Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

Hajavunja katiba mzee; usitafute visababu. Yeye katoa mawazo yake kama ambavyo hata mimi nilivyotoa mawazo yangu miezi michache iliyopita kuwa Lissu hawezi kuwa rais wa nchi hii; wanaotoa ridhaa ni wananchi siyo sisi mashabiki watoa mawazo!!
Acha uongo , muogope hata mungu wenu wa CCM wa uongo mwenge Nyamrunda . Waliowapa ridhaa ni tissccm , tumeccm , polisiccm , wakurugenziccm sio wananchi hata Mhutu mwenyewe analijua hili since 2015 alipoambulia kura milioni 3 .
 
Kutembea na rundola wapiga ramli kwenye mavx ndio kumcha Mungu ? Labda mungu Nyamrunda wa ccm mwenge .
bora wapiga ramli kuliko wanao enda kwa washirikina na wachawi.
eeewe Mungu muongoze Rais wetu ateue watu sahihi sio wanao tumia nguvu za GIZA.
inaonekana asilimia kubwa wanatumia sana Nguvu za GIZA kupata uteuzi wa nafasi za uwaziri. wachache sana wanao mtegemea Mungu.
 
Acha uongo , muogope hata mungu wenu wa CCM wa uongo mwenge Nyamrunda . Waliowapa ridhaa ni tissccm , tumeccm , polisiccm , wakurugenziccm sio wananchi hata Mhutu mwenyewe analijua hili since 2015 alipoambulia kura milioni 3

Nakushauri ujifunze kukubaliana na ukweli usiokufurahisha, itakusaidia kujenga mbinu nzuri za kupambanao nao. Ukiamini kila usichokubaliana nacho ni uwongo, basi utabaki vile vile na hutaweza kujua wengine wanaona mambo hayo livipi.
 
Katika vitu ninavyopata ugumu kuvifanya ni pamoja na kumfuatilia mtu wa namna hiyo kujua atasema nini.
 
Kwa maoni yangu Magufuli kuna ujumbe alikuwa anataka kuufikisha na wala hauwahusu Kabudi wala Lukuvi, lakini ipo siku atasema ukweli wake, kama angekuwa anazungumzia swala la umri mkubwa kwa mshika kijiti wake basi angezumzia kwa ujumla, laikini kitendo cha kutaja majina ya akina Kabudi na Lukuvi ina maana kwenye akili yake kuna watu anaowalenga na anaowajua wanaanda mazingira ya uchaguzi wa 2025. ("Ushindi wa CCM") umechangiwa kwa kiasi kikubwa na vijana wafia chama hivyo nayo ni kauli ya kuwatia moyo vijana wajitutumue ili teuzi zisiwapite kushoto huenda mmoja wao akawa mgombea wa uraisi wa CCM. Lakini "you are free to make choice you want, but you are not free from consequences of the choice."
Maendeleo hayana chama.
 
Raisi Magufuli ni lazima aelewe kuwa maafikiano na system ya CCM tokea Hayati Baba wa Taifa alipimuachia kijiti Mwinyi, msimamo wa kupokezana ulikuwa ni Muislamu/Mkiristo/Muislamu/Mkiristo ...., sasa yete akitaka kubadilisha awe wazi tuu na hakuna kujificha.

Na huu mpango wa Raisi kuja na majina mfukoni, haruutaki tena, Tunamlaumu sana Kikwete kwa kutuletea mfumo huu mbaya.

Baada ya Magufuli, tunamhitaji kiongozi wa kuwaunganisha watanzania wote bila kujali chama, kabila au dini, tunahitaji mtu mvumilivu na atakayeendeleza miradi aliyoyabakiza Magufuli, maoni yangu ni mmoja kati ya hawa:
1. KINANA
2. VUA NAHODHA
3. SAMIA SULUH
4. JANUARY MAKAMBA
5. ASHA ROSE
6. DR. RAMADHANI DAU
 
Umeongea hayo maneno kwa kumaanisha?

Or you have uttered those words just for jokes?
 
Umeongea hayo maneno kwa kumaanisha?

Or you have uttered those words just for jokes?
ni ajabu kubwa sana!! yaani ktk karne hii unakuta msomi mzima anahangaika kwa waganga na washirikina kutafuta vyeo na utajiri, haswa watanzania tumeeendekeza sana tabia za kutegemea nguvu za giza.
 
Mkuu, huyo Joe Baden ndiyo nani?
 
Swali la msingi zaidi tujiulize kwa kusema hivyo ana mtu wake kishamweka akilini nwake na sasa anatutayarisha kisaikologia? Anajuaje kama raisi ajae atatoka CCM ambako ana madaraka katika uteuzi wake au ndo haya yaliyotokea mwaka huu?
 
Hiyo katika imevunjwa hata huwezi tena kuiunganisha. tilisha kosea tanga mwanzo
 
Labda nawe nikuulize: umeanza lini kunisoma?

Maana mimi wala sijabadilika.

Ngabu wa 2005/2006 wakati JF inaanzishwa ndo yule yule wa 2020.

Na ushahidi wa kimaandishi upo humu.

Wewe hujawahi kuona nikiiponda CCM kwenye mabandiko yangu ya 2006 au 2007? 2008? 2009? 2010?
 
Mimi nimeanza kukusoma tangu 2011 ndipo nilipo join JF. Kwa mabandiko mengi niliyofanikiwa kukusoma nimekuona katika mtazamo huo hasa kuanzia 2015. Nitajitahidi nikufuatilie kwenye mabandiko mengine tunavyoendelea kuelekea 2025.

Vinginevyo tuko pamoja mkuu.
 
Linavunja katiba kila siku hilo
 
Basi huenda una matatizo haya mawili:

1. Unajua kusoma na kuandika lakini una tatizo la kuelewa ulichokisoma.

2. U msahaulifu. Kwa sababu nina mabandiko mengi tu humu kuanzia 2015 yanayomkosoa Magufuli, Makonda, na CCM kwa ujumla wake pamoja na vyama vya upinzani na wanasiasa wa vyama hivyo!

Haiwezekani kwa mtu makini, mwenye uwezo wa kuelewa akisomacho na mwenye kumbukumbu nzuri, afikie hitimisho kama ulilolifikia wewe kuhusu mimi!
 
Kama Trump tu!
Tofauti ni kwamba angalau kwa Trump kuna sauti toka ndani ya Republicans wenzake za kutokukubaliana nae. Huku kwetu hakuna hata sauti moja ndani ya chama chake iliyo na itakayothubu kusema lolote dhidi ya Mwenyekiti na Rais wa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…