisha system na hata ccm hawatamkubalia aongeze muda so atambana miaka 5 ijayo aache vitu kadhaa kwa hiyo tegemea midege, vivuko, meli, kununuliwa kwa wingi, miaka yake ikiisha atawaonyesha mafanikio ya vitu, maana anajua kauli yake ya tz ya viwanda ilikufa kabla hata hajawa Rais!!
 
Tunalipa kodi na hizi kodi lazima zitusaidie kiuchumi na kimaendeleo. Ndio maana ya kuchagua serikali. Kwa hiyo serikali lazima isaidie wananchi.
 
Kwa hiyo hao mama ntilie wanaofeli hawajui masoko? Maana market ni demand. Na pale mzunguko wa pesa ukiwa mkubwa demand inakuwa kubwa.
 
Hao wazawa wanao uwezo wa kufanya mradi kama wa daraja la Busisi kwenda Kigongo. Mbona wakati wa Mkapa kulikuwa na miradi mingi na ilijengwa na wageni na mzunguko wa pesa ulikuwepo? Yeye aangalie Fiscal policies nzuri ili pesa ziwafikie wananchi.
Kwa hiyo huna imani na wataalamu wazawa kwanini basi una imani na serikali za watawala weusi?
 
Kwa hiyo mnamaanisha aruhusu ufisadi kwenye pesa za umma sio?
Maana hizo ndo zilikuwa zinazunguka kwa haraka
 
Tunalipa kodi na hizi kodi lazima zitusaidie kiuchumi na kimaendeleo. Ndio maana ya kuchagua serikali. Kwa hiyo serikali lazima isaidie wananchi.
hivyo unavyowaza wewe Magu hawazi hivyo! kwan we si unaona hata kupambana na corona ana mbinu zake anazotaka zitumike kwa kifupi Magu kwa akili zake anaamini anajua kila kitu!
 


Wakati mnaifilisi NSSF mbona ulikuwa kimya?
 
Wakati mnaifilisi NSSF mbona ulikuwa kimya?

Habari kumbukizi mwaka 2017, mradi wa Dege Beach Eco Village wapigwa mnada

Yono Auction Mart madalali maarufu Tanzania watangaza mnada wa mradi mkubwa baada ya NSSF kuishiwa fedha na hivyo mradi kukwama kuendelea.

Dhima ya mnada huo ni kupata mwekezaji awe wa ndani au nje ya nchi ili kuwezesha mradi huo uweze kukamilika.

Mradi huo una thamani wa USD 350 milioni hivyo anatafutwa mwekezaji kutia kiasi hicho cha fedha ili ukamilishwe kupitia mnada huo.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni kutasaidia pia uchochezi wa kiuchumi ktk mradi huo na maeneo ya Kigamboni, Dar-es-Salaam.
 
Kwa hiyo huna imani na wataalamu wazawa kwanini basi una imani na serikali za watawala weusi?
Tumia akili kujibu hoja. Tofautisha watalaamu na wakandarasi wazawa.
 
Kwa hiyo mnamaanisha aruhusu ufisadi kwenye pesa za umma sio?
Maana hizo ndo zilikuwa zinazunguka kwa haraka
Kwa hiyo unadhani ili mzunguko wa pesa uwepo lazima kuwe na ufisadi? Zipo njia za kiuchumi kusaidia wananchi
 

Ningesikiliza hizo porojo kama NSSF ingeweza kuwalipa waliowekeza bila kuwadhulumu, lakini matokeo yake ni wachache tu ndio waliokuwa wanafaidi matunda ya wale waliovuja damu.
 

Lockdown ya aina hiyo uliyoielezea hapa ni imagination yenu ya mtaa wa lumumba. Haijawahi kuelezewa au kufanywa na nchi yeyote duniani.
 
Unafungua biashara gani.watu tunafanya biashara zinaenda.change mind set yako kwanza.
 
Unafungua biashara gani.watu tunafanya biashara zinaenda.change mind set yako kwanza.
Hongera kwa biashara yako kufanikiwa. Mimi nazungumzia hali ya watanzania kwa ujumla. Sio mtu mmoja kama wewe. Majority sasa hivi hali ni mbaya sana.
 
Nyie endeleeni kulialia tu, mimi ya kwangu ni hii miradi mikubwa nliiyoanzisha! Kwani kwenye kampeni niliwaahidi kuwajaza pesa kwenye mifuko yenu? Ukiona unapata taabu sana kuishi Tanzania hama nchi! Na mkinichagua hii 2020 msahau maisha bora, mimi siyo Kikwete aliyewaahidi maisha bora!
 
Viwanda vipya 8,500 uchumi utapaa tu kuwa na subiria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…