Kila nikikumbuka slogan hii huwa nawatathimini watanzania nashindwa kuwaelewa kabisa, je tumerogwa?
Mbona hatuhoji kama Tanzania hii ndiyo ya Viwanda tuliyoahidiwa au tungoje nyingine.
Najua waliodanganywa 2015 ni wale wale wanaodanganywa leo 2020 kuwa anakwenda kuifanya Tanzania iwe kama Ulaya na watu wanashangilia pasipo kuhoji utekelezaji wa Tanzania ya Viwanda.
CCM na Magufuli walivyo wajanja hata kugusia Tanzania ya Viwanda hawataki tena, wanajua wakiwaamusha waliolala watalala wao.
Tuendelee kusifu na kushangilia, tunywe mtori labda nyama tutazikuta kwa chini.