Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Asante mkuu Makoye Matale kwa kutujulisha kile kilichotamkwa.
 
Makoye Matale
Rais kafika BK kujiinea mwenyewe wapiga kura wake wanavyo teseka na wengine kufiwa zaidi ya kaya 15?

Kumtetea kwako hakuna maana yyt

..hivi kulikuwa na ulazima wa kumpiga picha Raisi akipokea MABULUNGUTU YA PESA zilizotolewa na Raisi Museveni? I think it is unprofessional and inappropriate.
 
..hivi kulikuwa na ulazima wa kumpiga picha Raisi akipokea MABULUNGUTU YA PESA zilizotolewa na Raisi Museveni? I think it is unprofessional and inappropriate.
Aibu sana Mkuu hasa ukizingatia kuwa serikali yake Magufuli haijachangia hata senti!
 
Aibu sana Mkuu hasa ukizingatia kuwa serikali yake Magufuli haijachangia hata senti!

..yaani wanaonekana hawana MBINU wala MIPANGO ya jinsi ya kupambana na majanga.

..huu siyo wakati wa wakubwa serikalini kuonekana na masuti huku wamekaa kwenye VIYOYOZI wakati waathirika wanalala nje.
 
Ee Mungu Baba wa viumbe vyote, zipumzishe pema roho za ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kutokana na tetemeko la ardhi Bukoba, wajalie kina mama, wazee, watoto, wababa na wahanga wote walionusurika wapate afya njema na uwajalie wapate riziki yao uliyowapangia, pia wasamehe wote wenye roho za kishetani wanaowatukana wahanga wote, Mungu wewe tu ndiye tunayekuabudu na ni wewe tu ndiye tunayekutegemea.
AMINA.

Maafa, shida, misiba, raha na starehe ni za wote, watu wote tuwe na huruma maana kila mmoja lazima apitie umauti kwa muda alopangiwa na Mungu Mkuu mwenye Enzi.
 
Kuna msemo unaosema "Ni afadhali ukae kimya watu waendelee kukutilia mashaka KULIKO kuongea na kuondoa mashaka yote yaliyokuwepo" Msemo huo leo umetimia Tanzania.
 
Walibugi kukubali kuwa kupatwa kwa jua kumeletwa na serikali.
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
 
Hizo hela zilizo changishwa kama hazijaenda kwenye kujazia bajeti ya mwakani sijui
 
kwa MAWAZO yangu kidogo niliyokuwa nayo; hizo michango ya watanzania na wengine ambayo imekadiriwa kuwa 2.3 billions inatosha kabisa kuwarudisha katika hali ya kawaida hawa waathirika; maana kuna wengine wametoa vifaa,wengine hela, wengine vifaa vya ujenzi;

sioni haja ya mkuu wa kaya kunyoosha mdomo kati michango imetolewa ya kutosha tu;
isitoshe cjaona mkono wa serikali hapo,
 
Rais yuko sahihi kabisa, nawashangaa mnaoshangaa. Mimi mtu mzima, mwenye akili timamu, mkulima au mfanyakazi nishinde kwenye hema kusubiri hela za serikali naumwa au nimepata ulemavu? Kwanini nisianze na kufyatua tofali ili mabati aliyotoa uhuru serikali ndo inisaidie. Kwa hiyo nikiendelea kushinda kwenye hema lile shamba serikali itanilimia? Acheni siasa, ukweli usemwe.
 
Wakati mwingine maneno ya busara huhitajika sana.. Hasa mtu anapo pata dharura kama huko bukoba. Vijembe wakati kuna watu wamepoteza mali zao..
Acha fikira za kizamani, tunza pesa zako zikusaidie nyakati za shida, watu mmeambiwa jiunge na bima za majanga mnabaki kukenua meno tu ooh ukawa, ukuta, ufedhuli !
 
sijui hayo maneno kama yana wajenga kisaikolojia waathirika wa tetemeko la ardhi au yanawaathiri!!?binafsi nawaombea kwa Mungu awajaze ujasiri yana mwisho hakuna awaye yote kwetu wanadamu zaidi ni Mungu,poleni sana wana kagera
 
Waziri mkuu endelea na moyo wako wa huruma mungu akujalie maisha marefu

Umeona eeh wakati Mkulu anazidi kuwa beza waathirika wa tetemeko la Ardhi.Kassim Maajaliwa alikuwa anaomba ardhi ipasuke ajifiche.Maana ule sio ukweli NI masimango
Halafu wadau wengi wamechangia sio pesa ngumu ya kodi zetu.
 
na aliowaita mashetani ...Badala ya kuipeleka haraka kupunguza majonzi anatoa kauli chafu.

Right, Rais ana kauli chafu. Kawaita watu shetani, wanafunzi vilaza, akiwa Unguja kasema tuwatumbukize watu kwenye visima vya maji, tutoboe matairi ya magari ya watu, kawananga wahanga wa tetemeko kwamba wamedhani tetemeko linaletwa na serikali as if ni wapumbavu kupita kiasi.... kila hotuba ya Magufuli imejaa lugha za ngebe.

Sitokei Kagera lakini nadhani tunakubaliana kwamba Kagera ni kati ya maeneo ya watu waliotangulia sana kwenda shule nchi hii, nani Kagera amelalamika kwamba Serikali imeleta tetemeko?

Magufuli angekuwa mchangiaji wa JF angefutiwa post zake nyingi na kufungiwa, amejawa na uchochezi, dhihaka, fighting words na matusi, hajui ustaarabu, hakosolewi, haheshimu Raia. Rais gani duniani anaongelea jukwaani style anazofanya mapenzi na mkewe?

Hatuheshimu na hajiheshimu, anategemea majeshi kumlindia heshima yake. We never probed his temperamental fitness to be head of state, now he has plunged the country into quasi dictatorship.
 
If you want to test a man's character, give him power- Abraham Lincoln
 
Beside tuna mahaba kwake 99% TWAWEZA wamepunguza kura za mahaba kwake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…