Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

kilichosemwa ninkuwa asilimia karibu 65% ya wapiga kura ni vijana
itapendeza wakiwekewa kijana mwenzao mwenye dam changa na mawazo mapya.
ni vision tu nayoona ni nzuri.
We, acha kupotosha kauli. JPM is always very serious with what he says. He is a final character in the game. He is alpha and omega.
 
hajavunja katiba bali kawapa ujumbe wale wote ambao wanautamani Urais. wasijiandae wala wasiandaliwe.......uongozi ni Karama kutoka kwa Mungu mwenyewe.
ukimuona mtu anakimbilia kwa waganga kutafuta uongozi huyo ni shetani
Tunachosema ni kuwa nchi yoyote inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, sasa ninachouliza je Rais Magufuli ametumia mamlaka gani nje ya Katiba ya nchi, kuwapiga "stop" akina Profesa Kabudi wasiwe na mawazo kabisa ya kugombea nafasi ya urais mwaka 2025?
 
Tunaposema kuwa CCM imehodhiwa na mtu mmoja muelewe kuwa tunamaanisha. Wanachama hawana tena uwezo wa kuchagua mtu wanayeona anafaa ila mmiliki wa chama ndiye anaamua kila kitu.
 

Attachments

  • FB_IMG_1589682992908.jpg
    41.8 KB · Views: 2
hajawapiga "stop" bali amewashauri tu, pia ametoa maoni yake, kama pia alivyo wahi kusema mtangulizi wake JK....kuwa "asingependa kuona Rais atakaye mrithi kumzidi umri......" hayo ni maoni tu sio zuio, na kauli hiyo haija walenga Kabudi tu bali na wengine wengi
 
Kwani Pascal Mayala mchumia tumbo anasemaje ?
 
Magufuli huwa hapimi maneno yake.

Huwa yanamtoka tu utadhani mtoto.
Tutamuelewa zaidi kipindi hiki cha pili. Kama anaongea hoja kama hiyo na sisi wabunge wa CCM kwa umoja wetu tunampigia makofi na vigerere unategemea yeye afanye nini zaidi ya kutimiza akitakacho. Mbunge "Bwege" alisema wabunge wa CCM hawajui kipi waseme NDIYO na kipi waseme SIYO. Wakiulizwa mmeshiba, wanajibu NDIYO, mna njaa, wanajibu NDIYO. Kwa hiyo hata huko kushangilia hiyo hoja ya Rais, hatujui walishangilia wakiwa upande upi kwa sababu wao kwao yote ni heri tu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Seriously?

Umeanza lini kunisoma hadi useme hivyo?

Hujawahi kuona nimemsema Magufuli hata mara moja?
Lakini hivi karibuni hasa baada ya huu "uchaguzi" au hata wakati wa kampeni, inaonekana umeguswa kwenye nerves hasa. Nadhani hii inatokea kwa watu wenye kujitambua kama wewe, kwa sababu huwezi kuufumbia macho ukweli. Lakini kuna wale ambao kwao liwake jua inyeshe mvua, ni vigeregere na mapambio tu.
 
hajavunja katiba bali kawapa ujumbe wale wote ambao wanautamani Urais. wasijiandae wala wasiandaliwe.......uongozi ni Karama kutoka kwa Mungu mwenyewe.
ukimuona mtu anakimbilia kwa waganga kutafuta uongozi huyo ni shetani
Umesahau? Yeye hakukimbilia kwa waganga 900 wa Gambushi kuzuia watu wasichukue fomu za kugombea urais CCM.
 
Umesahau? Yeye hakukimbilia kwa waganga 900 wa Gambushi kuzuia watu wasichukue fomu za kugombea urais CCM.
Magufuli ni mtu wa Mungu, ni mtu mwenye hofu ya Mungu, ni mtu mwenye kumtanbua Mungu, ni mtu anaye mtegema Mungu kwa kila jambo lake ndio maana anawachukia sana baadhi ya viongozi wanao endekeza na kutegemea ushirikina ili mambo yao yaende.
hata mimi siwapendi watu au mtu anaye tegemea ushirikina ili kupata kitu au kufanikiwa.

hatutaki viongozi wanao abudu ushirikina tunataka viongozi wenye hofu na Mungu hao ndio watakao tutendea haki
 
Mkuu hata Mm nlikuwa namchukulia Jamaa ni PRAISE TEAM
Huyo ni kigeugeu balaa , asilimia kubwa Ni kusifia utopolo wa Jiwe na ccm , baadaye timing chain ikikaa sawa anaponda the same person .
 
Hajavunja katiba mzee; usitafute visababu. Yeye katoa mawazo yake kama ambavyo hata mimi nilivyotoa mawazo yangu miezi michache iliyopita kuwa Lissu hawezi kuwa rais wa nchi hii; wanaotoa ridhaa ni wananchi siyo sisi mashabiki watoa mawazo!!
 
Kutembea na rundola wapiga ramli kwenye mavx ndio kumcha Mungu ? Labda mungu Nyamrunda wa ccm mwenge .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…