Rais Magufuli tusaidie Wananchi tunaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Iringa. Tanroads wanatusumbua sana kutulipa fidia ya mali zetu

Rais Magufuli tusaidie Wananchi tunaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Iringa. Tanroads wanatusumbua sana kutulipa fidia ya mali zetu

Mantombazane

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2014
Posts
579
Reaction score
367
Mheshimiwa Rais tumehangaika mapaka tumeona tukuandikie kupitia jukwaa hili utusaidie sisi wanyonge wa kijiji cha Igingilanyi ambao tumetakiwa kuhama ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli uliopo katika manispaa ya Iringa.

Baada ya kuelimishwa wananchi hatukuwa na pingamizi la mradi huu tukaanza kuondoa mali zetu na kuruhusu kuhamishwa kwa makaburi hata kabla ya kulipwa fidia yote tunayo stahili. Kwa upande mwingine serikali kupitia Tanroads waliahidi kutulipa haki zetu bila usumbufu wowote. Cha ajabu baada ya tathmini kufanyika baadhi ya wananchi walipunjwa fidia zao na kuamua kudai na kuahidiwa kulipwa mapunjo. Lakini kwa kuwa mradi unatakiwa uendelee baadhi ya wananchi waliamua kuondoka katika maeneo yao hata kabla ya muda walipewa ili kumpa nafasi mkandalasi kuendelea na kazi

Kibaya kinacho tuuma ni kuwa pamoja na kupewa fidia kiduchu kwenye nyumba zetu lakini mpaka sasa TANROADS ambao ndio wasimamizi wa mradi huu hawajatulipa fidia baadhi yetu. Kazi imekuwa kila siku kwenda Tanroads utadhani wanafunzi wanaenda shuleni hivyo kutupotezea muda wetu wa kuzalisha mali hasa wakati huu wa kilimo. Tukifika hapo tuna kutana na afisa anaye itwa Mgongolwa ambaye kila siku ana tupa ahadi za kutukera tu mpaka tumekuwa na hasira naye sana.

Katika kuhangaikia hilo tumefika mpaka kwa viongozi wetu lakini hawajaonesha kutujali wala kutusaidia zaidi ya wao nao kutupa maneno matupu yasiyokuwa na maana yoyote kwa maendeleo ya maisha yetu. DC ameshindwa kabisa hata kufika kuongea na wananchi ingawa hayuko umbali wa zaidi ya km 20 Lakini utashangaa anawasha shangingi kwenda kukamata eti bajaji iliyozidisha abiria mmoja na kurusha picha mtandaoni kutafuta kiki. Mkuu wa mkoa naye utafikiri katiwa Supa glue kajifungia mjini hapo wakati anaweza hata kutembea kwa miguu mpaka hapa Tanroads kufuatilia haki za wananchi.

Mbunge wetu Lukuvi naye tumewasiliana naye haoneshi kuguswa na shida yetu yeye zaidi atasema ninyi daini Tanroads wamepewa hela ya kutosha kuwalipa fidia zetu. Sasa unajiuliza kama Tanroads wamepewa pesa za kutosha na yeye ni waziri anashindwaje kufika na kufuatilia matatizo yetu? Lakini utamsikia akizunguka huko na huko akitatua migogoro ya ardhi lakini jimboni kwake hajali maana ameona huku ni wajinga kila akija ana nyeyekewa.

Kutokana na shida hiyo baadhi ya wananchi wameshindwa kujenga na kumalizia nyumba zao hivyo kuhangaika kila siku kufuatilia kwenye ofisi za serikali. Hivi fikiria eti leo serikali inayojiita ya wanyonge inatoa fidia ya nyumba ya milioni 3.5 nyumba ya tofari za kuchoma! Huyu mwananchi aliyehangaika miaka yote kujenga nyumba yake anaanze kujenga nyumba mpya? Kuna ambao nyumba zimekwamia kwenye lenta na wengine hawajaanza kabisa kutokana na kuzungushwa sana na Tanroads. Hata wale waliojenga wengi wametumia fidia za mashamba na mazao kujenga nyumba zao lakini ukweli fidia za nyumba zilikuwa ni kichekesho licha ya ahadi kuwa wangelipa vizuri.

Kwa kuwa mheshimiwa rais umetangaza mara nyingi kuwa serikali ina hela za kutosha na wananchi wasiondolewe katika maeneo yao bila kulipwa kwanza tunaomba utusaidie kufuatilia kuna nini Tanroads Iringa hadi kusumbua waathirika kuhusu haki zao. Yaani hawa maafisa wa Tanroads hapa Iringa wamejigeuza Miungu watu kuwa wao ndio wenye pesa kiasi walipe kadiri wanavyojisikia wao. Sasa hivi tupo katika msimu wa kilimo tuna hitaji kuwa mashambani zaidi kuliko kuzunguka kila siku Tanroads kufuatilia haki zetu.

Tuna imani kupitia jukwaa hili ujumbe wetu utafika kwako na kwavionozi husika wakiwamo wa Tanroads taifa na waziri wao wa ujenzi kwakweli tumechoka na manyanyaso ya Tanroads hapa Iringa. Tuanaamini Serikali haiwezi kuanzisha mradi kubwa kama huu halafu ishindwe kulipa fidia kidogo kabisa kwa wanakijiji masikini. Kinacho fanyika hapa Iringa ni kutaka kudhulumu haki za wananchi tu ili wakate tamaa wao watie mfukoni pesa za wananchi.

Asante
 
Mkuu mliwachagua CCM? Kama mmewachagua wafuateni muende mguu nao kwa mguu huko Tanroads. Wasipowapa ushirikiano wowote jueni mmeliwa na mjifunze kuchagua.
 
Mkuu mliwachagua ccm? Kama mmewachagua wafuateni muende mguu nao kwa mguu huko Tanroads. Wasipowapa ushirikiano wowote jueni mmeliwa na mjifunze kuchagua.
We ulitaka wamchague nan
 
Poleni sana,hapo mnapopeleka malalamiko yenu mmepotea,hamtalipwa.
 
Mkuu mliwachagua ccm? Kama mmewachagua wafuateni muende mguu nao kwa mguu huko Tanroads. Wasipowapa ushirikiano wowote jueni mmeliwa na mjifunze kuchagua.
Wakikosa ushirikiano wajue kuwa walidangangwa wakaacha betri wakachagua gunzi,hivyo wakati mwingine wajifunze kuchagua na kukataa kudanganywa.
 
Back
Top Bottom