Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Mbona waliopotea na kurudi kumekuwa na ukakasi walikuwa wapi?Halafu jukumu la Ulinzi na usalama wa Watanzania ni lako wewe Amiri Jeshi Mkuu.Sasa kama hivyo vitendo havikomeshwi nani wa kulaumiwa kama sio wewe?
Kwanza watu walipokuwa wanawahusisha usalama wa taifa na utekaji alikuwa ametoa ruhusa hiyo hadi sasa hivi ndo apige marufuku?

Ingekuwa sio hao basi hata Roma mkatoliki asingeona taabu kusema waliomshikilia siku zote zile na ukisikiliza waliokamatwa pamoja na Roma na maswali waliyokuwa wakiulizwa huwezi kupata taabu sana kujua walitekwa na nani
 
Kama Mh rais anajua kuwa bensaa8 na azorygwanda wameenda kwa wapenzi wao na wako salama ni jambo la kushukuru Mungu na kumshukuru mh rais kwa kutuhabarisha jambo ambalo wananchi walikuwa hawalijui
Cha muhimu ni vyombo vya habari viwajulishe watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
una ushahidi kuwa Usalama wa taifa ndio wanahusika na utekaji? haya ndio Mh. Rais amesisitiza watu kama ninyi mchukuliwe hatua..

Hakika mnaudhi sana..
Kwani kule Mara kwa Zakaria hawakujulikana?? Maana Adam Malima aliwatambulisha kabisa.
 
Alijuaje kama ni kikosi kazi?
Kulingana Mdude walikuwa wakimweleza hivyo .Sasa ni jukumu la vyombo Vya Ulinzi na usalama KuProve wrong kwa kuwakamata hao wahalifu.Bila hivyo wasikwepe hizo tuhuma!
 
Kutisha watu sio suruhisho dawa hapa ni kutafuta Kwann usalama wa Taifa unahusishwa na maswala hayo ya utekaji?
Zitt Kabw na Wanasiasa wa Upinzani TZ kwa utafiti Wangu nilioufanya wanaishi kwa siasa za Matukio/Kiki ili waonekane kwenye jamii kama nao Wapo, Wanaweza kuvitukana vyombo vya dola bila kuchukuliwa hatua yoyote ile ya kisheria kutokana na kujua TIS siyo Chama cha Siasa na ni chombo nyeti ambacho hakina muda wa kujadili masuala ya uongo na uchonganishi.

Kwa tabia hii ya ovyo Waliitumia baadhi ya viongozi wa upinzani kutaka kuwaondoa Duniani rivals wao kwenye Vyama na waliposhindwa hadith eti ni vyombo vya dola. Hii inapatikana TZ pekee Mwanasiasa badala ya kuongea sera anatafuta Kiki za kutafuta Huruma za kura kutoka kwa wapiga kura.

For that extent, naunga hoja ya Rais kila atakaye ituhumu TIS aombwe kutoa ushahidi na akishindwa kuthibitisha achukuliwe hatua kali kisheria. Kwani asili ya Wakong na Warund hawa akina Zitt Kabw kwao bila kuongea uongo wanaumwa kabisa ndiyo maana hata Madiwani wa ACT Waza katika Manispaa ya Kigoma ujiji wamemgundua kuwa ni
Kanjanja na wameapa hata awashawishi vipi usoni watamkubali ila mioyoni nooo. Eti anawapiga biti anawavua uanachama Wakati akiwa anajua ACT Wazalend ni kachama kachanga ambako hakajai hata kwenye kucha ya Chadema.

Alifanikiwa kuwanunua akina Omar Gind, Kachech,
Kalyang 😆😆😆😆😆😆😆😆 ety wanajiita Chama asisi wa mienendo ya Mwalimu wakati kutwa wanalilia kugawana Rushwa, kuibia Manispaa Mapato, kuuza maeneo ya wazi, kumiliki makampuni ya ukandarasi Mfano iliyojenga Shule ya Msingi Kigoma ni ya Zitt Kabw, kuwatishia wakuu wa Idara haswa MT ili awape posho bubu, kushinda Manispaa kutwa kama Watumishi wa Manispaa kuombaomba virushwa na hela za kula na kusababisha kero kwa Watumishi.
 
😀 😀😀😀Mzee kanifurahisha " eti mtu katoroka kaenda kwa mgang" Usalama wa Taifa
 
Kama hawahusiki waliopotea nani kawachukua? Wasiojulikana ni
Acha kupoteza muda
Kama ndugu yako kapotea onesha ushahidi kuwa kachukuliwa na usalama
Acha kuleta maswali yasio na tija
Assad alizima simu Zitto akachafua hali ya hewa mpaka bendera fuata upepo wakawa tayari kusoma itikafu,je angechelewa kuwasha simu hiyo itikafu si ingewarudia wasomaji
Tumekuwa ni taifa la wazushi tu
 
Anataka tukae kimya ili aendelee kula nyama za watu? No way.

Anajua siku hizi akiteka tu mtu anabanwa kila kona hadi anamtuma Mambosasa kusema aliyetekwa alipo.

Hatunyamazi, aendelee kutukamata kama ni kweli ana magereza ya kutujaza sisi sote!
Inaelekea ishu ya kushindwa kuwamaliza Kabendera na Tito bado inamuuma sana.
 
Huyu anajitoa ufahamu tu! Zakaria asingewachakaza kwa risasi wale watekaji angekuwa amepotea mpaka leo! Mbona hao ilikuja kujulikana ni TISS? Watu waache ujinga!
 
Back
Top Bottom