Rais Magufuli kukabidhi jukumu la Uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji, Philipe Nyusi

Rais Magufuli kukabidhi jukumu la Uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji, Philipe Nyusi

Yaani kukabiziwa tz, halafu anakabizi hapa hapa tz, sijui juu uoga wa kusafiri unatokana na nini,
 
Mkutano wa 40 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC) unatarajiwa kufanyika leo Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo Rais John Magufuli anatarajiwa kukabidhi jukumu la uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi.

Mkutano wa Dodoma utafanyika kwa njia ya video kwa kuongozwa na Rais wa Msumbiji. Kaulimbiu ya mkutano huo ni;’Miaka 40 ya kuimarisha amani na usalama, kukuza maendeleo na kuhimili changamoto zinazoikabili dunia’

Rais Magufuli amekuwa Mwenyekiti SADC kwa mwaka mmoja. Alikabidhiwa jukumu hilo Agosti mwaka jana kutoka kwa Rais wa Namibia Dk Hage Geingob.

Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alizishukuru nchi 16 wanachama wa SADC kwa namna walivyoshirikiana na Tanzania kufanikisha ajenda muhimu za kikanda.

Waziri Kabudi pia alimshukuru Rais Magufuli kwa uongozi mahiri ulioziwezesha sekta za jumuiya hiyo kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC jijini Dar es Salaam.

"Ushirikiano wa pamoja umewezesha haya. Uongozi bora wa Rais John Joseph Pombe Magufuli umetuwezesha kufikia malengo ya SADC yaliowekwa. Ushirikiano mkubwa wa Sekretarieti ya SADC kupitia Dk Tax umewezesha haya. Mawaziri wenzangu kutoka nchi zote 16 za jumuiya wakiwamo mawaziri wa afya, wamefanya kazi kubwa kuikabili Covid-19)," alisema Profesa Kabudi.

Alisema Tanzania inashukuru kuwa, inapoachia kiti cha uenyekiti, ajenda ya viwanda kupitia Mkakati wa Viwanda (2015-2063) imebaki kuwa endelevu katika kukuza uchumi wa SADC na hatua za utekelezaji zimefanyika ikiwamo kuanzisha viwanda vya dawa.

Kabudi alitaja maeneo mengine ambayo Tanzania imefanikiwa kutekeleza kama kipaumbele chake kuwa ni Kiswahili kuridhiwa kuwa lugha ya nne ya SADC.

"Wapendwa mawaziri, tunayashukuru maamuzi ya Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC kwa uamuzi wa kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya nne ya Jumuiya yetu. Kiswahili ni lugha ya ukombozi iliyotumiwa na wapigania uhuru kama lugha ya mafunzo na mawasiliano wakati wa kupigania uhuru kusini mwa Afrika.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, chini ya Uenyekiti wa Tanzania, ajenda ya viwanda imetekelezeka kwa nchi wanachama kupata uwezo wa kutengeneza dawa zenyewe baada ya mataifa mengi duniani kuzuia dawa zisitoke nje ya nchi zao kutokana na mahitaji kuongezeka katika kudhibiti Covid-19 na nchi za SADC zilitengeneza vitakasa mikono, barakoa, mashine za kupumua na vifaa mbalimbali vilivyohitajika.

Alisema ni katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, Tanzania imefanikiwa kuingia katika nchi za uchumi wa kipato cha kati, miaka mitano kabla ya lengo lake.
Tumpongeze kwa kukikabidhi kwa amani na utulivu tofauti na nchi nyingine zinavyofanya, hii inaonesha jinsi gani watanzania tulivyo na upendo na ukomavu wa kisiasa.
 
Ina maana Mwenyekiti aliyepo madarakani hajui Kiingereza mpaka Mwenyekiti mtarajiwa aongoze kikao?

Si ajabu Mama Samia akawakilisha TZ kwenye video conference hiyo.
 
Back
Top Bottom