Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Kweli ukisikia wadanganyika ujue wapo wengi. Mifuko ya plastic ni mkakati wa Makamba? Hujui amedakia juu kwa juu tena baada ya kuchelewa sana? Na hata kama angekuwa ni yeye, muda wote aliokaa serikalini wewe unaona hilo jambo dogo kabisa linahalalisha kumpa sifa? Wengine naona mlikuwa mahawara ndiyo maana mnajitoa ufahamu.
 
Nyumbu toa maelezo kidogo. Hebu tueleze ushupavu wa huyu mtu wako.
 
Dah aisee sishangai haya maana sio mara ya kwanza Magufuli kusema uongo ....Alishasema alikuta sukari kilo ni 5000 wakati yeye ndiye aliyesababisha sukari kupanda bei.
Hivi ile salary slip yake ya mil9 alishaitoa???
 
Kazito kanafki sana kwakweli, mama samiha anatikisa kichwa kukubali kuwa la mifuko ya plastiki lilicheleweshwa kenyewe kanapinga utadhani ndiye makamu wa raisi. Siasa za unafiki zitatuumiza!! Rais akifukuza shida enzi hawafukuzi wanafosi maumbea ili afukuze what a shame. Mlifosi lowassa akafukuzwa kisa mjisifu mmejenga hoja sana leo imedhihirika alionewa...akiwa mwenyekiti PAC mashirika ya umma yalikuwa corrupt balaa kakashindwa kubadili huku kakijidai kako makini kumbe kanavutiwa mapepa kanatulia. Kwendraaaaa mwanasiasa feki na baradhuli.
 
Tafadhali sana ndugu zito,
Usije ukamshauri bwana January kujiunga na upinzani.

Tunataka abakie huko huko ccm.

Januari usije ukaenda chama chochote ch upinzani.

Usije ukathubutu.

Baki hapo hapo.
Chezeni karata zenu vizuri.

Ndiko anakoelekea huko...
 
Kavutabangi toka ACT kalipokosa ulaji kupitia zitto kanaingia CCM na kutamka wakongwe waondoke...
Sikuhizi kila MTU ni msemaji na mchambuzi wa siasa. Member hajafanya lolote bays na anahaki ya kuamini yeye ni bora,anapoona chama kinavurugika anahaki ya kuongea faragha na mwenzake juu ya anachokiona. Tuache unafiki
 
Kama mh rais haikumpendeza kutoa sababu za kumfukuza haikuwa na haja kutoa sababu zisizo. lazima zitajadiliwa
 
Makamba aliyemponza ni baba yake, zile audio na mipango yake dhidi ya mwenyekiti wake ni ushahidi tosha wa kufutwa uwaziri
 
Makamba aliyemponza ni baba yake, zile audio na mipango yake dhidi ya mwenyekiti wake ni ushahidi tosha wa kufutwa uwaziri
J makamba alikuwa anafanya wajibu na kazi aliyoagizwa nana baba yake...!! Asingeweza kupinga wala kukataa maana lile jambo halikuwa na ubaya wowote... Maana musiba ni kweli anawatukana na kuwadhalilisha wastaafu so ingekuwa haina maana wazidi kukaa kimya
 
Mimi nimeamua kuwa mtazamaji na msikilizaji mzuri tuu katika siasa za sasa za hii nchi.
 
Ningeamini anastahili sifa unazompa JM kama angekuwa na msimamo imara kuhusu:
1. Steiglers Gorge hydro electric power project.
2. Uranium mining Bahi na huko Selous National Park
3. Asbestos removal from Dampo Ilala and else where
Lead contamination in building materials.
3. Mercury poison in gold mining areas.
4. PCB ground water pollution from industrial and automotive waste.
5. Annual flooding of the Msimbazi creek and it's impact on housing and infrastructure at Jangwani, Vingunguti and other areas.
6. Strict implementation of project environmental impact assessments in compliance with the existing laws.
7. Comprehensive public participation in the environmental assessments process.
Maana ya hayo mambo yote juu ni kuipa meno NEMC. Kitu ambacho JM, kama watangulizi wake, hakufanikiwa.
 
Kwa level ya wazaziri kupanga mambo kama yale ni utoto, na hao wote wanafutwa uanachama wa ccm, mda utakapo fika

Sasa unatumwaje na mzee wako ufanye mambo kama yale? kwann yeye asifanye na wazee wenzake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…