Rais Magufuli wapitishe wagombea wa Serikali za Mitaa njia ile uliyopita wewe 2015 vinginevyo hawatakuwa makini

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ninafahamu dhamana ya wizara ya Tamisemi iko direct mikononi mwa Rais Magufuli hivyo ushauri huu nampa akiwa katika nafasi yake ya ukuu wa Tamisemi.

Ni kwamba wagombea wanaobebwa siku zote hawawezi kuwatumikia wananchi hivyo ni heri tukaachana na hii dhana ya kupita bila kupingwa ili tupate viongozi bora.

Ninakumbuka namna wewe binafsi Dr Magufuli ulivyopambana usiku na mchana mwaka ule 2015 na hatimaye ukaibuka kidedea, Naamini changamoto ulizokutana nazo kwenye uchaguzi ule zimekufanya uwe Makini " zaidi " kwenye uongozi wako.

Nakumbuka hata kwenye chaguzi ndogo za ubunge huu utaratibu wa mtu kupita bila kupingwa ulionekana kupitwa na wakati ref Ludewa.

Ni hayo tu kwa uchache

Maendeleo hayana vyama!
 
Kupita bila kupingwa kunaondoa maana halisi ya uchaguzi. Mtu anapitaje bila kupingwa wakati wagombea wenzake wameondolewa. Huyo amepitishwa bila kupigiwa kura na siyo bila kupingwa.
Yes, maana kupita bila kupingwa ni ama fomu kachukua mtu mmoja tu au waliochukua fomu wamejitoa ili kumuunga mkono mmoja wao pekee!
 
Tayari kaishawapitisha njia hiyo kwani hujaona wagombea wote walioshindwa kujaza form wameenguliwa ili kipindi kingine akili ziwakae sawa? Viva JPM
 
Aaah mnataka aonekane Masihi sio?

Yaani ionekane tatizo limetengenezwa na TAMISEMI kupitia watendaji wa Kata na Vijiji halafu Magufuli aje kulitatua!

Tanzania bhna maisha yake yanafurahisaha sana, hata kwenye kikotoo alionekana shujaa, ingawa wenye akili timamu tunawaona tu na Sarakasi zenu.
 
Ahaaa ahaaa, Magufuli ndio kavuruga uchaguzi akiamini ataweza kuturudisha wananchi wote kuwa misukule ya ccm eti kisa kanunua ndege. Huko atabaki na wasiojitambua na hao wanaotegemea madaraka yake kula maisha.
 
Ninafahamu dhamana ya wizara ya Tamisemi iko direct mikononi mwa Rais Magufuli hivyo ushauri huu nampa akiwa katika nafasi yake ya ukuu wa Tamisemi.

Ni kwamba wagombea wanaobebwa siku zote hawawezi kuwatumikia wananchi hivyo ni heri tukaachana na hii dhana ya kupita bila kupingwa ili tupate viongozi bora.

Ninakumbuka namna wewe binafsi Dr Magufuli ulivyopambana usiku na mchana mwaka ule 2015 na hatimaye ukaibuka kidedea, Naamini changamoto ulizokutana nazo kwenye uchaguzi ule zimekufanya uwe Makini " zaidi " kwenye uongozi wako.

Nakumbuka hata kwenye chaguzi ndogo za ubunge huu utaratibu wa mtu kupita bila kupingwa ulionekana kupitwa na wakati ref Ludewa.

Ni hayo tu kwa uchache

Maendeleo hayana vyama!
Tatizo mnajipendekeza kwa MTU msiyemjuwa vizuri.

Jimbo LA Chato kwa miaka 10 mfululizo mgombea ubunge wake alikuwa anapita bila kupingwa.

Bwana huyu aliwahi kugombea jimbo LA Biharamuro na kupigwa chini na mgombea wa upinzani Phares Kabuye, tangia hapo bwana huyu swala LA sanduku LA kura halitaki kabisa na ndio msingi wa kuwachukia wapinzani, walimpa fedhea sana miaka 25 iliyopita.
 
Back
Top Bottom