Ndugu wana bodi,
Ningependa wale wote waliokunywa mvinyo wa vyama vyao au hawapo kuwasilisha mawazo na mitazamo yao huru na binafsi nawaomba kwa heshima na taadhima wapite hivi thread zipo nyingi humu JF, huu ni wakati sasa tunajenga Taifa tuko serious.
Nikirudi kwenye hoja ambayo ipo muda mrefu kidogo kuhusu mbio za mwenge kuna mawazo mchanganyiko hapa, kuna wale wanaotaka mwenge uwekwe jumba la makumbusho ubaki kuwa historia tu na kuna ambao wanaona mwenge uendelee lakini uwe kama kifimbo cha malkia ambacho kinakimbizwa kila baada ya miaka minne minne ila sisi tunaweza kuweka miaka sita sita au kumi.
Pia kuna kundi hili la tatu na bila kumung'unya maneno ni kundi la wanufaika wa mchezo huu wa mwenge, ukiwasikiliza hoja yao kuu ambayo ni dhaifu kabisa wanakwambia Mwenge unazindiwa miradi mingi ya maendeleo kana kwamba vile pesa za mwenge ndio zinagaramia ile miradi. Insanity.
Binafsi mimi mara ya mwisho kuchangia mwenge ni utawala wa Mwinyi kwa sababu ilikuwa shuleni ni lazima tuchangie mwenge, lakini kwa sasa kama afisa mtendaji hajipendi basi aje kwangu kunieleza habari za kuchangia mwenge kitakachopata atakuwa sample ya Taifa.
Kwahiyo mwenge umebaki kuwa mradi wa kuwakandamiza walimu kuwachangisha kinguvu (nipo tayari kukosolewa kama wameacha kuwalazimisha kuchangia mwenge) pili kuwandamiza wafanyabiashara hasa mabar maguest , mahotel hasa mikoani maana Dar watu wamepinda hata OCD anaweza kuliwa mitama.
Hivyo basi kwa maoni yangu binafsi kati ya mwenge na muungano mimi naona muungani ni zaidi ya mwenge, sasa najenga hoja kama Rais ameona umuhimu wa kuokoa pesa za kufanya sherehe za muungano kwa mwaka huu ili ziende moja kwa moja kwenye shughuli za maendeleo, je wadau huu si ni wakati muhafaka wa wa Rais kutumia option one kusitisha kwa miaka kadhaa au kuupeleka moja kwa moja jumba la makumbusho for good.
Naomba wadau tuweke mihemko ya vyama pembeni mimi chama changu ni Rais Magufuli, karibuni tuchangie kwa weledi na kwa mdau anayejuwa bajeti ya kukimbiza mwenge ni kiasi gani atuwekee hapa hili Rais apelekewe taarifa sahihi mchwa bado wengi wamemzunguka kila upande. Wale wanaohubiri uzalendo hebu onesheni uzalendo wenu hapa. Ni wakati sasa kila mtu ale kwa jasho lake tu.
Hapa kazi tu.
Cc:
Pasco Manyerere Jackton Nyani Ngabu Kiranga