Securelens
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 316
- 541
Moja ya kazi nzuri aliyofanya Mheshimiwa Rais Magufuli ni kupiga vita ufisadi na rushwa kwa vitendo. Mashauri makubwa ya ufisadi 407 yamepelekwa mahakama ya mafisadi na mashauri 385 yamesikilizwa.
Aidha kupitia Takukuru mashauri 2,256 yalifunguliwa ambapo mashauri 1,926 tayari yametolewa uamuzi na serikali imeshinda mashauri 1,013. Tayari Serikali imeokoa bilioni 273.38 zikiwemo fedha walizo dhulumiwa wakulima sehemu mbalimbali. Takukuru imetaifisha fedha taslim shilingi milioni 899, $1,191,651, €4,301,399, nyumba 8 za thamani ya bilioni 11.6, magari , viwanja na mali zingine.
Aidha serikali imerejesha mali za serikali zilizochukuliwa isivyo halali na watu binafsi zikiwemo nyumba na majengo 98 ikiwemo Mbeya Hotel, viiwanja 298, kampuni 3 na maghala 69. Pia zuio limewekwa kusubiria kukamilika kwa taratibu za kisheria za utaifishaji wa mali mbalimbali zikiwemo fedha kiasi cha shilingi bilioni 52.7, $ milioni 55.5, € miloni 4.3, magari 75, nyumba 41, viwanja 47 na Mashamba 13.
Kwa kweli hakuna kama Rais Magufuli. Watanzania wote tunaochukia ufisadi na rushwa tunakwenda na Rais Magufuli hadi 2025 kwa kumpa kura nyingi. Amethubutu na Ameweza (Source za Takwimu zote ni Hotuba ya Mheshimiwa Rais Magufuli alipokuwa akivunja Bunge tarehe 16 Juni 2020).
Mafisadi na wala rushwa kadhaa walioumia wakati wa utawala huu wanahangaika huku na kule laying wameshindwa. Watanzania tumeamua tunakwenda na jemedari huyu wa vita ya ufisadi na rushwa. Oktoba 28 tunampa kura za mafuriko Rais Magufuli. Jiunge na kundi la watanzania la ushindi kwa JPM.