Rais Magufuli na historia isiyofutika

Rais Magufuli na historia isiyofutika

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Emmanuel J. Shilatu

Kama ambavyo Watanzania tunavyomkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kusaidia ukombozi wa upatikanaji wa uhuru ama kama ambavyo Hayati Moringe anavyokumbukwa kwa mapambano ya ubadhirifu wa mali za umma, pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anazidi kujenga historia ya kipindi chote isiyofutika kutokana na utendaji, uchapakazi na uzalendo wake kwa Taifa.

Haya hapa ni baadhi ya Mambo ya kihistoria na yenye heshima kubwa kwa Taifa ambayo Rais Dkt. Magufuli aliyoyafanya;-

*(i) Kuhamia Dodoma*

Wazo la Serikali kuhamia kwenye makao makuu ya nchi mkoani Dodoma liliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwaka 1973 lakini lilishindwa kutekelezwa katika awamu zote. Si awamu ya kwanza, wala ya pili, ama ya Tatu au ya nne bali limeweza kufanikiwa kwenye utawala wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli. Leo hii karibia Serikali yote imehamia Dodoma. Wizara, taasisi na idara za Serikali, Waziri Mkuu wameshahamia Dodoma. Mwishoni mwa mwaka huu Rais Magufuli naye atahamia Dodoma. Iliasisiwa na Mwalimu Nyerere, ikahaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi, imekuja kutekelezwa vyema na Rais Magufuli. Hii ni historia isiyofutika ya uthubutu, uzalendo alionao Rais Magufuli.

*(ii) Ujenzi wa Miundombinu*

Hili halina ubishi kwa asilimia kubwa kabisa miundombinu ya nchi hii imejengwa chini ya usimamizi wa Dkt. Magufuli toka alipokuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Ujenzi na sasa Rais wa nchi. Hauwezi ukazungumzia uwepo wa mitandao ya barabara nchi nzima pasipo kumtaja Rais Magufuli; hauwezi kuzungumzia uwepo wa madaraja makubwa ya kisasa kama ya Daraja la Nyerere, Daraja la Mkapa pasipo kumtambua mchango wa Rais Magufuli. Leo hii nchini tunajivunia uwepo wa flyovers. Rais Magufuli ameonyesha uwezo na heshima kubwa ya ujenzi wa Miundombinu nchini ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kimawasiliano, usafirishaji wa Watu na mizigo, kukuza utalii, kuimarisha shughuli za kibiashara na kuongeza mapato ya nchi.

*(iii) Kulifufua Shirika la Ndege*

Tangu mwaka 1977 nchi yetu ilikuwa na shirika la ndege linalosua sua na linalojiendesha kihasara kubwa. Mara baada ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli imefanikiwa kununua ndege mpya 7 na mpaka sasa zimeshawasili ndege mpya 4 ikiwamo ndege kubwa aina ya Boeing 787-8. Wale baadhi wanaosema ndege si kipaumbele wala muhimu kwa Watanzania inabidi watambue Leo hii makusanyo ya mapato ndani ya Shirika la ndege (ATCL) yametoka Tsh. Milioni 700 mpaka kufikia Tsh. Bilioni 4.5. Hii ndio faida ambayo Watanzania tumeipata ya kuwa na kiongozi mwenye maono na mtazamo wa mbali zaidi, Rais Magufuli.

*(iv) Ujenzi wa Stiegler’s Gorge*

Utawala wa awamu ya kwanza uliokuwa ukiongozwa na Mwalimu Nyerere ulikuja na wazo wa kujenga Stiegler’s Gorge mnamo mwaka 1981 lakini umeshindwa kufanyika mpaka awamu hii ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli umeamua kufufua na kuliendeleza wazo hili. Mradi wa Stiegler’s Gorge kupitia Mto Rufiji utafanikiwa kuzalisha Megawattz 2100 utakapo kamilika. Ukamilifu wa mradi huu utajenga uhakika wa umeme nchini, utashusha bei ya umeme nchini na pia utamjengea Rais Magufuli heshima kubwa isiyofutika.

*(v) Mapambano dhidi ya Rushwa na ufisadi nchini.*

Rais Magufuli ameingia kwenye historia ya kiongozi ambaye Serikali anayoiongoza kuwa na mapambano ya dhahiri ya rushwa na ufisadi nchini. Tumeshuhudia Mafisadi Papa ambao walikuwa hawashikiki wala kukamatika wakipandishwa Mahakamani. Katika miaka ya nyuma ilikuwa suala gumu sana kwa Watuhumiwa “Mapapa” kuguswa tu, achilia mbali kupandishwa Mahakamani. Haya ni mapambano ya wazi wazi ya Serikali ya Rais Magufuli ya vita dhidi ya rushwa na ufisadi nchini. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na 2017 na pia ikishika nafasi ya pili (2) kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

*(vi) Uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za nchi*

Tumeshuhudia Serikali ikiweka uwazi kwenye mikataba na uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya yenye tija Mathalani tumeona uwazi wa sekta ya madini ya dhahabu, almas na Tanzanite ambapo Taifa tumeona namna ambavyo tulivyokuwa tukiibiwa na Serikali kuweka mikakati mipya ya kutokuibiwa tena. Kama haitoshi tumeshuhudia wawekezaji wakibanwa vilivyo juu ya mikataba isiyokuwa na tija kwa Taifa. Ni Serikali ya Rais Magufuli iliweka uthubutu wa kuwabana wawekezaji wa madini wa ACACIA iliyozaa matunda kwa Serikali ya Tanzania kumiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini, Serikali kupata gawio la faida ya madini ya asilimia 50 kwa 50. Yote haya yamewezekana kwa sababu ya uzalendo wake Rais Dk. Magufuli

*(vii) Ujenzi wa Bomba la Mafuta*

Serikali ya Rais Magufuli imefanikisha vilivyo kushirikiana na nchi ya Uganda kujenga Bomba la Mafuta linalotoka nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania. Ujenzi huo wa bomba la mafuta utazalisha ajira nchini na utaongeza pato la Taifa. Hayo yote yamefanikiwa kutokana na Serikali ya Rais Magufuli kuzidi kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo.

*Itaendelea …..*
*Shilatu E.J*
 
Nilipoona jina tu shilatu,hata sikutaka kujisumbua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Historia ya kununua kivuko kibovu

Historia ya kukwapua 1.5 trillion pesa za umma.

Historia ya kusimamia manunuzi ya wabunge wa upinzani.

Historia ya kulazimisha matokeo yaliyo kinyume na matakwa ya wananchi.

Historia ya kulindwa na maafisa usalama toka nchi jirani.

Kweli anayo historia iliyotukuka.
 
..Alphonce Mawazo.

..Ben Saanane.

..Aquilina Akwilini.

..Azory Gwanda.

..Simon Kanguye
 
Hayo uliyosema ni kweli japo hayajaiva sana na matunda yake bado kuonekana! Ukichambua mambo uwe unaangalia pande mbili pia ikimkuwa fair na kuondoa bias!
Hebu ongezea yafuatayo ambayo hayatasahauluka pia
1) Watu wasiojulikana
2) Watu kupotea
3) Watu kupigwa risasi
4) Kukiukwa kwa katiba
5) Kununua wapinzani badala ya kuwekeza kwenye maendeleo
6) Kukandamiza demokrasia ( refer from 4 above)

Naomba mwingine aendeleze, kila mtu ana mazuri yake na udhaifu wake, judgement inakua natural kutokana na yapi yamekuwa mengi!
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Kama ambavyo Watanzania tunavyomkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kusaidia ukombozi wa upatikanaji wa uhuru ama kama ambavyo Hayati Moringe anavyokumbukwa kwa mapambano ya ubadhirifu wa mali za umma, pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anazidi kujenga historia ya kipindi chote isiyofutika kutokana na utendaji, uchapakazi na uzalendo wake kwa Taifa.

Haya hapa ni baadhi ya Mambo ya kihistoria na yenye heshima kubwa kwa Taifa ambayo Rais Dkt. Magufuli aliyoyafanya;-

*(i) Kuhamia Dodoma*

Wazo la Serikali kuhamia kwenye makao makuu ya nchi mkoani Dodoma liliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwaka 1973 lakini lilishindwa kutekelezwa katika awamu zote. Si awamu ya kwanza, wala ya pili, ama ya Tatu au ya nne bali limeweza kufanikiwa kwenye utawala wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli. Leo hii karibia Serikali yote imehamia Dodoma. Wizara, taasisi na idara za Serikali, Waziri Mkuu wameshahamia Dodoma. Mwishoni mwa mwaka huu Rais Magufuli naye atahamia Dodoma. Iliasisiwa na Mwalimu Nyerere, ikahaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi, imekuja kutekelezwa vyema na Rais Magufuli. Hii ni historia isiyofutika ya uthubutu, uzalendo alionao Rais Magufuli.

*(ii) Ujenzi wa Miundombinu*

Hili halina ubishi kwa asilimia kubwa kabisa miundombinu ya nchi hii imejengwa chini ya usimamizi wa Dkt. Magufuli toka alipokuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Ujenzi na sasa Rais wa nchi. Hauwezi ukazungumzia uwepo wa mitandao ya barabara nchi nzima pasipo kumtaja Rais Magufuli; hauwezi kuzungumzia uwepo wa madaraja makubwa ya kisasa kama ya Daraja la Nyerere, Daraja la Mkapa pasipo kumtambua mchango wa Rais Magufuli. Leo hii nchini tunajivunia uwepo wa flyovers. Rais Magufuli ameonyesha uwezo na heshima kubwa ya ujenzi wa Miundombinu nchini ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kimawasiliano, usafirishaji wa Watu na mizigo, kukuza utalii, kuimarisha shughuli za kibiashara na kuongeza mapato ya nchi.

*(iii) Kulifufua Shirika la Ndege*

Tangu mwaka 1977 nchi yetu ilikuwa na shirika la ndege linalosua sua na linalojiendesha kihasara kubwa. Mara baada ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli imefanikiwa kununua ndege mpya 7 na mpaka sasa zimeshawasili ndege mpya 4 ikiwamo ndege kubwa aina ya Boeing 787-8. Wale baadhi wanaosema ndege si kipaumbele wala muhimu kwa Watanzania inabidi watambue Leo hii makusanyo ya mapato ndani ya Shirika la ndege (ATCL) yametoka Tsh. Milioni 700 mpaka kufikia Tsh. Bilioni 4.5. Hii ndio faida ambayo Watanzania tumeipata ya kuwa na kiongozi mwenye maono na mtazamo wa mbali zaidi, Rais Magufuli.

*(iv) Ujenzi wa Stiegler’s Gorge*

Utawala wa awamu ya kwanza uliokuwa ukiongozwa na Mwalimu Nyerere ulikuja na wazo wa kujenga Stiegler’s Gorge mnamo mwaka 1981 lakini umeshindwa kufanyika mpaka awamu hii ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli umeamua kufufua na kuliendeleza wazo hili. Mradi wa Stiegler’s Gorge kupitia Mto Rufiji utafanikiwa kuzalisha Megawattz 2100 utakapo kamilika. Ukamilifu wa mradi huu utajenga uhakika wa umeme nchini, utashusha bei ya umeme nchini na pia utamjengea Rais Magufuli heshima kubwa isiyofutika.

*(v) Mapambano dhidi ya Rushwa na ufisadi nchini.*

Rais Magufuli ameingia kwenye historia ya kiongozi ambaye Serikali anayoiongoza kuwa na mapambano ya dhahiri ya rushwa na ufisadi nchini. Tumeshuhudia Mafisadi Papa ambao walikuwa hawashikiki wala kukamatika wakipandishwa Mahakamani. Katika miaka ya nyuma ilikuwa suala gumu sana kwa Watuhumiwa “Mapapa” kuguswa tu, achilia mbali kupandishwa Mahakamani. Haya ni mapambano ya wazi wazi ya Serikali ya Rais Magufuli ya vita dhidi ya rushwa na ufisadi nchini. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na 2017 na pia ikishika nafasi ya pili (2) kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

*(vi) Uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za nchi*

Tumeshuhudia Serikali ikiweka uwazi kwenye mikataba na uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya yenye tija Mathalani tumeona uwazi wa sekta ya madini ya dhahabu, almas na Tanzanite ambapo Taifa tumeona namna ambavyo tulivyokuwa tukiibiwa na Serikali kuweka mikakati mipya ya kutokuibiwa tena. Kama haitoshi tumeshuhudia wawekezaji wakibanwa vilivyo juu ya mikataba isiyokuwa na tija kwa Taifa. Ni Serikali ya Rais Magufuli iliweka uthubutu wa kuwabana wawekezaji wa madini wa ACACIA iliyozaa matunda kwa Serikali ya Tanzania kumiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini, Serikali kupata gawio la faida ya madini ya asilimia 50 kwa 50. Yote haya yamewezekana kwa sababu ya uzalendo wake Rais Dk. Magufuli

*(vii) Ujenzi wa Bomba la Mafuta*

Serikali ya Rais Magufuli imefanikisha vilivyo kushirikiana na nchi ya Uganda kujenga Bomba la Mafuta linalotoka nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania. Ujenzi huo wa bomba la mafuta utazalisha ajira nchini na utaongeza pato la Taifa. Hayo yote yamefanikiwa kutokana na Serikali ya Rais Magufuli kuzidi kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo.

*Itaendelea …..*
*Shilatu E.J*
Hapo vi kuna uwalakini mkubwa, lkn pia uwepo wa kundi la wasio julikana linalo uwa, teka, poteza, piga risasi wale wote anao tofautiana nao kimtazamo, nayo itakuwa sehemu ya historia yake!!
 
Nafasi za uteuzi hazijai mkuu. Ongeza juhudi.
 
Rais Magufuli anaendekea kujijengea profile kubwa nchini
 
MImi siyo mtaalam wa uchumi lakini ni wazi mambo yaliyofanywa na Rais Magufuli kuhusu uwekezaji kwenye uchumi ni jambo zuri na la heri pamoja na changamoto kadhaa zilizojitokeza katika kipindi hiki cha mpito. Ninajenga hoja bila ushabiki wa kisiasa kuwa duniani kote hakuna taifa lililoendelea bila kuwa na mambo yafuatayo:
1.Sayansi,teknolojia na elimu
2.Uendezaji kilimo na viwanda
3.Miundo mbinu ya barabara,viwanja vya ndege na anga, majini na bandari na mawasiliano.
4. Umeme na Maji
Haya ndiyo maeneo yanayojenga misingi endevu ya uchumi. Umuhimu wa maeneo haya ni kuwa yanawezesha watu kuendelea na maisha yao kwa ustawi .Katika mukhtadha huu, watu hupewa elimu na afya ili waweze kupambana na mazingira yao. Sina shaka uwekezaji unaofanyika hapa nchini una malengo ya muda mrefu na unachukua fedha na raslimali watu kwa uwingi na hivyo kuathiri baadhi ya maeneo kwa muda mfupi(in a short run) k.m upandishaji mishahara na ugumu wa maisha. Hili halikwepi katika kipindi cha mpito. Lakini faida zake tutakuja kuziona miaka ijayo. Sambamba na miundo mbinu tumeona pia maeneo mengine muhimu yanaendelea kufanyiwa kazi yakwemo ya ustawi wa jamii mf ujenzi wa mashule na sekta ya afya. Wanasiasa wasitumie uelewa mdogo wa kiuchumi wa wananchi kupotosha ili kujipatia kura kwa kupotosha kuhusu kanuni za uchumi. Taifa hili limepitia kipindi kigumu sana tangu tupate uhuru kwa uwepo wa changamoto za umasikini, ujinga na maradhi.Dawa ya hisi changamoto ni kuweka uwekezaji sahihi na wa muda mrefu(Long Term Public Investment) ili kuweza kukabili changamoto hizo.Mwalimu Nyerere,Mkapa na Mwinyi nao walijitahidi kuwekeza lakini bado hatukufikia malengo kwa vile huu ni mchakato. Yeyote atakayepewa uongozi wa nchi hii kwa uchumi wa sasa wa dunia haya mambo hayakwepeki. Tena mimi ninakubaliana na Rais tumechelewa sana. Na maendeleo haya ni lazima yaendane na uboershaji wa maadili katika utumishi wa umma na usimamizi wa fedha na raslimali za nchi. Ameweza,Tumpe miaka 5 DK Magufuli atufikishe mahali.
 
Binafsi nataka aseme mwenyewe kwamba miradi hii inatokana fedha zenu wanyonge, mnapoona inajengwa tambueni;

1. Wafanyakazi nyongeza zenu halali na makato ya pension yanaenda huko

2 wafanyabiashara kodi kubwa mnazotozwa zinaenda huko

3.wakulima tozo zenu muuzapo mazao zinaenda huko

Ili mtu ujue haki zako huzipati kwa sababu zinaenda huko.

Badala yake unasikia ni fedha za ndani.

Hizi fedha za ndani ni zipi hizi? Ambazo zinaubaguzi?

Tunashuhudia viongozi wa ccm wao wanashiba vizuri na magari ya kifahari, kweli ni haki yao tu wengine tukipata shida?

Kama hawajaweka wazi, binafsi siwezi kuuza utu wangu kwa manyanyaso na kuvunja haki za wanaostahili

Bado anasema siwezi peleka maendeleo hapa kwa sababu kuna wapinzani wakati michango yao anachukua bila kuangalia vyama vyao.

Na wapinzani ndio huenda ukifanya utafiti ndio wanaotoa michango mikubwa zaidi na zile za kubambikiwa.

Huyu anafikiria kweli?
 
MImi siyo mtaalam wa uchumi lakini ni wazi mambo yaliyofanywa na Rais Magufuli kuhusu uwekezaji kwenye uchumi ni jambo zuri na la heri pamoja na changamoto kadhaa zilizojitokeza katika kipindi hiki cha mpito. Ninajenga hoja bila ushabiki wa kisiasa kuwa duniani kote hakuna taifa lililoendelea bila kuwa na mambo yafuatayo:
1.Sayansi,teknolojia na elimu
2.Uendezaji kilimo na viwanda
3.Miundo mbinu ya barabara,viwanja vya ndege na anga, majini na bandari na mawasiliano.
4. Umeme na Maji
Haya ndiyo maeneo yanayojenga misingi endevu ya uchumi. Umuhimu wa maeneo haya ni kuwa yanawezesha watu kuendelea na maisha yao kwa ustawi .Katika mukhtadha huu, watu hupewa elimu na afya ili waweze kupambana na mazingira yao. Sina shaka uwekezaji unaofanyika hapa nchini una malengo ya muda mrefu na unachukua fedha na raslimali watu kwa uwingi na hivyo kuathiri baadhi ya maeneo kwa muda mfupi(in a short run) k.m upandishaji mishahara na ugumu wa maisha. Hili halikwepi katika kipindi cha mpito. Lakini faida zake tutakuja kuziona miaka ijayo. Sambamba na miundo mbinu tumeona pia maeneo mengine muhimu yanaendelea kufanyiwa kazi yakwemo ya ustawi wa jamii mf ujenzi wa mashule na sekta ya afya. Wanasiasa wasitumie uelewa mdogo wa kiuchumi wa wananchi kupotosha ili kujipatia kura kwa kupotosha kuhusu kanuni za uchumi. Taifa hili limepitia kipindi kigumu sana tangu tupate uhuru kwa uwepo wa changamoto za umasikini, ujinga na maradhi.Dawa ya hisi changamoto ni kuweka uwekezaji sahihi na wa muda mrefu(Long Term Public Investment) ili kuweza kukabili changamoto hizo.Mwalimu Nyerere,Mkapa na Mwinyi nao walijitahidi kuwekeza lakini bado hatukufikia malengo kwa vile huu ni mchakato. Yeyote atakayepewa uongozi wa nchi hii kwa uchumi wa sasa wa dunia haya mambo hayakwepeki. Tena mimi ninakubaliana na Rais tumechelewa sana. Na maendeleo haya ni lazima yaendane na uboershaji wa maadili katika utumishi wa umma na usimamizi wa fedha na raslimali za nchi. Ameweza,Tumpe miaka 5 DK Magufuli atufikishe mahali.
Haya kikwete mlisema tumpe kumi . Watanzania wamebadilika Sana. uRais Sasa ni ajira Sio msaada.
 
Eeeh! Unajifanya mwana uchumi kumbe mchumia tumbo, Umaarufu wa Magufuli ilitokana na wizara ya miundombinu aliuokuwa akiisimamia enzi za Jakaya, kumbe enzi za Jakaya miundombinu ilifanyika kwa kiwango Cha juu hata magu akashawishika kuanzisha kampuni ya ujenzi ya Mayanga ili ichukur baadhi ya tenda za serikali. Lakini Huyu JK aliweza kuongeza mzunguko wa fedha, aliajiri kila sekta, miradi ya maji, umeme, n. K vilikuwa vinaenda Kama kawa, Sasa Magufuli amekuja amebana upande huu wa watu anajari lami na vitu vya kijinva huku watu wanasumbuka. Ndio maana akija Lissu, miradi hiyo itaendelea na maendeleo ya watu yatakuwepo yaani kutakuwa na uwiano sawa Kati ya macro na micro economic
 
Uo utawala wa sheria ndi ule wakuunda matume ya uchunguzi..!!!! Tunacheleweshana banah si tunataka mtu ambae akikuta tatizo amalize papohapo..!! Kama anatoka na kichwa cha mtu atokenacho... sio mara unda tume alafu report inakuja kutoka baada ya miez sita bado hachukuliwi hatua.
 
Wekend njema wapendwa!
Kulingana na hali ya simanzi tunayopitia watanzania kuondokewa na Kiongozi wetu, na mimi nimeona japo niandike kidogo nimeupokeaje huu wakati mgumu, ambao kila mtu anajiuliza ni kwa nn umetokea ikiwa ni mara ya kwanza kabsa tangu kuzaliwa kwa Tanganyanyika na baadae Tanzania
Ni kwa nn Mungu karuhusu wakati huu utokee? hakuna mwenye majibu Wenye akili timamu tunasema kazi yake haina makosa!

Mpendwa mheshimiwa hakika umeacha simanzi kwa watanzania wote walopenda kuona mabadiliko katika nchi yetu kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.Kiu yako ya maendeleo hailezeki, kujiamin kama sifa kubwa sana ya kiongozi kwako ilikuwa kubwa mno!,

Mh, siewzi heleza sifa zako zote lakini kwa kiasi kukibwa maisha ya watanzania wa chini uligusa kwa hili ata shetani hana ubishi
binafsi baada ya kumaliza elimu yang ya juu na kukosa hajira niliingia mtaani kufanya biashara ndogo ndogo, hali likuwa shwar, akuna aliyebugudhiwa,ofisi yangu ndogo ya matunda niliweka mbele ya ofisi kubwa ya Takukuru tena kwa kujiamni kwamba hakuna atayenifanya chochote, kwa hili kwakweli ulifanikiwa..

sifa zako ni nyingi mno, vyanzo vya maendeleo kama umeme,miondombinu kweli ulijitaidi acha sifa zako nikupe kabla hujazikwa

Usawa kwa watu, matajaili kuwaheshimu masikini, ukiwa umesoma katika utawala magufuli hakuna mtu ambae angeweza kukuonea kizembe,wanaoonewa ni wale ambao hawajui chochote kifupi ni wale ambao wakimuona askari wanatetemeka ata kama hawana makosa,ni wale watu wenye uelewa mdogo sana, niliwahi kumtetemesha inspector wa kitengo cha madawa mkoa mzima aliponiletea upuuzi akifkr na mm ni layman alitetemeka,simu za kinibembeleza zilikuwa aziishi, alichanganyikiwa sana nilipokuwa nikimwambia hii ni Serikali ya Magufuri nakutia jela kwangu umepotea njia uhuni wafanyie wasiojielewa, wakati huo kesi iko kwa R P C, na yeye akimueleza kijana katia ngumu anataka akupeleke mahakani, Askar huyo wa polisi alinilia, machozi yakadondoka akiomba msamaha, nilpotaka alie kidogo namtaja Magufuri, akisikia tu jina anajua hapa sina ugali, Hata R P C, nilikuwa simbembelezi na alikuwa mpole alipogundua kuna potential ndani yang,

kusema ukweli ukiwa unajielewa na unajua kidogo sheria, enzi za utawala wake ulitembea kifua mbele..

KWA HAYA BABA TAIFA LITAKUMBUKA

Mheshimiwa pamoja na hayo yote,lakini ulijenga chuki,ulikiuka utawala wa sheria na katiba
hili tuliona wazi watu wakitekwa hadharani, wakiuawa, lakini pia ulichukua mambo yoote wewe mwenyewe

Mh rais taifa pia litakukumbuka, kwa kuonea wapinzani wako kwa kiwango kikubwa sana, na hili ulilidhihilisha kwa vitendo kwenye chaguzi za serikali za mitaa 2019, serikali yako iliamua kufuta wagombea wa upinzani wote kwa hila, jeuri na kiburi kisa ulikuwa raisi, hapa ulikuwa unaongozwa na shetani
hukukoma,elf 2020, ukatoa wapinzani woote kwa kutumia dola kwa yyte mwenye akili timamu bila ushabiki hakuhitaji kuambiwa kupora haki ya mtu ni kumkosea Mungu kiwango cha juu kuliko mazuri yoote uliyofanya, na niukatili wa hali ya juu
utakumbukwa pia kwa kuua democrasia,
hukuvumilia kabisa kukosolewa kisiasa, kwa aliyejaribu alikamatwa na kama sio kuuwawa hili tumeliona hukujali kabsa kwamba blood is every human inheritence and should be serespected with all sensibilities.. hukuheshimu damu ya binadam ww, Hapa pia Ulimkosea Mungu Kwa Kiwango cha juu sana, serikali yako ilitengeneza kikundi cha watu na kukipa jian la wasiojulikana,kazi yake utamueleza Mungu

Katiba ambayo ndo baba mwenye ndevu wa taifa kwako ilikuwa ni uchafu,ulifanya chochote unachotaka wakati wowte bila kupingwa hapa mm nakuombea msamaha kwa Mungu
sheria za nchi kwako hazikuwa na madhara yoyote, haki za binadamu kwako haikuwa chochote wala lolote, hadi unafariki hakuna mtu yyte aliyepata nafas ya kukuombea angalau mungu asikie kilio cha watanzania pengine angekuponya, haya ni matunda yako lakni

Mwisho m napingana kidogo na taarifa iliyototelewa na kituo cha habar cha mataifa DW, kwamba ulipendwa kwa kiwango hicho hicho ulichochukiwa, m nafkr kwa ukatil wako walokuchukia walikuwa ni weng kuliko waliokupenda..
No offence rais wetu alifanya kazi nzuri sana. lakin si kusifia kinafki mpaka kupitiliza.
hivi kwani lazima uanzishe id mpya kila saa mkitaka kuandika makala kama hizi?
 
1616339128669.png
 
Umetisha sana na uzi huu uwe maalum kwa MATAGA wote wa lumumba.
 
Back
Top Bottom