Rais Magufuli: Msichague wanasiasa wanaohubiri chuki, vurugu zikitokea wao watakimbia kwenda kuishi kwingine

Rais Magufuli: Msichague wanasiasa wanaohubiri chuki, vurugu zikitokea wao watakimbia kwenda kuishi kwingine

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532


RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kutochagua wanasiasa wanaohubiri chuki na kutoa maneno ya vitisho.

Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 14 Agosti 2020, katika maadhimisho ya miaka 13 ya moto kwenye Mkutano Mkuu wa Kanisa la Assembly of God (TAG) jijini Dodoma.

“Hivyo, nawasihi wanasiasa wenzangu tujipange kufanya kampeni za kistaarabu, tusitumie lugha za kuwatisha wananchi wetu, niwaombe Watanzania tuwakatae wanasiasa wanaohibiri chuki na kutoa maneno ya vitisho,” amesema Rais Magufuli.
Katika kusisitiza hilo, Rais Magufuli amesema “wanafanya hivyo kwa vile hawana sera za kuwaambia wananchi, lakini wanajua vurugu zikitokea wao wanapakwenda kuishi.”

Rais Magufuli amesema, Serikali anayoiongoza itahakikisha kwamba uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, unakuwa huru na haki.

Pia amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanaliombea Taifa ambalo ni miongoni mwa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pamoja na kuzungumzia masuala mbalimbali, Rais Magufuli amegusia suala la uchaguzi mkuu akisema, “uchaguzi ni zoezi muhimu katika kupata viongozi kwa njia ya kidemokrasia.”

Amewasihi viongozi wote wa dini nchini kutumia nafasi walizonazo kuhimiza waminini kushiriki katika uchaguzi huo utakaofanyika siku ambayo si ya kusali kwa wamumini wa dizi zote “siku hiyo itakuwa ya mapumziko.”

“Hatuna budi kumwomba Mwenyezi Mungu atupatie viongozi wenye maono, wachapa kazi na wazalendo kwa Taifa letu, tusiangukie mikononi mwa viongozi wabadhirifu, wabinafasi au vibaraka,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, kazi ya viongozi kama hao huwa ni kubomoa badala ya kujenga, kung’oa badala ya kupanda na kutawanya badala ya kukusanya “hivyo Mwenyezi Mungu atujalie hekima ili tufanye maamuzi yaliyo sahihi.”

Rais Magufuli amesema, katika baadhi ya nchi, wakati mwingine zoezi la uchaguzi imekuwa chanzo cha kuzuka kwa vurugu na fujo.

“Niwaombe viongozi wa dini kuliombea na kuliweka Taifa letu katika mikono ya Mungu ili tumalize salama uchaguzi na kubaki na amani, umoja na mshikamano kama taifa.”

“Kwangu mimi naliona Taifa la Tanzania muhimu zaidi kuliko mifarakano ya mambo mengine. Napenda kuwathibitishia kama Serikali nilivyoahidi hapo nyuma, tumejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na haki,” amesema na kuongeza:

“Sisi kama Watanzania tusimame kama Taifa moja, vyama visitugawe na dini zisitugawe na makabila yasitugawe, sisi tuishi. Nina imani viongozi wa dini wakisimama sisi tutavuka salama,” amesema Rais Magufuli.
 
Hapana shaka tuko pamoja Rais wetu kipenzi cha wengi, lazima umwadabishe yule jamaa aliyetoka ughaibuni akitaka kutuharibia amani ya nchi yetu halafu yeye atokomee tena atuache tukiomboleza,huyu tutamuadhibu kwa kipigo cha kenge.
 
Hapana shaka tuko pamoja rais wetu kipenzi cha wengi ,lazima umwadabishe yule jamaa aliyetoka ughaibuni akitaka kutuharibia amani ya nchi yetu halafu yeye atokomee tena atuache tukiomboleza,huyu tutamuadhibu kwa kipigo cha kenge.
Wewe sijui unahitaji kufunzwa au pengine hata hufundishiki kutokana na uwezo mdogo!

Rais ameongea maneno ya busara na hekima, wewe unakuja kuyatia unajisi.

Maneno ya Rais yamekaa vizuri, lakini tatizo kubwa la Rais Magufuli ni kunena tofauti na kutenda tofauti. Ja pili ni namna ya kuwadhibiti wanaojipendekeza kwaje au Serikali kwa kuharibu taratibu na sheria, hasa jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi linatakiwa kudhibitiwa. Linaweza kutuharibia mchakato wa uchaguzi, linaweza kusababisha vurugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magu anasitahili kutunukiwa either degree ya kusahau ama ya kujitoa ufahamu, yaani just in a month amekwisha sahau ubaguzi, vitisho, double standards na chuki alizozieneza miongoni mwa watanzania for five good years kiasi Cha kupiga U- turn sasa. Kwa kweli he is so abnormal and unique
 
Wewe sijui unahitaji kufunzwa au pengine hata hufundishiki kutokana na uwezo mdogo!

Rais ameongea maneno ya busara na hekima, wewe unakuja kuyatia unajisi...
Tatizo maneno ya mtu yanapokuwa tofauti na matendo hata akisema nini inaonekana kama amesema ujinga. Anayosema Magufuli, anavyo act kama mcha Mungu na mtu mwema, mwenye upendo ni tofauti kabisa na serikali yake inavyotenda.

Kosa alilofanya la kukataza mikutano ya wapinzani limeenza kumrudi yeye kwani hakutegemea kabisa kuwa upinzani bado una nguvu kiasi hiki. Naona kama kuna ku-panic kwa upande wa serikali na tayari wanaanza kufanya mambo ya kihuni kabisa.
 
Nyinyi vyeti feki amuishi sababu za uzushi kumpinga JPM kisa tu aliwatumbua.
Tatizo maneno ya mtu yanapokuwa tofauti na matendo hata akisema nini inaonekana kama amesema ujinga. Anayosema Magufuli, anavyo act kama mcha Mungu na mtu mwema, mwenye upendo ni tofauti kabisa na serikali yake inavyotenda.

Kosa alilofanya la kukataza mikutano ya wapinzani limeenza kumrudi yeye kwani hakutegemea kabisa kuwa upinzani bado una nguvu kiasi hiki. Naona kama kuna ku-panic kwa upande wa serikali na tayari wanaanza kufanya mambo ya kihuni kabisa.
 
Kama yeye alivyokimbia Corona akaenda kuishi burigi karibu 53 days!
Tena umshukukuru sanaa maana alienda kutafuta ufumbuzi vinginevyo ingetukosa COVID19 basi ingetuua njaa
Tano tena kwa John Pombe Magufuli kiboko ya COVID 19
 
Back
Top Bottom