Tulimsikia Rais Magufuli wakati akimwapisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisema kuwa Profesa Kabudi na William Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya wagombea wa Urais wa CCM kwa mwaka 2025, kwa kuwa tu umri wao hauwaruhusu, kwa kuwa watakuwa na umri mkubwa, kwa kuwa ameeleza kuwa Rais ajaye atakuwa kijana na hataruhusu yeyote atakayekuwa na umri unaomzidi yeye Rais Magufuli, agombee Urais kwa mwaka huo wa 2025, je kwa kuyatamka hayo amevunja Katiba ya nchi?
Nimesoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,1977 ambayo imetaja sifa za mtu anayetakiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na inasema kama ifuatavyo katika ibara ya 39, kama ifuatavyo:-
39(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, isipokuwa kama:-
(a) Ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ya Urais
(b) Ametimiza umri wa miaka arobaini
(c) Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa
(d) Anazo sifa za kumwezesha kuwa mbunge au Baraza la Wawalikishi
(e) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi Mkuu, hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali
Katika masharti hayo naliona sharti la umri wa chini kabisa wa miaka 40 (minimum age) na sijaona kipengele chochote kinachomzuia mgombea yeyote kutokana na umri wa juu (maximum age)
Sasa nimuulize Rais Magufuli amepata wapi mamlaka nje ya Katiba ya nchi ya kuwatamkia akina Profesa Kabudi na William Lukuvi kuwa watakuwa disqualified kutokana na umri wao kuwa mkubwa?
Kwa kuwa kutokana na Maelezo yake hataruhusu mtu yeyote atakayekuwa na umri wa zaidi ya miaka 65, ifikapo mwaka 2025, kugombea Urais!
Hivi sisi wananchi tunaposema kuwa yeye Rais matamshi yake ndiyo yanakuwa sheria tutakuwa tunakosea kweli?
Hivi inawezekanaje yeye Rais Magufuli atoe matamshi, ambayo anajua wazi kuwa yanavunja Katiba ya nchi?