Rais Magufuli tunusuru vijana wako tunapitia kipindi kigumu

Serikali haiwezi kupunguza idadi ya Ufahili katika kada ya ualimu, kwasababu bado walimu hawatoshi nchini, kilichopo ni serikali kutokuwa na msuli wa kutosha wa kuajili, pia na upungufu wa sector binafsi. Kutokana na uchumi kubana.
 
Asante , member muongo!

Na iwe ivo.
 
Mie pia tatizo hili limenikumba ni mwalimu niliyehitimu SAUT ya Mwanza mwaka 2016,hili tatizo lilipoanza kutokea mwaka 2015 nilikuwa nasoma huku nawaza nikimaliza naenda kukabiliana nalo vipi kitaani ila sikuweza kupata majibu ya moja kwa moja cz unakuwa frustrated sana,baada ya kuhitimu nilikaa nyumbani kama miezi 3 hivi hali ikiwa ni mbaya sana mpaka ikafikia hatua hadi hela ya vocha au kuangalizia mpira naomba kwa mama au wadogo zangu kiukwl nilikuwa naumia sana
Kuna siku nimekaa gheto usingizi haukuja kabisa nikiwaza hii hali mpka lini?,ndipo hapo nilipoamua kujipa ujasiri wa kuingia kitaa kupambana na kuweke vyeti vyangu kabatini,kuacha kuona aibu kwa jamii kwamba itanionaje msomi mzima nafanya kazi za namna hii.
Ndugu zangu niliamua kutafuta fani ambayo ni fundi umeme wa majumbani,jamaa niliyempata wa kunifundisha alikuwa mwanafunzi mwenzangu aliferi form 4 akawa ndo boss wangu kuanzia hapo,nikawa saidia fundi kwa namna moja au nyingine wakati huo naendelea kujifunza
Baada ya miaka 2 hivi nikiwa na idea tayari ya ufundi umeme nikaamua kujifunza ufundi bomba(plumbing) ,mpaka sasa nimeiva napata site zangu maisha yanasonga siwazi tena ajira za magufuli cz nw naingiza fedha zinazokidhi mahitaji yangu na familia yangu sina stress tena
Ndugu zangu wasomi tuache kudharau kazi cz unaweza ukaona kazi flani ni za kijinga kumbe watu wanapiga hela nyingi sana kwenye hizo kama hasa kazi za ufundi like kujenga,ufundi umeme,welding etc,
Mwisho kama unaona hauna mtaji,wala hauna connection yoyote ya kukupatia ajira nakushauri tafuta fani(ujuzi)wowote utakusaidia sana nyakati hizi tulizonazo hauta kufa njaa popote uendapo
 
Akaishi wapi mkuu, atafikia wapi, Kodi ataliapaje, kula je? Madawa nk...mkuu yataka moyo Sana

Basi mpe mbinu aanzaje

Yeye atoke tu nyumbani hapo ndio pakuanzia.

Kula
Kulala
Huduma

Hivi vitu vitatu atavitafuta akishatoka nyumbani. Tofauti na hapo hakuna namna atulie
 
Una point ya muhimu sana bro.
 
Nipe Siri mkuu, maana nimefanya michongo mingi imefeli, napata hela ya kusurvive tu! Dah! Nikiri tu nlisoma ili niajiriwe niweze kujiajiri, Mana mtaji pia ni vigumu Sana kupata

rahisi sana, engange na watu waliofanikiwa one to one! but make sure your willing to sacrifice yourself
 
Kwa madudu yaliyo ibuliwa sina hamu tena na database bora kuomba upya mkuu
 
Kuna watu wanaongea kirahisi humu nadhani hawajui wanachokipitia vijana wenzao.
Hao ni wachache kati ya wengi wanaofurahia hizi shida tunazopitia! Kuna mwingine hadi alidiriki kunitamkia kwamba Magufuri asiendelee kuwaajiri hivo hivo ili tulingane maana mlijifanya kuipenda sana shule sasa mtaa umewapenda zaidi!

ila yote kwa yote naamini ni mapitio tu tunapita ipo siku yatakwisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…