Habari zenu!
Iwapo Rais Magufuli atakwenda kuwapa kombe Simba la Ubingwa 2018, tukio hili litakuwa ajabu ya dunia ama tunaweza kuita kituko cha karne katika soka.
Sisi wadau wa soka tunajua Karia ni mshabiki wa wazi wa Simba, tumshauri tu apunguze mahaba, sijawahi kusikia Rais kuenda kutoa kombe la ligi ya ndani.Kama sio dharau kwa Rais ni nini hii?.
Analeta habari za kuhalalisha eti nao Serengeti boys nao watamkabidhi kombe, upuuzi mtupu. Nilifikiiri wamemtumia Rais taarifa ya kwanini wachezaji wengi wa Taifa stars wanachaguliwa zaidi kutoka timu za Dar, pia wamueleze FIFA imetuma shiling ngapi kuwaajili ya Youth soccer, na kwanini ligi daraja la kwanza haina udhamini,ili awape hata ushauri wa namna ya kufanya.sio haya masinema.
Mimi naamini mngetaka kumualika Rais mgetafuta mechi ya taifa stars ili aone fedheha yetu. Siamini kama Rais atawaitikia ,haya mambo yenu ya kujipendekeza na kutafuta kiki.