Rais Magufuli, tusaidie kampuni ya SKOL Building Contractors LTD itulipe mishahara na NSSF

Rais Magufuli, tusaidie kampuni ya SKOL Building Contractors LTD itulipe mishahara na NSSF

Tata Omturya

Member
Joined
Mar 20, 2020
Posts
12
Reaction score
11
Hiki ni kilio chetu wafanyakazi cha zaidi ya mwaka mmoja tangu kuanza kufuatilia suala hili bila mafanikio katika ofisi zifuatazo:-

(1) Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

(2) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

(3) NSSF-Kinondoni

(4) Vyombo vya habari vya binafsi na serikali (Shirika letu pendwa la utangazaji).

Ikumbukwe kampuni hii imekuwa ikilipokea malipo ya fedha nyingi (IPC) toka katika taasisi mbalimbali; lakini madai yetu yamekuwa yakipuuzwa.

Mheshimiwa Rais Magufuli; Mkombozi na Mtetezi wa wanyonge nchini Tanzania, natumaini utatuokoa katika kilio hiki cha muda mrefu.
 
Huyu JPM lini awe na huruma kaachisha watu masikini ajira watumishi wengi wanalia hamna nyongeza likizo nk aje akusaidie wewe.
 
Kuna wazee wa TZR na URAFIKI wana miaka kumi na tano sasa.
 
Hivi hii kampuni si ndio ya yule jamaa aliyezimia baada ya kupigwa biti na Jafo??

 
Back
Top Bottom