Rais Magufuli kama unapenda nchi fikiria baada yako

Rais Magufuli kama unapenda nchi fikiria baada yako

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Magufuli anafanya kazi nzuri kwa ujumla hasa ukusanyaji kodi, miradi ya msingi na kurudisha heshima kwa kupunguza upotevu wa mali za Serikali. Lakini kuna vitu ambavyo haviko vizuri

1. Kwanza hakuna mikakati ya kubirosha mifumo ili iweze kwenda bila kutegemea watu. Hakuna mpangilio mzuri wa kazi ni kugombezana zaidi kuliko viongozi kujua madaraka yao ni yapi na wanatakiwa kufanya nini. Kazi ni vigumu kujua kama ni ya jiji au serikali kuu. Hakun mipaka mazuri endelevu ya madaraka

2. Kuua demokrasia kama nilivyosema wanaofurahia hawajui maana ni rahisi tu kupata kiongozi mbaya ambaye anaweza kuchukua madaraka hata kwa miaka 30 ijayo kwa sheria hizi hizi mbaya mabazo zinapitishwa kisheria. Nia nzuri ya Magu haiwezi kuchukuliwa kama kila siku itakuwa hivyo. Ni lazima sheria na mipaka na hata mikakati ya maendeleo iweze kwenda bila kutegemea mtu mmoja. Mkiua vyama iko siku tutatafuta jinsi ya kumpinga raisi mbovu na hatutakuwa na njia. Hii imetokea huko Sudan na nchi za kaskazini ya Africa.

Kama Magu anapenda nchi aweke misingi mizuri maana hawa viongozi wengine sio hivyo na sio wa kuwaamini. Kikwete alimwamini Lowassa lakini Lowassa alipoona pesa tu ya richmond tuliomwona mtu mpya. Kama kweli ni mzalendo kuza na si kubomoa demokrasia maana bila vyama hatutajua chochote. Angalieni hata China huko Hong kong hali ilivyo sasa. Hakuna sehemu ambako hakuna demokrasia na mambo yakawa shari kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom