1. Serikali ilisema inataka kuhakikisha makinikia yote yanasafishwa nchini ili tusiibiwe, jiulize Leo baada ya makubaliano haya, imekuwaje makinikia sasa ni ruhusa kwenda nje ya nchi Kama ilivyokuwa mwanzoni. Inamaanisha nn hii kwako wewe Mtanzania? Kama huna akili nzuri hata utaendelea kuona hakuna haja ya kusafishia ndani ya nchi, vinginevyo utaona kuna aina fulani ya pesa zitakazonufaisha watu wachache na sio watanzania...
2. Kama unakumbuka vzur,baada ya kukamata makinikia,serikali ilisema na kupitisha sheria tatu bungeni (maboresho ya mining act) kuwa mikataba yote ya madini yajadiliwe na kupitishwa na bunge,hii ilitufanya tujue kweli mikataba itakuwa ya uwazi,ila unajua kilichotokea juzi? Mkataba huu wa madini umepitishwa wapi? Kwa hakika sio bungeni.. Hapa ndio tujiulize tunakumbuka yale tuliyokubaliana au sie tuna fuata upepo tu..
Kulikuwa na fine ya bilioni za kimarekani 190 ($190bn) ambazo sawa na pesa za kitanzania (190 bn ziwe Mara 2307) yaani bilioni 190 ya kwanza mpk zifike 2307(elfu mbili mia tatu na saba),hapo utajua ni kiasi gani hiko,Sasa tujiulize baada ya kampuni ambayo tunaidai kufa na kuzaliwa ingine,hizi pesa tunazodai tutalipwa na Nan? Hapo hapo ujue kampuni iliyozaliwa ni yetu pia hata km ni kwa asilimia ndogo,nan atakae dai pesa kutoka mfukoni mwake ili aweke mfuko mwingine?
Je pesa hizi zilipaswa kulipwa kabla ya makubaliano? Ni nan amepokea? Mbona wengi hatujui?
Tuje kwenye makubaliano hayo ya twiga.
Sehemu pekee itakayoipatia faida nchi ni katika mrabaha na share yetu ya 16%, lakin tunafahamu kwenye share hapa faida inapatikana kwenye gawio(devidents) au kwa kuuza hisa za mwanahisa..
16% ipo kwenye divident wakati makampuni mengi makubwa ya uchimbaji madini hayatoi dividents. Faida kubwa kwa wanahisa wa makampuni ya madini ni kutokana na mauzo ya shares wakati zinapokuwa zimepanda. Kwa mfano tangazo hili tu la kusema Barrick imefikia maafikiano mazuri na serikali ya Tanzania, hisa za Barrick zitapanda, na baadhi ya wanahisa watauza hisa zao na kutengeneza faida. Kwa bahati mbaya serikali haitaziuza hisa zake kipindi chote, na hivyo kutokufaidi faida itokanayo ya kuongezeka thamani kwa hisa zake.
Jambo la pili, hata kama watatoa gawio, itakuwa ni baada ya muda mrefu maana kwenye migodi uwekezaji huwa ni mkubwa na haukomi. Bahati mbaya gawio ni mpaka baada ya Barrick kurudisha pesa yake aliyowekeza. Atarudisha lini wakati uwekezaji unaendelea? Ndiyo swali la kujiuliza
Kwa upande mwingine wa barick sasa tuangalie inafaidika vipi
Barrick katika hili wamefanikiwa sana kuliko hata mazingira ya mwanzo. Sasa wataweza kuipata hata miradi ambayo zamani wasingeipata. Maana ndani ya Barrick, sasa ipo serikali.
Kule kusakamwa kuwa mara Barrick wametiririsha maji ya sumu, mara Barrick wanawaonea wafanyakazi wazalendo, mara Barrick ni majizi na mabeberu - yote hayo sasa wameyashinda. Yamefikia mwisho. Hii sasa ni kampuni yetu. Kampuni ya Taifa letu inayobeba nembo ya Taifa, TWIGA. Mwenye kutaka kuihujumu kampuni hii kwa namna yoyote ile, anaihujumu kampuni ya serikali, atakuwa analihujumu Taifa. Na anayelihujumu Taifa amekosa uzalendo.