kwa MAWAZO yangu kidogo niliyokuwa nayo; hizo michango ya watanzania na wengine ambayo imekadiriwa kuwa 2.3 billions inatosha kabisa kuwarudisha katika hali ya kawaida hawa waathirika; maana kuna wengine wametoa vifaa,wengine hela, wengine vifaa vya ujenzi;
sioni haja ya mkuu wa kaya kunyoosha mdomo kati michango imetolewa ya kutosha tu;
isitoshe cjaona mkono wa serikali hapo,
Uko sahihi kabisa. Huu si wakati wa mkuu wa kaya kunyoosha mdomo.
Kwanza kabisa wanaKagera ni wachapakazi, wala si watu wa kubweteka (achilia mbali kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ya mkuu wa kaya). Mkuu wa kaya analijua hilo, analijua sana.
- Huu ulikuwa ni mkoa uliokuwa umejaliwa neema ya maliasili na pia malijamii lakini Muumba mwenyewe ndiye anajua kwa nini ameusukumia majanga, janga juu ya janga. Mkuu wa kaya analijua hili.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa mzalishaji mkuu wa zao la kahawa tokea kilimo cha biashara kilipoletwa na wakoloni. Hadi leo hii kuna kiwanda cha kusindika kahawa lakini zao la kahawa soko lake la dunia limedorora.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa na chama kikubwa cha ushirika - BCU - kilichosimamia uzalishaji, ununuzi, na uuzaji wa zao la kahawa. Kabla ya Mwalimu JKN kufuta vyama vya ushirika vilivyokuwa vimefanikiwa sana, BCU iliweza kufadhili watoto wa wakulima kwenda kusoma shule za private za Uganda na Kenya na hata masomo ya utaalamu ughaibuni.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa, na bado, unazalisha zao la chai japo kwa kiwango kidogo. Hadi leo hii kuna shamba kubwa la chai na kiwanda cha kusindika chai pale Maruku.
- Mkoa wa Kagera umekuwa mzalishaji mkuu wa zao la miwa na hivyo kuwepo kiwanda cha sukari cha Kagera. Majeshi ya Idd Amin yalikibomoa lakini kiliweza kujengwa upya na kimeendelea kuzalisha.
Hii mifano michache ya ukulima wa mazao ya biashara (kahawa, chai, na sukari) ni ushahidi wa kutosha kuwa wana wa Kagera hawabweteki, hawajawahi kubweteka. mkuu wa kaya analijua, tena sana.
Mkuu wa kaya anajua vizuri sana kuwa mkoa wa Kagera umekumbwa na mfululizo wa majanga (ya asili na ya kijamii) pengine kuliko sehemu nyingine yo yote ya Tanzania na matokeo yake umeporomoka kutoka mikoa iliyokuwa na ukwasi na kujiunga na mikoa fukara:
1. Itikadi ya ujamaa iliua BCU - chombo kilichokuwa kikisimamia kwa ufanisi uzalishaji na uuzaji wa kahawa.
2. Kana kwamba hiyo haitoshi, soko la kahawa duniani nalo likadorora - uzalishaji wa kahawa ukafifia.
3. Vita ya Kagera ya 1978. Vidonda vyake vipo hadi leo
4. UKIMWI - miaka ya mwanzoni mwa 80 Kagera ilikuwa lango kuu ulipoingilia UKIMWI. Vidonda vyake bado vipo hadi leo.
5. Ajali ya MV Bukoba.
6. Ugonjwa wa Mnyauko umeteketeza migomba yote- zao kuu la chakula na rubisi - lililowezesha watu kujikimu na wakati huo huo kudumisha utambulisho wa utamaduni wao. Zamani hizo ilikuwa ni aibu kwa Mhaya kujulikana amekula ugali. Lakini myauko ulipopiga hodi, wamekubali hali halisi na leo hii ni walimaji wakubwa wa mahindi na ugali umegeuka kuwa chakula kikuu.
Majanga ni mapenzi ya Mungu. Mkuu wa Kaya anajua wanaKagera hawawezi kubweteka wala kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ijapokuwa wanayo haki ya kikatiba kupewa huduma za dharura na serikali yao kwa sababu wanalipa kodi. Mkuu wa Kaya ameshauriwa vibaya, au kama amejishauri basi inabidi ajitafakari na ikibidi atafute fursa nyingine atumie lugha ya kuwafariji wahanga.