Honorable GPA
Senior Member
- Mar 31, 2019
- 149
- 223
Just imagine upo katika kipindi cha majonzi una tafakari hili na lile baada ya kukosekana kwenye ajira! unaulizwa maswali kama haya na wazazi, ndugu na majirani;
Nasikia ajira zenu zimetoka. Vipi sasa umefanikisha? Unajibu sijafanikisha.
Anaendelea kuuliza, kwanini sasa au hukutuma maombi? Unajibu, maombi nilituma ila imetokea bahati mbaya sijafanikisha. Anauliza tena, mbona wengine wamepata wewe umekosaje? Unashindwa hata ujibu vipi hili swali ila kwakuwa umeulizwa unaamua kujibu kwamba mpangaji ni mwenyezi Mungu huenda hakuamua niwemo kipindi hiki alafu pia yale ni maombi kwahiyo kupata au kukosa ni sehemu ya matokeo.
Kiufupi tu! Ni kwamba ajira zinapotoka wazazi wetu wanaamini kwamba utapata. Sasa inapotokea kama hivi hujapata imani yao kwako inapungua wanaanza kufikiria labda ulifeli shule ila unaficha ndio mantiki ya kuulizwa maswali kama hayo!
Ukiachana na wazazi, jamii ndio kabisaa ukikosa ajira wanakuona si lolote si chochote. Just imagine mtu anakuuliza, umekosa ajira kwahiyo utaishije?
Wengine jinsi ajira hizi zinavyotoka wanaamini una ufaulu mdogo ndio maana umeachwa. Wengine wanasema badala ya kwenda chuo kusoma wewe ulienda kuendekeza umalaya matokeo yake chuo ulifeli ona sasa wenzako wameajiriwa wewe upo upo tu!
In fact vijana tunapitia kipindi kigumu sana. Kudharaulika kwingi, kuseng'enywa kwa sana, kusimangwa ndio usiseme.
Tunaomba mheshimiwa Rais utunusuru na masimango haya. Pamoja na kazi kubwa unayoifanya ya kulipeleka taifa letu mbele pia tukumbuke na sisi vijana wako tunanyanyasika sana mitaani!. Kwenye ajira 13000 ulizosema ni 8000 tu zimetoka, sema japo neno ili 5000 zilizosalia nazo zitoke angalau zitasaidia kupunguza idadi ya vijana wengine mtaani.