Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Zito na January wote hao walishatuhumiwa humu Jf kuhusu NSSF. Ningeshangaa eti zito awe chanya kwa JPM.
 
Hapa Zitto anasaidia kuonesha Makamba amekuwa akiwasimulia issue ya kutafutwa . Badala ya kumtetea mnazidi kufanya iaminike Makamba alikuwa anatoa siri kwenu kuhusu mwenendo wake na serikali. Mnakurupuka sana na kuzidi kuharibiana tu.
 
Nimeona madini, nikajiuliza nani huyu kashakua mjeolojia ??? Big up Zitto Zuberi
 
Katika hili Raisi hakuna mtu mwenye akili timamu atakuelewa, wizara hii ilikuwa kama haipo. Ni huyo mbunifu January ameiinua. Kijana ni mchapa kazi anaeleweka nchi nzima. Visingizio ulivyovitaja havina mashiko. Haya bwana kisasi ulicholipiza kwa makamba. Mazingira oyee. Namshauri kijana akomae ndani ya chama 2020 wapambane tupate mgombea mzalendo, mkweli asiye mnafiki,msanii na mbaguzi
 

Environmental Impact Assessment ni zoezi la kitaalam ambalo hufanywa kabla ya mradi kuanza kubaini vihatarishi vya ki-mazingira na kijamii vinavyoweza kujitokeza kama mradi fulani utatekekelezwa. Zoezi hili hutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo " Environmental Management Plan" ndani ya muda fulani. Mradi hupatiwa cheti kinachofahamika kama Environmental Impact Assessment Certificate. Kwa miradi ile ambayo ilianza kabla ya sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 hii hufanyiwa ukaguzi wa mazingira " environmental audit" na zoezi huangalia athari za kimazingira na kijamii ambazo mradi umesababisha na mwishowe hotoa mapendekezo ya kukabilina na athari hizo ndani ya muda fulani " Environmental Audit Certificate" Kwa pendekezo la leo la mheshimiwa Raisi wetu la kutoa vyeti kabla ya miradi kuanza inabidi Nemc watafute aina nyingine ya cheti ili kuendana na kasi ya Mheshimiwa Rais, kwa mfano wanaweza wakatoa kitu kinachoitwa " An interim Environmental Impact Assessment Certificate" ili kuendana na speed ya Rais na pia tuweze kutoharibu maana ya ya vyeti hivi viwili i.e EIA na EA
 
Nimekuja kugundua wapinzani nao ni mafan WaCCM,usikute hapo wamekaa standby ili mmoja akichomoka CCM wampe nafasi ya ugombeaji kiti cha urais kana 2015.

Ila kaeni mkijua CCM ni watoto wa baba mmoja na siku zote ugomvi wa ndugu hauingiliwi,we waache ,waswahili wana msemo wao "ndugu wakigombana chukua jembe ukalime,wakipatana chukua kapu ukavune".Wao upinzani wanatakiwa wa assume hawajui kinachoendelea.
 
Mwigulu naye alipotumbuliwa tulielezwa sababu ingawa watu waliamini sababu kubwa zaidi hazikusemwa!
 
bila kusahau viroba maana bodaboda asubuhi tu walikuwa wamelanduka lakini baada ya kupigwa marufuku na miajali ikapungua
 
Hivi kwa akili zako mwenyekiti, sababu uliyoitaja yaweza kuwa sababu ya kumfukuzia Makamba jr uwaziri?
Mbona mdomo wake uliomponza haujauweka tukaisikia clip?
Hata ungelikuwa wewe kwenye Act yako, waweza kufanyakazi na 'joka', mtu ambaye hamuendi pamoja kiuelekeo huku akijifanya muadilifu sana kwako wakati kiuhalisia anakuchoma?
Waraka mreefu! Wewe waambie wote hao wahamie kwenye chama chako ndiyo mtaendana.
Haya maelezo uliyotoa hayawezi kumvutia mTz yeyote mwenye akili timamu, akayasadiki na kuyaamini.
 
Jiwe mpuuzi sana!
 

'Bwana Rais'.... mara tatu umeandika hayo maneno Zitto! Bwana Rais!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…