Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

Mkuu pole sana wewe unaye iheshimu hiyo katiba
 
Jamaa kaanza kuwaandaa watu kisaikolojia! Kwamba no one like him.. Lazima niseme na huo ndo ukweli wenyewee.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hivi hata mgombea atakuwa na umri kama Museveni au Joe Baden, atakuwa amevunja ibara ipi ndani ya Katiba ya nchi?

Sasa yeye Rais Magufuli anaposema kuwa Rais ajaye ni lazima awe kijana, je anatuandalia mtu wake wa mfukoni?

Tutakapokuwa tunahisi kuwa anatuandalia mtu wake wa dizaini ya Bashite, tutakuwa tunakosea kweli?
Upo sahihi
 
Hajavunja, maoni/msimamo yake kuhusu raisi ajae ni irrelevant. Hakuna anaejua nani atakua raisi baada ya yeye. Na Nguvu yake ya ushawishi imepungua tayari kwakua yupo kipindi cha mwisho cha uongozi wake.
 
Magufuli huwa hapimi maneno yake.

Huwa yanamtoka tu utadhani mtoto.
Urais siyo Nguvu za mwili kama kubeba Zege ni Ukomavu, Hekima, Busara na maarifa. Mu7 our friend is 70+ Yuko kwenye Kampeni hivi anajisikiaje?
 
Mara paap mda uwadie halafu atangaze hiyo nafasi anampa anaemtaka yeye sio Wanaccm.halafu anamteua gwajima au makonda apite bila kupingwa mtafanyaje?
 
Mkuu huyo mwamba ashatuona vilaza ndiyo maana anaongea anachojisikia. We huoni licha ya kuongea huo utopolo bado wabunge walimpigia makofi.
chuki za wazi kwa wabunge, pale ikulu kulikua na watu wengi sana na wengi tu walishangilia ila ww uliishia kuwaona wabunge
 
Haa😁😂😀😅😄😄😃😁😂🤣😅😄😄
Usimseme Mwenyekiti Vibaya 🤨😑😏😐
Wanachama Hatujapenda Kabisa 😁😂😅
Kiongozi Wetu Huwa Hakosei


Jamiiforums.com Ina Thread Nyingi Nzuri Sana
Katiba Imevunjwa Na Itaendelea Kuvunjwa
Mtake Msitake (Atake Asitake, Tutamuongezea Muda)😶🤨😑😎😐😏😏


Kosea Kuoa Lakini Siyo Kuchagua Ukikosea Kuchagua Ni Mpaka Baada Ya Miaka Mitano
Ila Tumeibiwa Uchaguzi Mkuu Huu
Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti.

Hiyo dhana siyo sahihi kabisa, kwa kuwa sisi kama binadamu kuna mahali huwa tunakosea.
 
hajavunja, maoni/msimamo yake kuhusu raisi ajae ni irrelevant. Hakuna anaejua nani atakua raisi baada ya yeye. Na Nguvu yake ya ushawishi imepungua tayari kwakua yupo kipindi cha mwisho cha uongozi wake.
Wewe wasema kuwa nguvu yake ya ushawishi imekwisha!

Hivi unadhani katika uchaguzi uliopita ulitumika ushawishi wowote?

Ni dhahiri kuwa washindi walitokana na nguvu ya dola, ambayo ni Polisi+Wasimamizi wa chaguzi+NEC
 
Haya ndiyo maajabu makubwa ya nchi hii.

Watu unaodhani wana uelewa wa kutosha kuweza kujua nchi yetu ilipo sasa hivi, inashangaza kuona watu hao hao wanajifanya kana kwamba hawaelewi chochote!

'Mystery' ni mmoja wa watu ninaojua wana uwezo mkubwa wa kifikra, kwa michango yao mbalimbali wanayoitoa hapa JF; lakini unapoendelea kuona aina ya mada kama hii wanapoileta hapa; hapo ndipo unapojiuliza waTanzania tuna akili za ajabu sana.

Sasa kwenye mada kama hii, wachangiaji wajadili nini, huku kila mtu hapa anajua asemalo huyo anaye elezwa kutoa maelekezo amekwishatamka? Kuna nini tena cha kujadili hapo kama sio kusubiri tu wakati ufike atimize alicho ahidi? Ni lini alipotamka jambo akashindwa kulitekeleza kwa sababu yoyote ile?

Kaamrisha uchaguzi uliopita anataka pasiwepo wapinzani, huyajui matokeo? Alisema 'wasaliti' adhabu yao ni kuuawa..., na mengi mengine!

Sasa watu wajadili nini hapa juu ya hili la akina Lukuvi?
 
Mkuu huyo mwamba ashatuona vilaza ndiyo maana anaongea anachojisikia. We huoni licha ya kuongea huo utopolo bado wabunge walimpigia makofi.

Na kwa hakika sisi ni VILAZA katika umoja wa vilaza.
 
kilichosemwa ninkuwa asilimia karibu 65% ya wapiga kura ni vijana
itapendeza wakiwekewa kijana mwenzao mwenye dam changa na mawazo mapya.
ni vision tu nayoona ni nzuri.
 
Ukweli ni kuwa ni lazima mtu unapokuwa na nafasi kubwa kama hiyo ya Urais upime kila unachokitamka, mbele ya hadhara..........

Cha kushangaza ni kuwa kwa Rais tuliye naye hapimi kabisa madhara ya maneno yanayomtoka

Kwanza ni lazima ajue kuwa nchi yetu ina mfumo wa vyama Vingi, kwa hiyo hapaswi kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa ni lazima mshindi wa kiti cha urais ni lazima atoke kwenye chama chake cha CCM!
He is alpha and omega. Kila anachotaka kitafanyika. That is his conviction.
 
kilichosemwa ninkuwa asilimia karibu 65% ya wapiga kura ni vijana
itapendeza wakiwekewa kijana mwenzao mwenye dam changa na mawazo mapya.
ni vision tu nayoona ni nzuri.
Tangu lini taifa hili wazee wa 60+ wamewazidi idadi vijana wa 18+ mpaka 50? Kwanini hatukuona hayo? Halafu Leo mtu amasema huwezi kuwa rais kwa sababu una umri kubwa how? Tuweni makini kama taifa.
 
hajavunja katiba bali kawapa ujumbe wale wote ambao wanautamani Urais. wasijiandae wala wasiandaliwe.......uongozi ni Karama kutoka kwa Mungu mwenyewe.

ukimuona mtu anakimbilia kwa waganga kutafuta uongozi huyo ni shetani
 
Huku mnaema hamumtambuwi kama Rais, huku mchana kutwa na bila shaka usiku pia mnakesha mitandaoni kumfuatilia.
Je unamfuatiliaje mtu usiemtambua?

Mbona msimfuatilie mwamba wa kaskazini au tundu wenu.
Badala ya kujikusanya muangalie mlipokosea na muanze kujijenga upya kwa wapiga kura.

Nyinyi mnakaza misuli kukodolea TV na kumfuatilia mtu anaetimiza alichokiahidi kwa wananchi waliomchagua.
Hayo ndio yamewakosesha nafasi zote mlizopoteza kwenye uchaguzi uliopita.
 
Back
Top Bottom