Watanzania wenzangu nawaomba tuwapige na kuwakataa watu wanaotaka kuvuruga amani yetu. Amani tuliyo nayo ni muhimu sana katika maendeleo ya Tanzania, kuna watu wenye nia ovu huku wakijificha kwenye mwavuli wa chama chao wakidai wanatafuta haki; haki gani mnayoitafuta?
Watanzania tunachotaka nimaendeleo na tayari tumempata Rais mwenye uchungu wakuleta maendeleo. Katika awamu ya kwanza ya miaka mitano ya Raisi Magufuli amefanya mengi mfano vituo vya afya kila kata, hospitali za wilaya, hospitali za kanda zimejengwa, umeme karibia vijiji vyote Tanzania vina umeme, miundo mbinu ya reli na barabara kila kona ya nchi yetu inajegwa, mikopo kwa wanafunza wa elimu ya juu imetolewa kwa kiasi kikubwa.
Nidhamu kazini kwa wafanyakazi, mishahara mwaka huu imeongezwa, ametimiza ndoto ya baba wataifa kuhamia Dodoma, Magufuli kaweza kuthibiti majizi ya Rasilimali zetu.
Nawaombeni Watanzani tuwakatae kwa nguvu zote hawa watu na hichi chama kinachotumiwa na mabeberu kuharibu Amani ya nchi yetu. Tumchague JPM kwa kipindi kingine cha miaka mitano.