Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,467
- 1,697
- Thread starter
-
- #101
Sasa povu la nini?Unadhani serikali yetu inauwezo wa kuajiri watu wote wenye umri wa kufanya kazi? Zingatia kati ya trillion 1.3 inayokusanywa sasa, billion 600 ni mshahara kila mwezi achilia mbali matumizi mengine.
Kama unadhani inawezekana toa mwangaza wako makosa yalipo na nini kifanyike watu wapate ajira.
Magufuli yeye anadhani hilo swala ni impossible anafikiria long term solution kutengeneza miundombinu itakayotoa access ya kufikia sehemu mbali mbali na umeme wa uhakika kwa bei nafuu ili kuvutia uwekezaji wa private sector na kutoa ajira.
Sasa wewe kama una mbinu mbadala ya haraka ebu tuelezee utawasaidia vipi hao watu wenye kipato cha chini.
Kwanza napenda utambue kuwa mimi sio ndiye niliye panda jukwaani na kupayuka kuwa nchi hii ni tajiri, ni Rahis wetu mwenyewe ndiye ameyatoa hayo.
Pili mimi sio ndiye niliye hamishia wizara zote Dodoma kwa mabavu, ni matakwa yake.
Sasa naomba upige mahesabu ya costs zote za kuzipeleka wizara zote Dodoma na gharama za majengo yote ya wizara Dodoma. Alafu ongeza na costs za kuijenga infrastructure ya Dodoma within 5 years.
Ukisha maliza, naomba sasa linganisha na costs za kujenga mtambo mmoja wa kutengenza chuma.
Ukisha maliza, angalia chain ya agira zitakazo tokana na mtambo mmoja tu wa kuoka chuma.
Tuanze na kiwandani kazi zaid ya 3000 zingezalishwa directly.
Tuje kwenye mazingira: mji mpya unge anzishwa na ambao ungekuwa na facilities zote za kimji kama manispar ya mji, shule, ofisi, maduka, barabara, wafanya biashara, soko, usafiri, watoa huduma kama vinyozi, mafundi bomba, fundi seremala, fundi cherehani, fundi ujenzi na kadhalika na kadhalika.
Hapa kazi au ajira zaidi ya 200.000 zingeweza zalishwa.
Tuje kwenye viwanda ambavyo directly vitatumia hiyo chuma hapa nchini. Ajira ngapi zingezalishwa kwenye viwanda hivyo? Tuseme laki 7 na vitakavyo kuwa sio vya utumiaji chuma directly, tuseme milion moja na multiply effect yake karibu ajira ya watu milion tano zingezalishwa. Hapa tayari jumla ya ajira milioni saba zingeweza patikana.
Kwa hiyo utaona kuwa, kuwa na kiwanda kimoja cha kuoka chuma na LNG plant moja peke yake ajira sio chini ya milion 12 zingezalishwa. Hayo ni makadirio ya chini tu.
Tukiongeza Sekta ya maji taka na uangalizi wa barabara, commuter trains, Sky trains, SGR zaidi na Nyerere Dam mbona tungekuwa mbali?
Tukija kwenye skilled manpower au Labor kama; smithy, product Management, project engineering mechanical engineering, process engineerig, design engineering, products designers, mechantronic, Computer scientists, quality controlling managemet, na kadhalika na kadhalika. Tungekuwa na wataalam wa kujivunua.
Hapo tayari tuna scientific research institutes kwenye medicine, metallurgy, chemical, electrical, digital, telecommunication na kathalika na kadhalika
Hapo sijahesabu ongezeko la ajira kwenye sekta nyingigine kama; kilimo, uvuvi, utalii, afya, elimu na huduma nyingine.
Tunacho experience so far kwenye skilled manpower ni civil engineering kwa wingi sana, wanacho kifanya wala hatukioni. Ni usanii tu. Barabara hawajui kutengeza na kwenye mitaro ndiyo kabisa. Kwenye majumba ndiyo hivyo kulipua lipua. Magorofa yote makubwa na madaraja, wajenzi ni makampuni ya nje na wahindi.
Medical doctors kwa wingi pia, electricians na Electrical engineering, system adminstration na wajasiliamali kadha wa kadha.
Sasa katika hawa wako ambao wewe unawaona wanaweza anzisha viwanda vya kufanya manufacturing?
Kaa pembeni kijana tusileteane masihala.