KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Bila shaka na "watakao shauri" na watakao'criticise', nao kwako watakuwa sawa, au sio?Sijaandika ili nipewe like au watu wakoment, nimeandika watu wasome, watakaopenda wapende, watakaochukia wachukie, watakaojifunnza wajifunze, watakaopuuzia wapuuzie.
Naona kama 'ngozi' yako kidogo ni nyembamba kutokana na majibu unayowapa wanaodhani andiko lako haliko kamilifu. Najua, kwa umri wa miaka 26, pengine jambo hili sio la ajabu sana. Lakini ukitaka kukomaa katika fani hiyo ya uandishi, bila shaka hata hao wanao'critic' maoni yao utayapima kwa kina na sio kuwashambulia kama unavyofanya kwa kuamini kwamba "...kila mtu unam'treat' jinsi anavyokuja." na kwamba "hiyo ndio haki"?
Nitakubaliana na dhana hii kama mhusika katukana, au kaandika upuuzi usioendana na mada yenyewe. Lakini kama ni kupishana misimamo tu, utakuwa unapoteza fursa ya kujifunza toka kwa wengine.
Nimeona nikupe tu ushauri huu kama unataka kuwa mwandishi mahiri.
Hamna Mkuu, kila mtu unamtreat jinsi anavyokuja hiyo ndio haki