Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Leo Rais wetu wa JMT amehudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya mahakama kuu hapa nchini. Kauli mbiu ya kudhimisha miaka 100 ni kujenga nchi inayozingatia haki, udugu na amani katika kuleta ustawi wa jamii.
Mimi binafsi nilitarajia kama mkuu wa nchi ulienda kwenye haya maadhimisho, je unafahamu kuwa unatawala raia ambao haki zao zinaminywa?
Mimi sikutarajia uende hapo kwenye maadhimisho na kuanza kusifia habari za kumaliza mashauri ndani ya miezi sita au mwaka mmoja. Nilitajia uende ukawaeleze Jaji muu, Jaji kiongozi na umma wa Watanzania kuwa raia wengi bado wanaminywa haki zao huku tukiwa karne ya science na teknolojia.
Changamoto kubwa ni polisi kubambikia kesi Wananchi wanyonge huku walio na pesa wakifanya makosa na kupeta uraiani. Jeshi la polisi ambalo halina weledi ambalo kazi yake kubwa ni kupiga na kutesa watuhumiwa kwenye vituo vya polisi, huku baadhi yao sio wakosaji.
Mimi nilitarajia leo hii kama Rais mpenda haki, utangaze kumfuta kazi IGP wa polisi, utangaze kuunda jeshi la polisi la kisasa ambalo halivunji sheria linapopambana na wahalifu huku likitumia mbinu za kisasa.
Nilitarajia uunde tume ya kudumu ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, huku ikiwa na mamlaka ya kukupa wewe amiri jeshi mkuu mapendekezo ya kuwafuta kazi wakuu wa polisi wanaovunja sheria.
Kwa ujumla leo ilikuwa ndio siku ya kurekebisha mfumo mzima wa utoaji haki hapa Tanzania, maana miaka 100 toka kiundwe chombo cha kutetea haki za wanyonge lakini hakuna haki kwa raia wanyonge.