chamaclotus
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,079
- 2,273
Kwa kitendo ulichofanya cha kutaka kuihujumu timu yetu ya simba tunasema hatuna imani na wewe tena kwenye mpira wa miguu. Hii timu ya simba sio timu ya serikali bali ina wanachama wake ambao wanafanya maamuzi juu ya klabu. Na sisi ndio wanachama ambao tumeamua kumpa timu Mo Dewji na ametusaidia kufika robo fainali africa mpaka kusaidia Tanzania kuingiza timu nne mashindano ya africa lakini hilo hulioni. Tunakuomba ujiuzulu mapema kabla hatujafanya maandamano ya kukupinga hadharani.
Nawasilisha.
Tunakoelekea Tanzania itafungiwa kwasababu ya Waziri wake kuja na
sheria zake ambazo si rafiki kwenye
soka...Serkali ya Tanzania kuingilia Soka la Tanzania ni kosa sana...
Tunafungiwa si muda mrefu
Amewashwa na nini huyu waziri mpaka kuanza kutoa maoni kabla ya mjadala kufunguliwa afterall kama upo?Hajasema ni sheria ametoa maoni na mawazo yake kama mtu mwingine wa kawaida mpaka wakae na wahuska yaani wadau wa michezo waamue na kupanga sio kwamba inaanza kutumika kesho acha kukurupuka. Zingine wadau wanaweza kuzikataa hata mimi hii ya idadi wachezaji wa kigeni kupunguzwa siiungi mkono kabisa au kuchezesha mechi 1 wageni wachache siitaki wawekwe wengi tu ili wachezaji wetu wa kitanzania wapate changamoto wakaze buti
Limeniboa hili jitu...Hili tuungane wote bila kujali club. Ushenzi mtupu
Huyu mwakyembe ubachela umemlemea...Tunakoelekea Tanzania itafungiwa kwasababu ya Waziri wake kuja na