Rais Magufuli, ulipotaja kuwa umezalisha ajira milioni 6 huoni kuwa unanidanganya hata mimi?

Jiwe alidanganya mambo mengi ikiwemo kudai kuwa biashara ya nje kwenye utawala wake imekua kuliko alivyoikuta mwaka 2015 wakati JK anaondoka, kiukweli ni kwamba biashara ya nje imeendelea kuporomoka, kavuruga korosho, exoorts zetu zimezidi kushuka siku baada ya siku halafu Jiwe anasimama mbele ya kadamnasi na kudanganya umma.

Takwimu zote zipo za BOT na TRA zote zinaonyesha Sekta ya uzalishaji, na mapato ya Exports yamepungua, ila Jiwe anatupiga Fiksi tu hivi waziwazi kuwa biashara ya nje imeongezeka kwenye utawala wake kuliko kipindi cha JK

Kitu kingine wakati anahutubia bunge juzi pia kajimilikisha Miradi ya JK kuwa ni mafanikio ya awamu yake, kwa mfano nilimsikia akitaja daraja la Kigamboni kuwa ni achievement ya utawala wake, wakati yeye alikwenda kuzindua tu na kila kitu kilishafanywa na utawala uliomtamgulia!
 
Ajira laki tano tu zingeweza leta impact kwenye Jamii.
Tatizo la ajira upimwa kwa kuangalia ongezeko au punguzo la idadi ya machinga.Kama machinga ni wengi uhitaji kujua jibu la ajira ajira milioni 6.
 
Huwezi ukasaomesha watu namba ili uwatawale then ajira ziongezeke hii sayansi ya wapi.Hata Kama ni formula mpya ya uchumi sio correlation kabisa.Kusomesha watu namba ni kuuwa au kupunguza idadi ya ajira.Kama matajiri, wafanyabiashara, wakulima, wavivu,nk wameshughukiwa haswaa wengine Hadi wamekimbiza nje mitaji yao hizo ajira zinaongezeka vipi.
 
Tujuavo takribani ajira milioni 3 zimekufa tangu awamu hii ya dabo standard na kuleta umasikini nchini iingie,wengi wanalimia meno.
 
Ajira zisizo rasmi ndizo uongoza kwa kuingiza pesa nyingi shida wamenyimwa akili ya darasani.Je wajua ukahaba, ombaomba wanaingiza pesa nyingi kwa siku sawa au zaidi ya mwajiriwa wa kiwango cha Kati.
 
Muasisi wa viwanda tanzania ni nyerere, aliyefuata kwa kuhamasisha kwa ukubwa kabisa ni kikwete na ndo matunda tunayoyaona leo 2020 huku jiwe akijisifu vimejengwa awamu yake,

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
Nia ya Nyerere ya kuanzisha viwanda ilikuwa ni nzuri sema alikosa wasimamizi aliwakabidhi mchwa,yaani soma ule SU mabucha yalikuwa wazi kwa mafisi.Asingewafukuza wakoloni angewaomba usawa tu Kama ilivo South Africa Ila anaetaka kuondoka kwa hiari yake ni sawa
 
Ajira zisizo rasmi ndizo uongoza kwa kuingiza pesa nyingi shida wamenyimwa akili ya darasani.Je wajua ukahaba, ombaomba wanaingiza pesa nyingi kwa siku sawa au zaidi ya mwajiriwa wa kiwango cha Kati.
Ndio maana yake, usijifanye msomi ukadharau kuingiza kipato kwa ajira isiyo rasmi. Huyu amedharau na kudhihaki ajira ya wauza barakoa
 
Wadadavue hizo ajira mil. 6, mambo ya kulishana matango pori hauwezi kuwa ustaarabu wa karne hii..
 
Ndio maana yake, usijifanye msomi ukadharau kuingiza kipato kwa ajira isiyo rasmi. Huyu amedharau na kudhihaki ajira ya wauza barakoa
Ajira rasmi za wafunga tai kutumikishwa kwenye kiyoyozi then unastaafu masikini huna cha kurithisha watoto maana hata vyeti avirithiki.
 
Ndugu naona umeanza kulemewa na tarumbeta la vigelegele.likikushinda lishushe tu.Maana raha yakupuliza tarumbeta uwe unaujua wimbo vizuri na kufurahia utamu wake.
 
Huyu bwana alisema,..msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Inaonekana hataki kuwa mpenzi wa Mungu siku hizi.
Tena alisema wakati wa utawala wake,matajiri wataishi kama mashetani,na wote walishangilia.

Tunaona ukweli wa maneno yake,kwamba,walalahoi tunaishi kama masheitwani.

Ahsante JPM
 
Mimi naomba tu nipate list ya hivyo viwanda, unatengeneza nini na viko wapi?

Hakuna mega factories ,bali kuna Sido size zilizoanzishwa toka Bwana Pesa Mbili Mramba.
Mega factories kama Mangula Mechanical Tools,Tanganyika Pakers,Urafiki,Mwatex,General Tyres,n.k vilishakufa.
Viwanda Mama vya kuzalisha Chuma na mkaa vipo drawing board zaidi ya miaka 40.
Viwanda vya kati vilivyotokana na mazao kama mkonge,pamba,korosho,ufuta,ngozi,ambavyo kwa sasa vinapumulia ICU.
Kuna wakati waziri Kangi Lugola akiwa naibu waziri mazingira alikuwa anasaidia sana kuvifunga kana kwamba ana alegi na viwanda.

Viwanda vya Tehama ni sifuri japo gharama zake ni ndogo sana,Kenya na Rwanda wameishaanza Silcon Valley zao,sisi je?
 
Mkuu andiko lako sijapenda kwa nini umeamua kuandika haya leo na juzi ,hii pana sijaipenda kama mkuu anakufaham vizuri na mnafamiana why ulete hapa kwa nini usimfuate ukamnongoneza
Msema kweli ndio mpenzi wa Mungu.
Amen
 
Jifanye mjanja ila jua za mwizi arobaini, huwezi kua na akili kumzidi mkuu wa nchi na haiwezekani unaenda chooni kwa kukulipa sisi bado uje kujitia kidomodomo huku.... Ungekua mwema ungeachia hiyo nafasi yako achukue mtu mwingine, Watch out.[emoji837][emoji837]

Capo Dei Capi
 
Misifa tu,hili daraja lilijengwa kwa fedha za NSSF kila Mara kujisifia nalo.Hizo fedha zilikuwa za wanachama wa mfuko huo,je walizichukua kama mkopo?Wamelipa na riba?
 
Sisi na viwanda wapi na wapi?Tulivyokuwa navyo vilienda wapi awali?Kama hatujatafuta vilipoenda Kilimanjaro Machine Tools,Mang'ula,Mgololo Paper Mills,UFI,ZZK nk hatuwezi kuwa nchi ya viwanda.
CCM iache usanii,hata hiyo Sera hawaiamini wakati ndiyo iliyokuwa main agenda.Wamebadilisha na kuwa nchi ya Bombardier, Boeings,SGR,Stigler,Flyovers, madaraja,barabara kabla hatujakamilisha main agendas ambazo hizi mpya zingefuatia kama outcome ya kuimarika uchumi.
Kuna mwenye Ilani yao tuone kama siyo copy&paste ya 2015/2020.Wanatwist versions ila hawatakuwa na jipya,ni usanii.Wapi 50mil za kila Kijiji?
 
We Jamaa utakua huna unalolijua unapelekwa na akili za kushikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…