Rais Magufuli: Ndege nyingine 3 kuwasili mwakani. Wahudumu wa ATCL wana ‘shape’ nzuri

Ni swala zuri.
Magu namkubali kuwakataa wachina na kujenga ATCL mengine sikubaliani naye

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sipingi ununuzi wa ndege ndogo kama hizi Bombadier
Hizi zinafaa kwa short distances regional routes na zinafaa kwa soko la domestic ndio mahala pake

Lakini soko la long haul ni hasara tu kwa sababu ni Crowded na mashirika makubwa ambayo hatuwezi kushindana nayo tuyaache yawe yanatuletea watalii Dar na Kilimanjaro halafu Bombardier zinawachukaua na kuwapeleka kwenye mbuga zetu za wanyama

Hiyo ndio Win win.
 
Marekani watakuja kuomba msaada kwa Tanzania
Hii ya kusafirisha fresh agricultural produce kama mbogamboga mm naunga mkono. Rais anastahili pongezi hapa. Kwa sasa shipping line mbogamboga zetu ni kupitia Jomokenyata na KQ zao. Wakulima Tanzania wamekuwa wakiuza mbogamboga zao kwa madalali wa Kenya kwa sababu ya kutokuwa na usafiri wa uhakika nchini.
Lakini kuingia kwenye soko la dunia hasa EU kwa mbogamboga zetu kuna safari ndefu kidogo kwa sababu kwa sasa kama nchi hatuna mpango mahususi wa kanuni ya kilimo kinachokubalika kimataifa (Good Agricultural Practices; GAP). Kama nchi tuanze agricultural schemes zinazofuata GlobalGAP ili tuwe na uhakika wa masoko duniani.
 
Watumishi wa umma nao wapewe ofa ya kupanda ndege kama wale wajumbe wa chama, maana kwa vile vimishahara wataishia tu kushuhudia ndege zinapokelewa pale airport, walimu mpoooo..
 
Kwenye issue ya GAP ndio umekosea kabisa, sisi tuko vizuri lakini hatujui hio siri. Sasa hivi dunia nzima inataka Organic food na sisi ndio practices zetu toka enzi hizo.

Cha muhimu ni namna gani ya ku-scale up production ya organic food, na uzuri ni kuwa bei ni kubwa zaidi ya hizo GMOs zilizojaa kwenye supermarkets
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nafurahia sana ukuzaji wa UCHUMI wa nchi yetu, jitahada zote za dhati ukizingatia changamoto zilizopo. LAKINI hakuna biashara yoyote duniani inayoongizwa HOVYO HOVYO ikaenda popote. Hakuna!

ATC mnajitahidi kidogo ila ACHANENI na kwenda KISIASA.

Haiwezipandi akilini mnachota manauli ya WATEJA, na hapa ni pamoja na wasio Watanzania kwenye route za ndani na nje halafu mnafaya mambo ya kidaladala za Mbagala. Mnatia aibu!
1. Kwenye route ya DAR- HARARE- LUSAKA- DAR yenye abiria kibao mnatesa wateja. Flight zinaairishwa bila hata taarifa .... mfano ya juzi Ijumaa(13/07) for 14 hours! Mbaya zaidi CUSTOMER care Mamantilie style ni aibu tupu licha ya maumivu yatokanayo. Alafu Jumamosi ilee Airbus mlipeleka kulee kwa kina geteegete .... abiria mkawapa ilepangaboi iliyopakwa rangi na wataalamu wa KIPAWA kwenye international route. Mkawanyima na lunch mchana wote. Hivi nyie mnafanya biashara au mnajaribu KUIGIZA? Igizeni vizuri basi! Hata wateja wa Mbagala mkiwafanyia hivi watawakimbia. Narudia hizi ndege za nini kwa uendeshaji wa aina hizi?
 
such a mindful message
 
Wahudumu wa ATCL wapuuzeni wanaosema ninyi wabaya, ninyi ni wazuri, na ‘shape’ zenu ni nzuri, roho zenu ni nzuri na sauti zenu ni nzuri. Chapeni kazi.”


😂😂
"Hebu wewe uliyesababisha mimi nisiendelee na upadri toka humo kwenye gari shuka usalimie watu" Alisikika akisema
 
Ninadhani tulipaswa kununua ndege za mizigo zaidi kulikonza abiria. Siku si nyingi air travel itakuwa saturated na ndege zetu wenyewe na kukosa abiria wa kuzipatia faida. Disposable income ni ndogo kwa sababu ya ukosefu wa uzalishaji na ajira - watu wachache wataweza kutumia ndege na hasa reli ikianza kufanya kazi. Ndege za mizigo zingechochea kilimo cha maua na mboga na bidhaa za nyama.

Kuna sehemu tunakosea na tutakuja kujua tumeshachelewa.
 
Mambo yanavyoendeshwa katika awamu hii ya tano yaani hovyo kabisa, hapa Songwe sasa kila mwananchi michango yote ukiunganisha kila mmoja analazimishwa atoe Kiasi cha tsh 45000.00 halafu likiwa jukwaani linasema wananchi msitoe michango mimi rafiki wa wanyonge, bullshit kumbe linaongea kinyume.
 
Kwa hakika Tanzania ya madege yasiyokuwa na uhakika wa biashara yenye tija inawezekana. Tumebadili gia angani kama vile alivyofanya DJ, kwa hiyo tumebadili hata kauli mbiu yetu yenye kuhusu viwanda. Siku zote tunahitaji kuwa makini sana na kauli wanazozitoa wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani unaona hatari gani kuchangia hiyo 15000
 
Naam Tanzania inaanza kuheshimika tena kimataifa
Sana bro ! I tell you come 2025 watanzania tutakua anga zingine kabisa ! The best place ever. Tulicheleweshwa mno ! JPM ipaishe nchi yetu, tunakuombea kwa Mungu sana. Najua ntapopolewa mawe humu Divided Republic of JF country lakini habari ndio hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…