Hakuna mega factories ,bali kuna Sido size zilizoanzishwa toka Bwana Pesa Mbili Mramba.
Mega factories kama Mangula Mechanical Tools,Tanganyika Pakers,Urafiki,Mwatex,General Tyres,n.k vilishakufa.
Viwanda Mama vya kuzalisha Chuma na mkaa vipo drawing board zaidi ya miaka 40.
Viwanda vya kati vilivyotokana na mazao kama mkonge,pamba,korosho,ufuta,ngozi,ambavyo kwa sasa vinapumulia ICU.
Kuna wakati waziri Kangi Lugola akiwa naibu waziri mazingira alikuwa anasaidia sana kuvifunga kana kwamba ana alegi na viwanda.
Viwanda vya Tehama ni sifuri japo gharama zake ni ndogo sana,Kenya na Rwanda wameishaanza Silcon Valley zao,sisi je?