Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Huyu mkulu kitu anachotakiwa kujua ni kwamba wananchi sio wajinga wanajua tetemeko ni nini. Pili hakuna mwananchi amekaa hapo akisuburi serikali imsaidie, watu wanasaidiana pale wanapoweza. Mkulu inabidi aelewe kazi ya kiongozi wakati wa majanga ni kuwapa watu hope na kuweka siasa pembeni.
 
Endelea kufanya kampeni.

Kampeni gani? Msaada wa PESA Na vifaa vya ujenzi vimechangwa Na wadau wengi.Kazi ya hiyo michango NI kuwasaidia Waathiriwa.
Halafu msema kweli sio Mkulu peke yake.Ukisema ukweli basi umekuwa mpinzani
Ukweli lazima usemwe.
 
Ila watu WA Bukoba wanajibebisha sana kwenye hili suala la tetemeko.

Pale Mwakata Kahama kwenye mvua ya Mawe zaidi ya watu 36 walikufa na zaidi ya 200 waliachwa bila makazi mwaka jana na mpaka leo hakuna aliyejengewa hata choo na mwezi jana kapita hapo na kuwaambia akiwa Isaka kuwa serikali yake haitamjengea mtu hivyo waanze kujijengea.
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Kuna watu wanalaumu serikal haikutoa taarifa mapema kama utabiri kma vile inavyofanyika kwa mvua,
 
Mtu yuko nje..familia na watoto...amepoteza vitu vyake...hajapata hata hema bado afanye kazi..
Kwahyo akae tu? Huku kutafuta hema pia sio kazi? Hv kila mkoa ukipata tetemeko nyumba zikabomoka serikali itajenga? Nyumba za kahama mvua ya mawe, ss hv tetemeko, ije mvua, serikal ina uwezo huo?
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Hujui maana ya neno mshari?
 
Nimemsikia akisema waathirika wa tetemeko la ardhi wafanye kazi wasikae tu kusubiria Serikali iwasaidie, tetemeko halijaletwa na Serikali
Magufuli ni mkweli, au mnataka awe kama kikwete nyumba za kahama mpk leo kimya?
 
Wataanzania tumekiingia cha kike, watu wanahitaji maneno ya faraja wanaenda kuambiwa hivyo kweli!
Mmezoea kudanganywa hampendi kuambiwa ukweli, mnataka aseme atawajengea wote nyumba zilizobomoka?
 
kwa MAWAZO yangu kidogo niliyokuwa nayo; hizo michango ya watanzania na wengine ambayo imekadiriwa kuwa 2.3 billions inatosha kabisa kuwarudisha katika hali ya kawaida hawa waathirika; maana kuna wengine wametoa vifaa,wengine hela, wengine vifaa vya ujenzi;

sioni haja ya mkuu wa kaya kunyoosha mdomo kati michango imetolewa ya kutosha tu;
isitoshe cjaona mkono wa serikali hapo,
Uko sahihi kabisa. Huu si wakati wa mkuu wa kaya kunyoosha mdomo.
Kwanza kabisa wanaKagera ni wachapakazi, wala si watu wa kubweteka (achilia mbali kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ya mkuu wa kaya). Mkuu wa kaya analijua hilo, analijua sana.
- Huu ulikuwa ni mkoa uliokuwa umejaliwa neema ya maliasili na pia malijamii lakini Muumba mwenyewe ndiye anajua kwa nini ameusukumia majanga, janga juu ya janga. Mkuu wa kaya analijua hili.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa mzalishaji mkuu wa zao la kahawa tokea kilimo cha biashara kilipoletwa na wakoloni. Hadi leo hii kuna kiwanda cha kusindika kahawa lakini zao la kahawa soko lake la dunia limedorora.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa na chama kikubwa cha ushirika - BCU - kilichosimamia uzalishaji, ununuzi, na uuzaji wa zao la kahawa. Kabla ya Mwalimu JKN kufuta vyama vya ushirika vilivyokuwa vimefanikiwa sana, BCU iliweza kufadhili watoto wa wakulima kwenda kusoma shule za private za Uganda na Kenya na hata masomo ya utaalamu ughaibuni.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa, na bado, unazalisha zao la chai japo kwa kiwango kidogo. Hadi leo hii kuna shamba kubwa la chai na kiwanda cha kusindika chai pale Maruku.
- Mkoa wa Kagera umekuwa mzalishaji mkuu wa zao la miwa na hivyo kuwepo kiwanda cha sukari cha Kagera. Majeshi ya Idd Amin yalikibomoa lakini kiliweza kujengwa upya na kimeendelea kuzalisha.
Hii mifano michache ya ukulima wa mazao ya biashara (kahawa, chai, na sukari) ni ushahidi wa kutosha kuwa wana wa Kagera hawabweteki, hawajawahi kubweteka. mkuu wa kaya analijua, tena sana.

Mkuu wa kaya anajua vizuri sana kuwa mkoa wa Kagera umekumbwa na mfululizo wa majanga (ya asili na ya kijamii) pengine kuliko sehemu nyingine yo yote ya Tanzania na matokeo yake umeporomoka kutoka mikoa iliyokuwa na ukwasi na kujiunga na mikoa fukara:

1. Itikadi ya ujamaa iliua BCU - chombo kilichokuwa kikisimamia kwa ufanisi uzalishaji na uuzaji wa kahawa.
2. Kana kwamba hiyo haitoshi, soko la kahawa duniani nalo likadorora - uzalishaji wa kahawa ukafifia.
3. Vita ya Kagera ya 1978. Vidonda vyake vipo hadi leo
4. UKIMWI - miaka ya mwanzoni mwa 80 Kagera ilikuwa lango kuu ulipoingilia UKIMWI. Vidonda vyake bado vipo hadi leo.
5. Ajali ya MV Bukoba.
6. Ugonjwa wa Mnyauko umeteketeza migomba yote- zao kuu la chakula na rubisi - lililowezesha watu kujikimu na wakati huo huo kudumisha utambulisho wa utamaduni wao. Zamani hizo ilikuwa ni aibu kwa Mhaya kujulikana amekula ugali. Lakini myauko ulipopiga hodi, wamekubali hali halisi na leo hii ni walimaji wakubwa wa mahindi na ugali umegeuka kuwa chakula kikuu.

Majanga ni mapenzi ya Mungu. Mkuu wa Kaya anajua wanaKagera hawawezi kubweteka wala kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ijapokuwa wanayo haki ya kikatiba kupewa huduma za dharura na serikali yao kwa sababu wanalipa kodi. Mkuu wa Kaya ameshauriwa vibaya, au kama amejishauri basi inabidi ajitafakari na ikibidi atafute fursa nyingine atumie lugha ya kuwafariji wahanga.
 
Kwahyo akae tu? Huku kutafuta hema pia sio kazi? Hv kila mkoa ukipata tetemeko nyumba zikabomoka serikali itajenga? Nyumba za kahama mvua ya mawe, ss hv tetemeko, ije mvua, serikal ina uwezo huo?
Suala sio uwezo suala ni lugha inayotumika.
 
Right, Rais ana kauli chafu. Kawaita watu shetani, wanafunzi ******, akiwa Unguja kasema tuwatumbukize watu kwenye visima vya maji, tutoboe matairi ya magari ya watu, kawananga wahanga wa tetemeko kwamba wamedhani tetemeko linaletwa na serikali as if ni wapumbavu kupita kiasi....
Magufuli angekuwa mchangiaji wa JF angefutiwa post zake nyingi na kufungiwa, amejawa na uchochezi, dhihaka, fighting words na matusi, hajui ustaarabu, hakosolewi, haheshimu Raia. Rais gani duniani anaongelea jukwaani style anazofanya mapenzi na mkewe?
Hatuheshimu na hajiheshimu, anategemea majeshi kumlindia heshima yake. We never probed his temperamental fitness to be head of state, now he has plunged the country into quasi dictatorship.
Maana ake msisubiri serikali iwajengee nyumba ndo mana kasema tetemek halijaletwa na serikali, ni ajali km ajali ngingine tu, leo hii nyumba za sehem fulan ziungue pia mtataka serikal iwajengee? Kashasema atasaidia paliposhindikana, mnataka aseme nini? Au atoe ahad ambazo hatoweza kutekeleza? Kuna watu pia walishaanza kulalamika kuwa serikal haikuweza kutabiri juu ya ujio wa tetemeko, magu anajua anachoongea, ttzo mna negative mind kila kitu mnakitafsiri kinegative tu, ukiniambia hakuwa sawa kutokwenda bukoba nitakuelewa ila ktk hiyo speech sijaona ubaya,
 
Lakini afadhali kawaeleza ukweli ingawaje mchungu. Nafikiri kipindi hiki watu watatia akili tu.

Leo wameguswa wana Kagera, kesho ni zamu ya wengine kila mtu ataguswa kwa wakati wake. Wewe shangilia utadhani wanakagera wamenunua tetemeko dukani.
 
Mi nadhan haya maneno kayaongea indirectly ndani kabisa ya moyo wake wala hakuwalenga zaid wananchi wa kagera itakuwa kuna watu kawafikishia ujumbe ili wazid kukasirika
 
Kujaza kwenye post yako maneno kama Hovyo hovyo na ******** hakukusaidii chochote katika kufikisha ujumbe wako!
Mtu wa hovyo hovyo anastahili aitwe wa hovyo hovyo!Sina neno mbadala

Unamshangilia Rais ambaye hata kuwqjulia hali wapiga kura wake hawezi?Wamekufa zaidi ya watu 15 hajaenda!Anataka wafe wangapi ndiyo aende?

Akina mama na watoto na wazee wanalala migombani BK lkb ww una m support Rais asiye jali raia wake

Shame on you!
 
Uko sahihi kabisa. Huu si wakati wa mkuu wa kaya kunyoosha mdomo.
Kwanza kabisa wanaKagera ni wachapakazi, wala si watu wa kubweteka (achilia mbali kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ya mkuu wa kaya). Mkuu wa kaya analijua hilo, analijua sana.Majanga ni mapenzi ya Mungu. Mkuu wa Kaya anajua wanaKagera hawawezi kubweteka wala kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ijapokuwa wanayo haki ya kikatiba kupewa huduma za dharura na serikali yao kwa sababu wanalipa kodi. Mkuu wa Kaya ameshauriwa vibaya, au kama amejishauri basi inabidi ajitafakari na ikibidi atafute fursa nyingine atumie lugha ya kuwafariji wahanga.
Umeisikiliza speech yote? Au ndo hii ya kutafsiriwa kinegative negative? Muwe mnaelewa before comenting chchte, hiyo mifano inafananaje na alichokiongea rais?
 
Hebu niambie lugha gani mbaya hapo katumia?

Unadhani alikuwa na sababu yakuyasema haya? Alikuwa anawajibu wale wanoilalamikia serikali kuwa imechelewesha misaada. Kuna maana gani kumjibu mhitaji? Mwenye shida, mtu aliyepotelewa kila kitu. Tatizo liko hapo.
 
Mpaka sasa Serikali imetoa shilingi ngapi?
Hata senti 1
Kaenda kwa akina Mengi alio wakashfu kuwa yy ni Rais wa maskini

Lkn hqo ho maskini anao sema ndiyo anawatetea wamekufa wengi BK na hajaenda!Sijui maskini gani huwa anawazungumzia
 
Leo wameguswa wana Kagera, kesho ni zamu ya wengine kila mtu ataguswa kwa wakati wake. Wewe shangilia utadhani wanakagera wamenunua tetemeko dukani.
Rais kaongea ukweli, mkiongea suala la kutokwenda kwakweli rais km rais hayuko sawa, tulitakiwa kumuona akiwa kule, ni faraja tosha tu, lakini kwa speech sijaona ubaya
 
downloadfile-5.jpeg
 
Back
Top Bottom