Rais Magufuli, pamoja na Corona unayo nafasi ya kuiunganisha nchi

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Rais Magufuli kwa mara nyingine nakuletea ushauri ambao ni nadra kuupata toka kwa wanaojipendekeza kwako kwa maslahi yao.

Kwa bahati mbaya pana watu gonjwa hili la Corona wamelifanyia siasa kwa maslahi binafsi. Busara na hekima vimewekwa pembeni kujaribu kuifanya jamhuri ya Tanzania kuwa ni kama ya watu wa ramli ramli, waswalihina, walokole nk.

Ni muhimu kutambua nchi haina dini, wananchi wana dini zao na wengine hawana dini. Si sahihi kuwachukuwa watu wote katika hizi bandwagons za imani ambazo wakati mwingine zinakinzana na imani za wengine.

Katika hali ya kushangaza wanaohimiza kuwepo na total lockdown (japo kuanzia katika maeneo, miji au mikoa iliyothibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huu) wamekuwa branded ati kuwa ni wapinzani wa CCM. Kwa upande mwingine wale wanaopinga lockdown wamekuwa nao wakijitanabaisha zaidi kama wana CCM (ama wafuasi wako). Bora hata ingekuwa Simba na Yanga.

Ni ukweli kuwa haupo ukweli thabiti katika mgawanyiko huo. Si siri kuwa wapo wana CCM wenye uelewa ambao wanauona umuhimu wa lockdown.

Kwani:

1. Kimsingi wanaokubaliana kuwa lockdown itatusaidia kuudhibiti ugonjwa huu, ni wale wale waliokuwa wakihimiza kwa uhakika kabisa njia ya kuuzuia ugonjwana huu kuingia nchini kabla haujaingia.

2. Wanaokubaliana kuwa lockdown itatusaidia wana rejea za kutosha zinazo shehenisha hoja (kisomi na kisayansi) kuwa japo njia hii ni chungu, ndiyo ilikuwa ya kwenda.

3. Wanaopendekeza lockdown hawaonekani kuwa na maslahi binafsi kwani hawajaonesha wala haijaoneshwa ni vipi watanufaika wao zaidi ya kuwa kweli mnyororo wa maambukizi kweli utavunjwa.

4. Kuwa hali itazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyoenda.

5. Nk, nk.

Kwa upande mwingine wanaopinga lockdown:

1. Wamejikita zaidi katika imani za kidini wakipendekeza maombi zaidi na sala.

2. Wamekuwa wakijitanabaisha na kukuunga wewe mkono katika kila jambo (watakuunga mkono vilivyo hata ukiitisha total lockdown ya nchi nzima leo).

3. Bahati mbaya wengi wao ni mbumbumbu wa kutupwa wenye kuamini ati kuwa Corona ilikuwapo Tanzania na Afrika muda mrefu. Ati kuwa haiathiri watu weusi (waafrika).

4. Wanaamini kuwa kwa vile kuna wanaopona Corona basi tiba ya corona ipo.

5. Wanaamini kuwa Corona ni kama upepo tu, ugonjwa huu utatoweka wenyewe.

6. Nk. Nk.

Wanasema wajuzi:

"If you can't beat it you join it".

Tunayo nafasi ya kupambana na huu ugonjwa sote kwa umoja wetu tukaushinda. Lockdown ni ngumu bali ni muhimu na njia pekee iliyopo kwa sasa itakayotuokoa.

Wapinga lockdown wote kwa bahati nzuri, wote watakuunga mkono blindly kama walivyo siku zote. Hali wanaoona hii ndiyo njia pekee nao watakuunga mkono zaidi kwa kufikia maamuzi ambayo wanaamini ni sahihi zaidi.

Kwa kudeclare lockdown utakuwa u meungana na wazalendo wote. Kwa hakika hayupo mzalendo wa kweli anaweza kuwa na ujasiri wa kufikiria jambo jingine la maendeleo wakati ugonjwa huu ukiwa unatishia maisha yetu kwa kiasi hiki.

Si mpinzani wala CCM anayeweza kuota ndoto hata za uchaguzi mkuu kama ugonjwa huu haujadhibitiwa. Kwa hakika kuudhibiti ugonjwa huu ni suala la dharura mno kwa sasa.

Tutoke kwenye majidiliano ya lockdown au no lockdown tujikite katika kuona ni jinsi gani tutapita salama sote kabisa katika kipindi cha siku kama 21 za lockdown.

Mambo ya uchumi tuyaweke pembeni. Uhai wetu kwanza
 
Lockdown - angalia rate ya maambukizi inavyopungua. Sample ngapi zimepimwa na ngapi zimekuwa positive.

Covid-19: Good News for Kenyans as Number Jumps to 191

Wanayo haki ya kutembea vifua mbele.
Wakenya wengi ni wasafiri na wanawatalii kuliko sisi na kibaya zaidi maeneo mengi ni makavu hakuna hata maji ya kunywa sembuse maji ya kuosha mikono watayapata wapi! Wanyarwanda nao kama wakenya ni watu wa kusafiri sana. Tanga wamejifungia kiasi cha kulazimisha mabasi ya abiria kwenda mikoani kusimama! Chekelea kutofungiwa ila kufa utakufa peke yako, mwenzako akiugua madakitari wote wakuu na bifaa vyote vitszunguka kitanda chake.
 
Ni wazi kuwa wasioona umuhimu wa lockdown ni kushindwa kuelewa tu.

Kuna mambo mawili ambayo ni distinct:

1. Lockdown kama ufumbuzi wa kuuvunja mnyororo wa maambukizi ya corona.
2. Kula ya watu wakati wa lockdown kama athari.

Haya ni mambo mawili ni tofauti anayeyachanganya anafanya hivyo kwa ufinyu wa mawazo yake tu.

Haya mawili na validity yake ni yakujadiliwa separately.
 
Hizi hatua zikichukuliwa, haimaanishi watu watashindwa hata kwenda kununua chakula, tutakuwa na utaratibu unaoruhusu Hilo.

Kabla haujaingia Ugonjwa, waona mbali walishauri vema kabisa kwamba tufunge mipaka na kuwa, wanaoingia wawekwe quarantine, tukakaza.

Ukaingia na tayari tumepoteza roho za watu ambao pengine wangekuwa salama jitihada za makusudi zingechukuliwa mapema kabisa Kama ambavyo, waona mbali walishauri.

Nyoka Yuko ndani ya nyumba tayari na ameshaua. Watuwanapendekeza kuwa tukiwa wengi tuko salama, na hatujashuhudia vifo vingi zaidi, tugonge total lockdown. Kukata mnyololo wa ugonjwa huu kabla haujawa mrefu. Bado tunakaza.

Sasa tunasubiri watanzania wafe kwa wingi ili tuwe tumetoa kafara. Maana Hali inaonekana wazi kuwa Ni tete na Tata, hatua zinazoelekezwa Ni za kuzuia watu Fulani kutoa takwimu, hii inasaidia kukata mnyololo wa huu ugonjwa?

Sizonje, Tuombe Mungu aisee maana ni hatari, Lockdown haitakuwa tatizo kwakuwa watanzania wanahitaji, lifanyike. Mwitikio utakuwa mkubwa mno. Na ugonjwa utapita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haieleweki wanaopinga lockdown ni kwa nini wanadhani wanaoipendekeza kama ufumbuzi kuwa ni wana chadema.

Hivi huko South Africa, Rwanda nao ni chadema? Huko Spain, Italy nako je?

China nao?

Ninadhani kama chadema wanahusishwa moja kwa moja na jambo hili ambalo ni hakika kuwa litatuokoa, basi wanapashwa sasa kwa nguvu sana na dharura ya hali ya juu mno kujipambanua hivyo.

Kwa kuanzia wawe mfano kuhitaji shughuli zote zinazoleta mikusanyiko yoyote kusimamishwa. Hii ni pamoja na shughuli zote za bunge, masoko, usafiri wa umma nk.

Wakati ni sasa.
 
Hizi hatua zikichukuliwa, haimaanishi watu watashindwa hata kwenda kununua chakula, tutakuwa na utaratibu unaoruhusu Hilo.

Kabla haujaingia Ugonjwa, waona mbali walishauri vema kabisa kwamba tufunge mipaka na kuwa, wanaoingia wawekwe quarantine, tukakaza.

Ukaingia na tayari tumepoteza roho za watu ambao pengine wangekuwa salama jitihada za makusudi zingechukuliwa mapema kabisa Kama ambavyo, waona mbali walishauri.

Nyoka Yuko ndani ya nyumba tayari na ameshaua. Watuwanapendekeza kuwa tukiwa wengi tuko salama, na hatujashuhudia vifo vingi zaidi, tugonge total lockdown. Kukata mnyololo wa ugonjwa huu kabla haujawa mrefu. Bado tunakaza.

Sasa tunasubiri watanzania wafe kwa wingi ili tuwe tumetoa kafara. Maana Hali inaonekana wazi kuwa Ni tete na Tata, hatua zinazoelekezwa Ni za kuzuia watu Fulani kutoa takwimu, hii inasaidia kukata mnyololo wa huu ugonjwa?

Sizonje, Tuombe Mungu aisee maana ni hatari, Lockdown haitakuwa tatizo kwakuwa watanzania wanahitaji, lifanyike. Mwitikio utakuwa mkubwa mno. Na ugonjwa utapita.

Sent using Jamii Forums mobile app

Si mbaya kutambua tumekuwa taifa ambalo mambo yamegeuka kuwa kinyume. Imekuwa shaghala baghala. Imekuwa ndivyo sivyo. Kushoto kumekuwa kulia na ujinga umefanywa kuwa ndiyo werevu.

Hoja zako za dhati kabisa kama ilivyo kwa uzi huu:

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

haitakuwa ajabu ukiwasikia wanazihusianisha na u chadema.

Ninadhani ni wakati sasa wa kuchukua hatua. Hivi kwani hawa chadema nao wako wapi kusaidia kuisukuma mbele ajenda hii yenye maslahi sana kwenye nchi hii kwa sasa?
 
You are very right. Kama sizonje hataki, tuchukue hatua wenyewe at an individual level, za lockdown. Maana sizonje haonyeshi dalili.

Kikubwa Ile wanayoita social distancing itumike au igeuzwe kuwa lockdown. Tunao jitambua tujipe wenyewe lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You are very right. Kama sizonje hataki, tuchukue hatua wenyewe at an individual level, za lockdown. Maana sizonje haonyeshi dalili.

Kikubwa Ile wanayoita social distancing itumike au igeuzwe kuwa lockdown. Tunao jitambua tujipe wenyewe lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu lockdown ya mtu mmoja mmoja haisaidii. Huu ugonjwa ni airborne. Virus y Corona anaweza kusalia hewani masaa nane ukipita ukamvuta ana wewe.

Ni kwa njia hiyo kina Boris Johnson, Queen Elizabeth, Prince Charles na wengine huko ulaya na marekani huenda wanaambukizwa.

Corona ingekuwa ukimwi peke yako ungeweza kujikinga. Hili mbona hakuna aliye salama?
 
Rais Magufuli kwa mara nyingine nakuletea ushauri ambao ni nadra kuupata toka kwa wanaojipendekeza kwako kwa maslahi yao.

Kwa bahati mbaya pana watu gonjwa hili la Corona wamelifanyia siasa kwa maslahi binafsi. Busara ba hekima vimewekwa pembeni kujaribu kuifanya jamhuri ya Tanzania kuwa ni kama ya watu wa ramli ramli, waswalihina, walokole nk.

Ni muhimu kutambua nchi haina dini, wananchi wana dini zao na wengine hawana dini. Si sahihi kuwachukuwa watu wote katika hizi bandwagons za imani ambazo wakati mwingine zinakinzana na imani za wengine.

Katika hali ya kushangaza wanaohimiza kuwepo na total lockdown (japo kuanzia katika maeneo, miji au mikoa iliyothibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huu) wamekuwa branded ati kuwa ni wapinzani (wa CCM). Kwa upande mwingine wale wanaopinga lockdown wamekuwa nao wakijitanabaisha zaidi kama wana CCM (ama wafuasi wako). Bora hata ingekuwa Simba na Yanga.

Ni ukweli kuwa haupo ukweli thabiti katika mgawanyiko huo. Si siri kuwa wapo wana CCM wenye uelewa ambao wanauona umuhimu wa lockdown.

Kwani:

1. Kimsingi wanaokubaliana kuwa lockdown itatusaidia kuudhibiti ugonjwa huu, ni wale wale waliokuwa wakihimiza kwa uhakika kabisa njia ya kuuzuia ugonjwana huu kuingia nchini kabla haujaingia.

2. Wanaokubaliana kuwa lockdown itatusaidia wana rejea za kutosha zina shehenisha hoja (kisomi na kisayansi) kuwa japo njia hii ni chungu, ndiyo ilikuwa ya kwenda.

3. Wanaopendekeza lockdown hawaonekani kuwa na maslahi binafsi kwani hawajaonesha wala haijaoneshwa ni vipi watanufaika wao zaidi ya kuwa kweli mnyororo wa maambukizi kweli utavunjwa.

4. Kuwa hali itazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyoenda.

5. Nk, nk.

Kwa upande mwingine wanaopinga lockdown:

1. Wamejikita zaidi katika imani za kidini wakipendekeza maombi zaidi na sala.

2. Wamekuwa wakijitanabaisha na kukuunga wewe mkono katika kila jambo (watakuunga mkono vilivyo hata ukiitisha total lockdown ya nchi nzima leo).

3. Bahati mbaya wengi wao ni mbumbumbu wa kutupwa wenye kuamini ati kuwa Corona ilikuwapo Tanzania na Afrika muda mrefu. Ati kuwa haiathiri watu weusi (waafrika).

4. Wanaamini kuwa kwa vile kuna wanaopona Corona basi tiba ya corona ipo.

5. Wanaamini kuwa Corona ni kama upepo tu, ugonjwa huu utatoweka wenyewe.

6. Nk. Nk.

Wanasema wajuzi:

"If you can't beat it you join it".

Tunayo nafasi ya kupambana na huu ugonjwa sote kwa umoja wetu tukaushinda. Lockdown ni ngumu bali ni muhimu na njia pekee iliyopo kwa sasa itakayotuokoa.

Wapinga lockdown wote kwa bahati nzuri, wote watakuunga mkono blindly kama wanalivyi siku zote. Hali wanaoona hii ndiyo njia pekee nao watakuunga mkono zaidi kwa kufikia maamuzi ambayo wanaamini ni sahihi zaidi.

Kwa kudeclare lockdown utakuwa u meungana na wazalendo wote. Kwa hakika hayupo mzalendo wa kweli anaweza kuwa na ujasiri wa kufikiria jambo jingine la maendeleo wakati ugonjwa huu ukiwa unatishia maisha yetu kwa kiasi hiki.

Si mpinzani wala CCM anayeweza kuota ndoto hata za uchaguzi mkuu kama ugonjwa huu haujadhibitiwa. Kwa hakika kuudhibiti ugonjwa huu ni suala la dharura mno kwa sasa.

Tutoke kwenye majidiliano ya lockdown au no lockdown tujikite katika kuona ni jinsi gani tutapita salama sote kabisa katika kipindi cha siku jana 21 za lockdown.

Mambo ya uchumi tuyaweke pembeni. Uhai wetu kwanza
Amekimbia Vita huyo ameenda kujificha eti amechukua likizo hahahahhahahahahaha atarud tu atakutana na corona ikimsubiria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom