S.M.P2503
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 2,421
- 4,344
Tafadhali sana mheshimiwa sana, Raisi wetu, Dkt. Magufuli, yahusu huyu Tundu Lissu atakaporudi nyumbani Tanzania. Kama kweli alikuwa msaliti, ni Mungu tu ajuaye na ni Mungu tu aliye hakimu wa haki.
Mheshimiwa sana, wewe ni Mkatoliki na pia mseminari, waijua vema hadithi ya mwana mpotevu na kondoo aliyepotea.
Tundu Lissu ni Mtanzania kama wewe, baba, kaka na mtoto wa familia Tanzania yetu wewe. Hotuba yako (Uchaguzi House) ya leo 22/07/2020 nimependa na iwe ya kweli kwa vitendo.
Tafadhali, chondechonde, akirudi huyo (Tundu Lissu) Jumatatu, muacheni arudi kwa style yake, afanye anayotaka kufanya bila kuvunja sheria. Hakuna haja ya kutunishiana misuri kwa sasa, muacheni aje, kama figusu, mfanyieni baada ya uchaguzi na sio sasa. Tutachafuka na kuchafuana sote, nyumba yetu sote (Tanzania) itanuka, mpeni Tundu Lissu ushirikiano, msaidieni atulie na baada ya uchaguzi ndio kesi zake ziendelee au figisu zozote.
Mheshimiwa sana Rais Magufuli, kama umesoma, umesomea au kutaarifiwa. Ni hayo tu yangu. Nyumba Tanzania ni yetu sote. Bila matusi au mkwaruzo tuwe kama nguchiro na Mchwa, nyumba moja bila mkwaruzano.
Ni hayo tu kwa leo. Ubarikiwe na Uongozwe kwa niaba aliye juu na amri ya uhai wako kwake.