Rais Magufuli mtumbue Bosi wa TTCL anaihujumu kampuni

niliomba uwakala wa TPesa....sasa ni mwakka mzima wanajichanganya...nimefuatilia mpaka nimenyoosha mikono...sijui wanakwama wapi hawa jamaa
 
The Black Godfather,
Si afadhali huyu angalau hata tumepata simu za mkononi kuliko huyu aliyekula fedha za maskini wa maskini za TASAF na hakutumbuliwa akasamehewa akaambiwa arudishe.

Arudishe na riba basi na awaombe msamaha Watanzania.Hata yale makontena alisamehewa hivihivi.Lakini Mungu yupo.
 
wafanyakazi wote wa umma walishurutishwa na Baba Jurgen watumie line za TTCL 🤣 🤣 🤣
 
Kwani Bashite alikuwahi kuwa meneja wa TTCM?
 
niliomba uwakala wa TPesa....sasa ni mwakka mzima wanajichanganya...nimefuatilia mpaka nimenyoosha mikono...sijui wanakwama wapi hawa jamaa
kuna Mangi alienda kununua voha za jumla akaambiwa subiria mpaka sijui nani aje ndio atie saini ili awepe hizo vocha.
MPAKa leo ukienda kwa Mangi haupati vocha za TTCL ila vocha zingine anazo
 
Ainisha ubovu wa huduma za TTCL.Tuanzia hapo kamanda!
 
Naunga mkono hoja. Taasisi kubwa ya serikali kwa nini ishindwe ns taasisi ndogo ya mtu binafsi. Aondolewe maana ameshindwa. Awapishe wengine watakaoweza kuiongoza kampuni ya TTCL.
Jamaa yupo tu ofisini katulia ghorofani anaangalia mandhari ya jiji ilivyo.
 
tafuta uzi uliletwa na jamaa nani sijui wa buza huko alilalamika alitoka buza mpaka posta makao makuu ya ttcl kwa ajili ya kununua vocha ya 500 na akaambiwa zipo za 1000
 
Nimeenda kwa mawakala wa kusajili zaidi wa wanne wanasema hawakamilishi ttcl kwa sababu kifaa cha ttcl(scaner) cha kukamilisha hawana,

Mmoja nikamwambia si afate ofcn,akanambia wamemwambia wanasubiri bajet

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilitupa Laini baada ya kuhangaika Siku nzima bila kupata Salio..... Nilivyowasiliana nao wakaniambia niweke Hela Mpesa kisha nihamishie TPesa ninunue Vocha.

Hapo hapo nikaamua kuachana nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…